Monday, March 31, 2008

Chameleon jambazi


Mdau huyo (jina tunalo), aliliambia gazeti hili wikiendi iliyopita kuwa Chameleon ni jambazi wa kazi za wasanii wenzake na kuongeza kwamba ameshajitengenezea pesa nyingi kwa wizi, hivyo Watanzania wanatakiwa kumuogopa.

Alisema, kitendo cha Watanzania kuendelea kumpenda mwanamuziki huyo raia wa Uganda na kununua kazi zake, wakati alimuibia ala (beats), Mtanzania mwenzao, Joseph Haule ‘Profesa Jay’ ni sawa na kukosa uzalendo.

“Chameleon hana ubinadamu, alichomfanyia Profesa Jay hakikuwa kitu cha kiungwana hata kidogo, unajua ile ‘beat’ aliyomuibia ilimuingizia shilingi ngapi za Kiganda? Alimkumbuka mwenzake?” Alihoji mdau huyo.

Aliendelea kusema, pamoja na kuiba beat ambayo aliitengenezea wimbo na kujiingizia mamilioni ya shilingi, Chameleon alifanya kiburi kwa kukaa kimya bila kutoa kauli yoyote, wakati Profesa Jay alipokuwa akilalamika kuibiwa.

Aliongeza, licha ya kufanya kiburi, bado msanii huyo alianzisha ‘bifu’ na Jay katika ugomvi ambao chanzo ni yeye kumuibia mali yake.

“Ugomvi huo, uliisha pale Jay alipokwenda Uganda. Alimtafuta Chameleon na alipoonana naye, alimuambia hana bifu naye, halafu alitunga wimbo wa Ndivyo sivyo ambao waliimba pamoja.

“Baada ya kurekodi wimbo huo, Chameleon aliusajili kama wake, wakati mtunzi ni Jay na ndiye aliyeandika mashairi. Kwa sasa jumuiya za kimataifa zinatambua wimbo ni wa Chameleon,” alisema mdau huyo.

Alifafanua kuwa hivi karibuni msanii huyo alipewa tuzo kupitia wimbo huo wa Ndivyo sivyo, wakati mtu ambaye aliistahili ni Profesa Jay kwakuwa ndiye aliyefanya kazi kubwa.

Hata hivyo, mdau huyo aliwataka wasanii wa Kitanzania kuamka, kuzisajili nyimbo zao na kuzipatia haki miliki ili wapate utetezi pale watakapoibiwa na wenzao wenye nguvu kuliko wao.

Wimbo wa Profesa Jay ambao beat yake iliibiwa na Chameleon unaitwa Nikusaidieje ambao mkali huyo wa Bongo Flava aliufyatua mwaka 2005.

Msondo


Mnenguaji wa bendi ya Msondo Musica Mama Nzawisa akiwapagawisha mashabiki katika onyesho la bendi hiyo lililofanyika jana usiku katika ukumbi wa Africenter uliopo Ilala jijini Dar es salaam.

Papaa Musofe


Pedeshee maarufu jijini Dar es Salaam “Papaa Msofe" (katikati) akimwaga pesa katika jukwaaa la Akudo Impact Msasani Beach jijini DSM (Picha na Richard Bukos)

Muuza Kahawa


Bongo pamoja na jua kali lililopo lakini watu vijiweni kahawa na kashata kama kawa

Fumanizi






Tukio hilo lilichukua nafasi Jumatano iliyopita (Machi 26), saa 6:15 mchana kwenye nyumba ya kulala wageni yenye jina la Timova Bar & Guest House, iliyopo Mbezi Mwisho, jijini.

Jopo la waandishi wetu, lilikuwepo kamili kushuhudia ‘muvi’ hiyo na lilifika mapema eneo la tukio, kwakuwa lilijulishwa siku mbili kabla, kuhusu kuwepo kwa mkakati huo wa kumshika mtu ugoni.

Jumatatu iliyopita, mume aliyefumania (jina tunalo), alipiga simu kwenye dawati la gazeti hili, akitaka waandishi wetu kufika Timova Gesti, Machi 26, 2008, saa sita mchana, wakiwa na kamera zao kwa ajili ya kupiga picha za tukio la fumanizi.
Alisema: “Kuna jirani yangu ambaye namheshimu sana, kwa jinsi tulivyo na ukaribu, mimi huwa namchukulia kama kaka yangu, lakini ananifanyia unyama kwa mke wangu, nimemvumilia nimeshindwa, nimeandaa mtego, nataka nimshikishe adabu.”

Baada ya kupata simu hiyo, gazeti hili lilitumia muda wake na kukutana ana kwa ana na mlalamikaji huyo Jumanne iliyopita, ili kupata ‘data’ za kutosha, kuhusu sekeseke hilo.

Katika maelezo yake, mume huyo alimtuhumu Ali a.k.a Ngosha kuwa, kwa muda mrefu amekuwa akimtaka kimapenzi mke wake (jina tunalificha) na kumhadaa kwamba atamfanyia mambo makubwa endapo angemkubalia.

“Mwanzoni mke wangu alikuwa haniambii, alinificha kwa kuogopa kuvunja ujirani wetu, lakini siku chache kabla ya Pasaka ya mwaka huu, Ngosha alivizia mimi sipo nyumbani, akamfuata mke wangu na kutaka kumbaka, tena chumbani kwangu.

“Ilibidi mke wangu afanye ujanja ili ajiokoe, kwa hiyo akafanya kama anamkubalia na kumuomba wapange siku nyingine, wakutane mbali na maeneo ya nyumbani kwetu, jamaa akawa amemkubalia,” alisema mume huyo.

Mtoa habari huyo alifafanua kwamba baada ya Ali Ngosha kukubali wazo hilo, aliiteua Timova kama sehemu muafaka ya kula ‘nanasi kwa nafasi’, pia akaipendekeza Machi 26, 2008 kuwa ndiyo siku ya kukata utepe wa penzi kati yao, mambo ambayo mwanamke huyo aliigiza kuyakubali.

Aliongeza: “Niliporudi, mke wangu alinipa ‘full story’, jinsi alivyoanza kumtongoza miezi miwili iliyopita, alivyotaka kumbaka, mpaka walivyokubaliana wakutane gesti. Nilishtuka sana! Mwanzoni sikuamini, lakini nilipofanya upelelezi wangu, niliamini.”

Habari zaidi ni kwamba siku ya tukio, Ijumaa Wikienda lilitinga kwenye gesti hiyo saa mbili asubuhi, kabla ya kumshuhudia Ngosha akiingia hapo takriban dakika 60 baadaye na kukodi chumba namba tatu.

Saa 6:08 mchana, mwanamke aliyekuwa akimezewa mate na ‘mgoni’ huyo, aliwasili katika gesti hiyo na kuwauliza wahudumu sehemu kilipo chumba namba tatu, kisha baada ya kuoneshwa aliingia ndani.

Dakika saba baadaye, mume mtu alifika akiwa ameongozana na timu ya watu sita na kuvamia chumba hicho, ambapo walimkuta Ngosha akiwa ameshachojoa nguo zote, wakati mwanamke alikuwa amejifunga taulo.


Aidha, habari zinaongeza kuwa baada ya mume mtu na timu yake kuingia chumbani, walianza kumshushia mkong’oto mgoni huyo, kabla ya kumfanyia kitu mbaya kwa kumvalisha shanga mwili mzima.
Hata hivyo, polisi walifika eneo la tukio na kumuokoa Ngosha mikononi mwa timu hiyo yenye hasira.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa Ngosha naye ana mke na watoto wawili (majina tunayahifadhi), pia uligundua kuwa majirani hao baada ya kufika polisi waliamua kusameheana, huku wakipeana onyo kwamba kila mtu asitamani cha mwenzake.

Saturday, March 29, 2008

Usafiri kwa wanafunzi


Weka kigongo sukuma twende ni usafiri kafiri kwa wanafunzi serikali liangalieni tatizo hili

Maji Safi na Salama


Maji Safi na Salama yanapatikana hapa bila gharama yoyote

Hatari


Habari za ndani zinasema kwamba purukushani zilizofanywa na changudoa huyo (kama anavyoonekana pichani ukurasa wa kwanza wa gazeti hili), hasa baada ya kulazimisha kufanya mapenzi kwa nguvu na mwandishi wa gazeti hilo, zilimfikia mkewe ambaye bila kujua mumewe alikuwa kazini, alifungasha virago na kutimkia nyumbani kwao.

Ilielezwa kuwa fujo zilizofanywa na mwanamke huyo, ziliamsha baadhi ya majirani wa nyumba ya tukio, ambapo kati ya hao, wapo wanaomfahamu mwandishi huyo (Jina tunalo) na kuamua kufikisha umbea kwa mke wake.

“Kuna majirani ambao walimtambua mwandishi wa gazeti hilo, hasa ukizingatia kwamba kutoka nyumba iliyofanyika tukio siyo mbali na anapoishi, kwahiyo tunahisi kuna mtu alimpigia simu mke wake,” kilisema chanzo chetu.

Kiliendelea: “Tuliamini kuwa kuna mtu alimpigia simu mke wake kwasababu hakuchelewa kufika eneo la tukio, ingawa alikuta changudoa huyo ameshaondoka.”

Chanzo hicho kiliongeza, mara baada ya mwanamke huyo kufika eneo la tukio, alimvaa mumewe na kumtuhumu kuwa anatamaa, ndiyo maana alimuacha nyumbani na kwenda kuhangaika na machangudoa.

Sambamba na kumporomoshea tuhuma hizo, habari zinadai kuwa mwanamke huyo alidai apewe talaka kwa vile mume wake amemdhalilisha kwa kitendo hicho.

Hata hivyo, chanzo hicho kiliongeza kuwa timu ya waandishi wa Ijumaa Wikienda ambayo ilikuwa pamoja na ‘kachero’ aliyekumbwa na kizaazaa hicho, ilimuelewesha mwanamke huyo ukweli kwamba mume wake hakuwa na nia ya kimapenzi na changudoa huyo, isipokuwa alimchukua kwa minajili ya uchunguzi wa kikazi.

“Aliambiwa kwamba mume wake alikuwa kazini, lakini hakuelewa, badala yake akawa anasisitiza apewe talaka kwa madai kuwa mume wake hafai.

“Usiku huohuo, hakulala nyumbani kwake, badala yake alikwenda kwa rafiki yake. Asubuhi, alirudi nyumbani kuchukua nguo na mizigo mingine, kisha akatimkia kwa wazazi wake, Tandika, Dar es Salaam,” alisema mtoa habari huyo.

Risasi, liliongea na mwandishi anayedaiwa kukachwa na mkewe, ambaye alisema kuwa anafikiria mwanamke huyo anaweza kubadilisha uamuzi wake wa kuondoka, baada ya Gazeti la Ijumaa Wikienda, kutoa habari, inayoelezea ukweli wa tukio hilo, Jumatatu hii.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, mwandishi wake mmoja, usiku wa Ijumaa Kuu, alimnunua changudoa huyo kwa shilingi 7000 kwa lengo la kukamilisha uchunguzi wa kukithiri kwa vitendo vya ukahaba ndani ya Jiji la Dar es Salaam.

Baada ya kumnunua, mchunguzi huyo hakutaka kufanya naye mapenzi, hivyo aliishia kumhoji maswali yanayohusiana na biashara ya ukahaba na changamoto zinazowakumba wao kama wahusika wakuu.

Hata hivyo, mwandishi huyo alimpatia changudoa huyo pesa waliyokubaliana bila kufanya mapenzi, kitendo ambacho kilipingwa na mwanamke huyo, aliyesema hataki kupewa hela ya bure mpaka aifanyie kazi.

Katika kusisitiza hilo, mwanamke huyo alivua nguo na kubaki mtupu, kisha akawa anamlazimisha mwandishi wa gazeti hilo, afanye naye mapenzi.

Pamoja na kulazimisha ngono, mwanamke huyo aliyekuwa amelewa, alifanya fujo zilizoamsha majirani wa nyumba hiyo, iliyopo Kijitonyama, jijini.

MISS ABAKWA


Habari za kuaminika kutoka kwa rafiki wa karibu wa Miss huyo zilisema, kisa cha mrembo huyo kufanyiwa kitu mbaya kilitokana na utapeli alionao kwa wanaume, huku ulevi ukitajwa pia kumwingiza mtegoni.

Ilielezwa kuwa, usiku wa sikukuu ya Pasaka iliyoadhimishwa Machi 23, mwaka huu, ndani ya Ukumbi wa Travetine mrembo huyo alionekana akiwa na kijana mwenye asili ya kiasia akitumia naye kilevi.

“Tulikutana na (anataja jina la rafiki yake aliyebakwa) ukumbini, yeye alikuwa na kaka mmoja mhindi akanitambulisha kuwa ni rafiki yake,” alisema mtoa habari wetu ambaye jina lake linahifadhiwa na kuongeza kuwa hadi anaondoka aliwaacha wakiwa pamoja.

Aliongeza kuwa, siku ya pili usiku alipokea simu kutoka kwa rafiki yake (Miss) iliyomtaarifu kuwa hali yake ilikuwa mbaya na kwamba alihitaji msaada wa mawazo.

Ilielezwa kwamba, baada ya taarifa hiyo ndugu na jamaa walifika nyumbani kwa mrembo huyo na kumuuliza kilichomsumbua lakini kwa aibu alishindwa kuweka wazi kubakwa kwake hadi alipobaki na rafiki zake wa karibu ambao aliwaeleza ukweli.

“Alituambia kuwa alifanyiwa kitu mbaya na vijana wapatao wanne lakini aliyesuka njama hiyo alikuwa ni mtu wake aliyemtaja kwa jina la Hashim, huyo ndiye aliyemlewesha kisha kumpeleka gheto kwa rafiki zake,” kilisema chanzo chetu.

Nakaaya msagaji?


Nakaaya kupitia kipindi cha Friday Night Live cha Luninga ya EATV, Ijumaa iliyopita alisema kuwa uzuri wake unawadatisha watu wa jinsia tofauti, hivyo hashangai wanawake wenzake kumtongoza.

Kabla ya kauli hiyo ya Nakaaya, mtazamaji mmoja mwanamke, alituma ujumbe wa simu ya mkononi (sms) na kusomwa na mtangazaji wa kipindi hicho, Denis Busulwa ‘Sebo’, akieleza jinsi anavyovutiwa na msanii huyo.

Kwa mujibu wa ujumbe huo wa maneno na jinsi ulivyosomwa na Sebo ni kwamba mtazamaji huyo wa kike, alikuwa akivutiwa na Nakaaya kimapenzi.

Mara baada ya kuiona sms hiyo, Sebo alimuuliza Nakaaya kuwa iweje awavutie mpaka wanawake wenzake?
Hata hivyo, msanii huyo alijibu kwamba yeye anawavutia watu wote, kauli ambayo ilitafsiriwa na baadhi ya watazamaji kuwa pengine anapenda ‘hako kamchezo’ ndiyo maana hakuchukia kutongozwa na mwanamke mwenzake.

“Huyu dada naye yumo nini katika mambo hayo, maana jibu lake linaonesha anaona poa tu kutongozwa na wanawake wenzake!” Alisema mtazamaji mmoja, katika baa moja iliyopo Sinza, jijini Dar es Salaam, huku mwandishi wetu akimsikia.

Katika kipindi hicho, Nakaaya alialikwa akiwa na mwenzake Jacqueline Ntuyabaliwe ‘K-Lyn’ pamoja na wanamuziki nguli wa R&B duniani, Wamarekani KCI & Jojo.

Wasanii hao wote, walikuwa wakizungumzia ‘shoo’ ya KCI & Jojo, iliyoandaliwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo ambapo Nakaaya na K-Lyin waliisindikiza katika Ukumbi wa Hoteli ya Movenpick jikjini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita.

Aidha, siku moja baada ya kipindi hicho, habari tulizozipata kutoka kwa rafiki wa Nakaaya zilisema kuwa msanii huyo amekuwa akipigiwa simu na wakati mwingine kutumiwa ujumbe na idadi kubwa ya wanawake wakimtongoza.

Rafiki huyo alisema: “Wanawake wengi wamekuwa wakijieleza eti wanavutiwa na Nakaaya kwa sura yake halisi (natural), umbo, mtindo wake wa kukata nywele fupi na sauti yake.”

Nakaaya ambaye ni dada wa Miss Tanzania na Miss World Africa mwaka 2005-06, Nancy Abraham Sumari kwa sasa ‘anafunika’ katika anga ya burudani kupitia kibao chake cha Mr. Politician kilichobeba jina la albamu yake yenye jumla ya nyimbo 10.

Nyimbo hizo zinazopatikana katika albamu hiyo inayogombewa vilivyo sokoni ni Nervous Conditions, Mr. Politician, Matatizo, New day, Malaika, Iyeyo, Love me, Nyimbo za Uhuru, A town girl na I’m Free

MSHINDI WA BSS


Mshindi wa shindano la BSS Misoji Edward akiwa ameshikilia cheti kabla ya kutangazwa kuwa mshindi katika shindano hilo.

BRICK & LACE WAKIPAGAWISHA


Wanamuziki kutoka Jamaica Brick & Lace wakitoa burudani ya nguvu katika shindano la BSS.

MAFURIKO JIJINI DAR ES SALAAM



Gari hii aina ya Toyota Land cruiser ambayo namba zake za usajili hazikufahamika mara moja ilinaswa na Kamera yetu ikiwa imezimika katikati ya maji,katika makutano ya Barabara za Bibi Titi Mohamed na Morogoro eneo la Akiba Jijini Dar es Salaam,na hilo jingine ni coaster likifanya kazi zake kama kawaida Tanzania,kufuatia mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni (Picha na Christopher Lissa)

Friday, March 28, 2008

Dunia ya Tatu


Baada ya kutamba kwa muda mrefu,wasanii wa muziki wa kizazi kipya,Mandojo na Domokaya au ukipenda “wazee wa magitaa” wameamua kuongeza nguvu kwa kumuingiza kundini msanii ajulikanaye kama Squiza. Na kutokana na ongezeko hilo,wameamua pia kubadili jina lao kutoka Mandojo na Domokaya na sasa watajulikana kama Dunia ya Tatu au D3 wakiwa ni wasanii watatu kama wanavyoonekana pichani.




Wengi mtakuwa mnatambua jinsi ambavyo Mandojo na Domokaya waliwahi kutamba na vibao vyao kama vile Dingi,Wanok nok,Niaje na nyinginezo nyingi.


Wakiwa pamoja hivi karibuni wasanii hao wameiambia BC kwamba wameamua kuongeza nguvu na kubadili jina kwani wameamua kutoka kivingine huku wakiendelea kuweka nakshi miziki yao kwa kutumia magitaa na vyombo vingine.Mpaka hivi sasa wameshatoa single inayokwenda kwa jina We Nenda ambayo hivi sasa wako mbioni kutengeneza video yake.




D3 wanasema hayo yote ni katika maandalizi ya kutoa albamu yao ya kwanza wakiwa kama D3.Kazi zao nyingi hivi sasa wanazifanyia ndani ya studio za 41 Records.BC inawatakia kila la kheri D3.

Muumini amfanya mkewe anywe sumu


Na Imelda Mtema
Mke wa mwanamuziki wa dansi nchini Muumini
Mwinjuma, Chiku Kasika amekunywa sumu kwa nia ya kutaka kujiua, kwa kile kilichodaiwa ni baada ya kunyimwa talaka na mumewe....

Saturday, March 22, 2008

Mchina afumwa!


Sao Tong alikamatwa nyumbani kwake akiwa na viumbe kadhaa wakiwemo kaa na kamba walio hai wakiwa tayari kusafirishwa kwenda nje ya nchi.

Kwa mujibu wa mtoa habari wetu ambaye alishuhudia tukio hilo (jina tunalihifadhi), baada ya kutiwa mbaroni, Mchina huyo alipelekwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay kabla ya kufikishwa katika Mahakama ya Kisutu kujibu tuhuma zinazomkabili.

Akiwa katika Mahakama hiyo, Mchina huyo aliwaacha hoi wananchi waliokuwepo baada kuangua kilio kama mtoto akiomba msaada wa dhamana.

Hatua ya Sao Tong kulia mahakamani hapo, ilitokana na Mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi Nassoro Sisiwayah aliyekuwa akiendesha kesi hiyo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo John Msafiri kumuwekea pingamizi la dhamana.

Ndugu wa Mchina huyo waliokuwa wameongozana naye mahakamani hapo walikuwa na wakati mgumu kutokana na kutojua Kiswahili wala Kiingereza hivyo, kushindwa kuifuatilia kesi hiyo.

Hata hivyo, Sao Tong alikanusha kutenda kosa hilo na kutupwa rumande hadi Aprili 9, mwaka huu kesi yake itakapotajwa tena.

Friday, March 21, 2008

Ray, Johari kuozea jela


Hii ni baada ya wasanii hao kwa mara nyingine tena, kushindwa kuitikia wito wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni – Kinondoni, kufika hapo kusikiliza shauri la madai lililofunguliwa dhidi yao.

Wiki iliyopita mahakama hiyo ilitoa tangazo katika vyombo vya habari, likiwataka wasanii hao kufika mahakamani hapo juzi Jumatano kuanzia saa 2:30 asubuhi ili kusikiliza shauri hilo lililofunguliwa na McDonald Mwakamele.

Mahakama ilifikia hatua hiyo baada ya wasanii hao kukataa kusaini samansi wanazopelekewa, huku wakidaiwa kumtisha karani anayewapelekea.

Baadhi ya mahakimu katika mahakama zilizopo Kinondoni, walipohojiwa kuhusu mwenendo wa kesi hiyo, walisema kitendo cha wasanii hao kukimbia kinawaweka hatarini kwani wanaweza wakafungwa kwa miezi sita kwa kosa la kuidharau mahakama.

“Kitendo hiki cha kutofika mahakamani ni kuonyesha dhahiri wanaigomea mahakama, sisi hatutaki kujua kama wameonewa au vipi tunachotaka waje wasikilize kesi zao kisha wajitetee wawezavyo, sasa kutofika ina maana gani?
“Unajua labda ni utoto unawasumbua maana wanaona kama wanaigiza vile, lakini wajue mahakama haichezewi, huyu Johari ndio hajawahi kukanyaga hata siku moja,” alisema hakimu mmoja.

Ray na Johari wamefunguliwa shauri hilo, ambapo McDonald analalamika kuibiwa filamu yake ya Revenge na wasanii hao, iliyomgharimu zaidi ya Sh milioni 30 na anadai arudishiwe na kulipwa fidia.

Shauri hilo la madai lililopewa na. 370 f 2007, linasikilizwa na Hakimu Mkuu Mkazi Mfawidhi, Kalombola na limeahirishwa hadi Mei 6, mwaka huu.

Kuozea kwao jela kwa wizi kunakuja iwapo hukumu itatolewa bila wao kuwapo mahakamani, adhabu inayoweza kuambatana na dharau zao kwa mahakama kutokana na kuitwa na kukaidi.

Thursday, March 20, 2008

MAIMARTHA


Na Mwandishi Wetu
Mtangazaji maarufu wa Kituo cha Televisheni cha EATV cha jijini Dar es Salaam, Maimartha Jesse, anashutumiwa kuyaweka hatarini maisha ya wanawake wenzake nchini kufuatia kudaiwa kuuza dawa za kuongeza makalio na matiti....

Wednesday, March 19, 2008

Mr. Blue, Dully Skkes Watekwa


Chanzo chetu kilitujuza kwamba vijana hao, walitekwa Alhamisi iliyopita, majira ya saa 10 alasiri katika eneo la Tabata Kimanga, jijini.

Imelezwa kuwa watekaji waliotekeleza tukio hilo, walikuwa na mapanga, visu na silaha nyingine mbalimbali ambapo msanii Mr. Blue alijeruhiwa begani, shavuni na kwenye kiganja cha mkono.

“Blue amekatwa mapanga kwenye shavu, yaani karibu na sikio, begani na katika kiganja cha mkono, ingawa majeraha siyo makubwa sana,” kilisema chanzo chetu.

Aidha, chanzo hicho ambacho ni swahiba wa wanamuziki hao marafiki, kiliongeza kwamba kwa sasa Mr. Blue anatibu majeraha hayo, katika hospitali moja iliyopo Tabata (haijafahamika).

Akisimulia tukio zima lilivyokuwa, mtoa habari wetu, alisema: “Mr. Blue alikuwa akitokea katika mizunguko yake katikati ya jiji na baadaye akaamua kwenda kumsalimia rafiki yake Dully.”

Aliendelea kusema kwamba, Blue akiwa njiani kwenda nyumbani kwa Dully, Tabata Kimanmga, gari lake aina Starlet, lililoandikwa neno ‘Micharazo’ ubavuni, lilizimika ghafla.

Mara baada ya tukio hilo, mnyetishaji wetu alisema kuwa walitokea vijana wapatao tisa ambao walidai wanataka kumsaidia msanii huyo maarufu.

“Mwanzoni wakajifanya wanamsukuma ili gari liwake, lakini baadaye wakamteka na kumuweka chini ya himaya yao, kisha wakaanza kumpekua mifukoni na kwenye gari,” alisema mtoa habari wetu na kuongeza:

“Uzuri kwenye gari, Mr. Blue alikuwa na rafiki yake (jina halijafahamika), yeye aliwahi kumtumia sms Dully ambaye alifika haraka kumsaidia ‘besti’ wake.”

Hata hivyo, imeelezwa kwamba Dully Sykes baada ya kufika eneo la tukio, naye alitekwa na wahuni hao na kuanza kumpekua mifukoni.

Habari zaidi zinaeleza kuwa kabla ya kuingia kwenye mapambano ya kumsaidia rafiki yake, Dully aliwapigia simu wapambe wao na kuwafahamisha kuhusu sakata hilo.

“Dully alipotekwa, ilichukua takribani saa nzima ndipo wapambe wao walipofika kuwaokoa, ingawa haikuwa kazi rahisi kwasababu yalizuka mapambano makali,” alisema mtoa habari wetu.

Aliongeza, pamoja na kuokolewa, Mr. Blue alipata hasara kubwa, kwani gari lake lilivunjwa vunjwa na baadhi ya vifaa kuibiwa.

Vifaa hivyo ni kioo cha mbele cha gari na vile vya kuangazia pembeni (side mirrors), simu ya mkononi, nyaraka zake binafsi ambazo ni muhimu, pamoja na pesa.

Ilielezwa kuwa wahuni hao pia walimsababishia Dully hasara, baada ya kumpora kiasi cha pesa ambacho idadi yake haijafahamika.

Mwandishi wetu, aliongea na Dully ambaye alikiri kutokea utekaji huo na kusema: “Walitusumbua sana, nadhani lengo lao ilikuwa ni kuiba na hivyo walifanikiwa.”

Alipoulizwa kama waliripoti tukio hilo polisi, Dully alijibu: “Hatukwenda polisi kwasababu tuliamua kuyapuuzia mambo hayo, ila Blue yeye alikwenda hospitali kwasababu aliumia kidogo.”
Blue alipotafutwa, hakuweza kupatikana.

CCM waibeba Simba kuiua Enyimba




Habari moto-moto zilizolifikia gazeti hili, juzi, Jumamosi kutoka chanzo chetu na kuthibitishwa na Katibu Mkuu Msaidizi wa Klabu hiyo, Mohammed Mjenga zilisema vigogo hao wameamua kuchukua uamuzi huo baada ya kuona mambo hayaendi vizuri.

Ziliendelea kueleza kuwa baada ya kuona kuna uwezekano wa Simba kushindwa kwenda Nigeria kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Enyimba kutokana na kukosa fedha, wadau hao walijitolea gharama za kuisafirisha.

Hata hivyo, chanzo chetu hakikuwa tayari kuyataja majina ya vigogo hao, licha ya kuendelea kulihabarisha kwamba, vigogo hao wamekuwa wakitoa misaada mbalimbali klabuni hapo ikiwa ni pamoja na kugharamia kambi na posho za wachezaji.

Championi likiwa linahaha kutafuta ukweli wa habari hizo ndipo lilipomnasa, Mjenga ambaye alikiri na kuongeza kuwa vigogo hao wa CCM wamekuwa wakishirikiana bega kwa bega na Kundi la Marafiki wa Simba ‘Friends Of Simba kuisaidia timu yao.

Katibu huyo aliweka bayana kuwa, licha ya vigogo hao kutoka serikalini na Friends of Simba, pia wapo wadau wengine kutoka taasisi binafsi ambao kwa mapenzi yao huisaidia Simba ili isonge mbele.

Baadhi ya vigogo wa CCM ambao wanadaiwa kuwa ni wanazi wakubwa wa Simba ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Sophia Simba, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Prof. Juma Kapuya.

Wengine ni Mbunge wa Rorya, Prof. Phillimon Sarungi, Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azzan, Mbunge wa Singida Mjini, Mohammed Dewji, Mawaziri Wakuu Wastaafu, Rashid Mfaume Kawawa, Fredrick Sumaye na aliyejiuzulu hivi karibuni, Edward Lowassa.

Orodha ya vigogo hao wa CCM haina maana kwamba wao ndiyo waliohusika moja kwa moja kuisaidia Simba kwa kipindi hiki.

MWALIMU AFUMANIWA


Fumanizi hilo ambalo lilishuhudiwa na mwandishi wetu, lilitokea Ilala Bungoni eneo la Shariff Shamba saa 8.30 usiku baada ya mwalimu huyo kuwekewa mtego na mchumba wake huyo bila kufahamu.

Habari zilizopatikana katika eneo la tukio kutoka kwa jirani na mwalimu huyo, zilidai kuwa ticha huyo alikuwa na mchezo wa kumuingiza mjeshi huyo chumbani humo kwa muda mrefu.

“Bila kujali kuwa chumba hicho alikuwa amepangiwa na mchumba wake huyo, mwalimu alikuwa akimuingiza mwanajeshi huyo na kulala naye hadi asubuhi pindi mchumba wake anapokuwa hayupo,” alisema mtoa habari wetu.

Kutoka na hali hiyo, habari zinasema kuwa, baada ya kuchukizwa na tabia ya mwalimu huyo, wasamaria wema walimtonya mchumba wake ambaye anaishi mbali na eneo hilo.

Siku hiyo mchumba huyo alikwenda na kuweka mtego eneo hilo ambapo ulizaa matunda na kumfumania mwanajeshi huyo akiwa chumbani kwa mwalimu huyo, hivyo alichomoa funguo mlangoni na kufunga kwa nje.

Baada ya kufunga mlango, mwanaume huyo alikwenda kuita polisi na kumwamsha mwenye nyumba ili ashuhudie fumanizi hilo.

Wakati mfumaniaji huyo na wapambe wake wakiwa katika pilikapilika za kuwafuata polisi katika Kituo cha Pangani, Ilala huku nyuma mjeshi huyo alichukua chuma ambacho kilikuwepo chumbani humo na kuvunja kitasa cha mlango, kisha kutoweka.

Mwanaume huyo na wenzake waliporudi kutoka polisi, walipigwa na butwaa kukuta kitasa cha mlango kimevunjwa na mwanajesi aliyekuwa amemfungia ndani hayupo.

Aliyebaki chumbani humo alikuwa ni mwalimu ambaye alikuwa amejilaza kitandani huku akilia.

Majirani ambao walijazana kwa wingi eneo hilo walimwambia mwandishi wetu kuwa walishindwa kumzuia mjeshi huyo baada ya kutoka chumbani kwa sababu aliwatisha kuwapiga na chuma endapo ‘wangemtilia kiwingu’.

Hadi mwandishi wetu anaondoka eneo la tukio, mwanaume huyo na mchumba wake walikuwa wakizozana, huku mwanamke akiomba msamaha.

Wakati huohuo, Richard Bukos anaripoti kuwa mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Mussa hivi karibuni alipewa kipigo kikali na mkewe baada ya kufumaniwa akiwa na kimwana mwingine.

Tukio hilo lilitokea Machi 9 mwaka huu, ndani ya Ukumbi wa New Msasani Beach Club uliopo jijini Dar es Salaam ambapo kulikuwa na Bonanza la Bendi ya Akudo Impact 'Wana Pekechapekecha'.

Katika tukio hilo ambalo lilishuhudiwa na mwandishi wetu, mke wa mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina moja la Mayasa, alivamia ukumbini saa 6.15 usiku na kuanza kuangaza meza moja hadi nyingine kama vile mtu aliyeelekezwa kitu.

Baada ya dakika chache mwanamke huyo alifanikiwa kumbamba 'laivu' mumewe na kimwana mwingine wakiwa kwenye mwanga hafifu wakipeana raha za dunia.

Kufuatia tukio hilo, mwanamke huyo alikuwa kama Mbogo aliyejeruhiwa kwani alizusha vurumai la nguvu kisha kumwaga chipsi, nyama za mbuzi na vinywaji vilivyokuwa vimetapakaa mezani. Vyakula hivyo vilikuwa vikiliwa na wawili hao, (kama anavyoonekana ukurasa wa mbele akidhibitiwa asiendelee kufanya fujo.)

Wakati mume akishushiwa kipigo, kimwana aliyefumwa akitesa na mume huyo alifanikiwa kutoroka kwa kutambaa chini ya meza za ukumbi huo na kutokomea nje ya ukumbi.

Baada ya varangati kukolea, wapambe wa mume huyo walitokea na kutaka kulizima lakini ilishindikana baada ya mwanamke huyo kuwatuhumu wapambe hao kuwa ndiyo makuwadi wakubwa wa mume wake.


Sakata hilo lilitulizwa na mtunisha misuli maarufu aliyewahi kuwa mshindi wa shindano la Mr. Dar, Coster Siboka ambaye alimdhibiti mwanamke huyo.

AIBU KUBWA


Kukamatwa kwa warembo hao kumefuatia msako mkali uliofanywa na jeshi hilo la polisi kufuatia amri la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro ambapo aliwaagiza askari hao kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria makahaba wote wanaozurula usiku kusaka wateja.

Taarifa zilizopatikana ndani ya jeshi la polisi zimeeleza kuwa, warembo hao walikamatwa usiku wa manane wakiwa katika mawindo maeneo ya Ocean Road na katikati ya jiji.

Aidha, taarifa hizo zilidai kuwa warembo hao wamekuwa wakijipanga pembezoni mwa barabara huku wengine wakifanya mawindo katika kumbi za starehe kwa lengo la kuwanasa wanaume ili wafanye nao mpenzi.

Habari zaidi zinadai kuwa kitendo cha wanawake kuzurula ovyo nyakati za usiku ni hatari kwa usalama wa mkoa na wao wenyewe.

Imeelezwa kuwa tabia ya kujiuza ni hatari kwa kuwa hivi sasa kuna janga la ugonjwa wa Ukimwi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi, Ilala Bw. Faustine Shilogire alipohojiwa na mwandishi wetu alikiri kukamatwa kwa warembo hao na kudai kuwa hilo litakuwa ni zoezi la kudumu kwani wanawake hao wamekuwa na tabia ya kurudi katika maeneo ya biashara yao siku chache baada ya kuachiwa.

Aliendelea kusema kuwa zoezi hilo huwa gumu kutokana na ukweli kuwa makahaba hao wakipelekwa mahakamani huwa wanatozwa faini ndogo, jambo linalowafanya warudi katika maeneo yao kuendelea na biashara hiyo haramu.

“Unajua kwa sasa hakuna sheria ya uzembe na uzurulaji, hivyo, wanapofikishwa mahakamani kwa kipengele hicho huwa wanapewa adhabu ndogo ndogo ambapo wanalipa na kurejea katika biashara hizo,” alisema Kamanda Shilogire.

Aliongeza kuwa jeshi lake halitakata tamaa bali litaendelea na msako wa kusaka makahaba na ataelekeza nguvu zake maeneo ya Buguruni hasa karibu na baa ya Kimboka, Sewa na vichochoro vya hapo ambapo warembo hao wanajiuza.

Alisema vibaka pia watakamatwa kwani hutumika kuwapora pesa, simu na saa wateja wa makahaba hao au hata raia wema wanaokumbana nao mitaani.

Mtoto wa kigogo abambwa akijiuza


Mtoto huyo na wenzake kadhaa walinaswa katika mitaa ya Ohio, Mnazi mmoja na maeneo ya Buguruni usiku wa manane wakiwa katika mawindo yao.

Wasichana hao walitupwa rumande katika Kituo cha Polisi cha Buguruni jijini la Dar es Salaam mara baada ya kufikishwa kituoni hapo.

Hata hivyo, watu wanaomfahamu mtoto huyo wa kigogo walimwambia mwandishi wetu kuwa licha ya kufanya biashara hiyo haramu binti huyo yuko ‘njema’ kwao.

“Huyu msichana namfahamu, yuko fiti kwao Masaki, sijui ni kitu gani kinamzuzua hadi anakamatwa usiku wa manane akijinadi kwa wanaume,’’ alisema kijana mmoja aliyedai anamfahamu vema binti huyo wa kigogo.

Mtoto huyo wa kigogo alipohojiwa na mwandishi wetu alisema kuwa anafanya hivyo kwa ‘starehe yake’ kwani anapata kila kitu anachokihitaji nyumbani kwao.

“Mtoto wa mkurugenzi ndio nini? Acha nifanye mambo kwa raha zangu,” alisema msichana huyo huku akionyesha kukerwa na swali hilo la mwandishi.

Rafiki wa karibu wa msichana huyo, alimwambia mwandishi wetu kuwa pamoja na msichana huyo kujihusisha na biashara ya ukahaba, hafanyi hivyo kwa ‘njaa’ ya kutafuta fedha, bali kwa ajili ya kufurahisha nafsi yake.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi, Ilala, Faustine Shilongire alipoulizwa na gazeti hili kuhusu msako huo, alithibitisha kufanyika na akasema litakuwa ni zoezi la kudumu.

Shilongire aliongeza kuwa watakuwa wakiwakamata mara kwa mara makahaba hadi waache tabia hiyo, licha ya kutozwa faini aliyoiita kuwa ni ndogo wanapofikishwa mahakamani.

“Tutapambana nao kwa kuwakamata kwa kuwa ni tabia mbaya ambayo inachangiwa na mahakama kuwatoza faini ndogo sana ambayo wahusika wanamudu kuilipa,” alisema.

Zoezi hilo la kukamata makahaba limeibuka kutokana na amri ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro ambaye amekuwa mstari wa mbele kupiga vita biashara hiyo inayoaminika kuwa inachangia kusambaza ugonjwa wa Ukimwi.

Friday, March 14, 2008

Nora azua kasheshe


Shuhuda wetu alisema, Nora alianzisha vurugu hizo mara baada ya kurejea kutoka matembezini saa 10 alfajiri huku akiwa amefuatana na mwanaume aliyedaiwa ni mchumba wake na alipogonga mlango ili afunguliwe mtoto wa mwenye nyumba ambaye ndiye anayemfungulia kila mara aligoma kufanya hivyo.

Chanzo chetu kilisema, baada ya kukataliwa kufunguliwa ndipo Nora alipoamua kwenda kumgongea mama mwenye nyumba huku akiporomosha matusi mazito na kudai iwapo hawataki kumfungulia wamrudishie kodi yake ili akapange kwingine.

Shuhuda wetu alisema, baada ya kuona juhudi zake za kutaka kufunguliwa mlango zinazidi kugonga mwamba, alizidi kupiga kelele huku akianza kuvua blauzi aliyovaa na kubaki tupu, hivyo kusababisha baadhi ya majirani kumshangaa kwa kitendo hicho.

Mwenye nyumba kwa kuepusha shari aliamua kufungua mlango, lakini hiyo inadaiwa kumpa nafasi mwanaume aliyefuatana na Nora kumtwanga chupa mtoto wa mwenye nyumba ambaye awali ndiye aliyegoma kuwafungulia mlango. Rafiki huyo wa Nora amefunguliwa mashitaka na anasakwa na polisi kwa hati na. MK/RB/63/08.

Mwandishi Wa habari hizi ilibidi aende katika nyumba anayoishi Nora ambapo mama mwenye nyumba aliyejulikana kwa jina la Mama Hilda, alikiri kumfukuza msanii huyo kutokana na vurugu zake ambazo alidai zimevuka mpaka.

Saturday, March 8, 2008

MAMISS WACHEZA MKANDA WA NGONO




Habari kutoka katika chanzo chetu cha kuaminika zinasema mastaa hao wa fani ya urembo walishawishiwa kucheza mkanda huo kwa malipo makubwa na kwamba usingeuzwa nchini.

“Yaani huwezi kuamini, nimeuona kwa macho yangu mwenyewe, ni uchafu mtupu! Warembo maarufu kama (anawataja majina) ambao hawana kashfa yoyote, wanaonekana katika mkanda huo wakifanya mambo ya ajabu,” kilieleza chanzo chetu.

Aidha chanzo hicho kiliendelea kupasha kuwa mkanda huo haupatikani nchini, lakini yeye alifanikiwa kuuona nyumbani kwa rafiki yake ambaye ni rafiki wa karibu sana na mmoja kati ya warembo walioshiriki kucheza muvi hiyo ya uchafu.

Hata hivyo baadhi ya warembo hao waliohojiwa na Ijumaa, waliruka madai hayo na kusema kuwa, wanaopakaza mambo hayo ni wabaya wao ambao hawapendi kuona mafan ikio waliyonayo katika urembo.

“Hizi habari umezitoa wapi? Lakini hazinishangazi sana, unajua watu hawapendi kuona mafanikio ya wengine ndiyo maana wanaamua kutuhusisha na mambo machafu ili kutiuharibia majina yetu,” alisema mmoja wa warembo waliohojiwa na gazeti hili.

Katika hatua nyingine, Miss Kanda ya Ziwa 2005, Maureen Gislasy ambaye pia anashikilia taji la mrembo anayevutia zaidi kwenye picha (Miss Photogenic) kwa mwaka huo, anadaiwa kutoswa na mpenzi wake wa kizungu raia wa Italia, baada ya kukataa kucheza mkanda mchafu.

Inadaiwa Maureen alipoambiwa na mchumba wake nia yake ya kumuoa, alianzisha mapenzi motomoto na mzungu huyo akijua fika kwamba kuolewa kupo njiani kumbe hakujua ana lake jambo.

Baada ya ndoa kukaribia kufungwa ndipo mtasha huyo alimuomba Maureen warekodi mkanda wa ngono ambao ungeuzwa Marekani na wao kulipwa fedha nyingi, ambazo zitawafanya waishi kwa raha mpaka mwisho wa maisha yao.

Inadaiwa Maureen aliamua kutokubali kurekodi mkanda wa ngono na ndoa isifungwe, kwa kile alichoona hata kama atalipwa fedha nyingi bado atakuwa amejidhalilisha.

Mafia ilipomsaka Maureen ili kujua kwa undani kile kilichopo, alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuachwa na mchumba wake huyo kwa kitendo chake cha kukataa kurekodi mkanda wa ngono.

“Kweli dunia imeisha yaani kumbe hawa Wazungu wanawapenda mamiss kwa ajili ya kuwafanyia mchezo huu huku wakijifanya wanakumwagia fedha nyingi ili wakuchanganye akili.

“Mimi alinifuata na kuniambia anataka kunioa lakini baada ya muda akaanza kuniambia nirekodi mkanda wa ngono kwa ahadi za kunipa Sh milioni 50, lakini nilimjibu fedha inatafutwa na siwezi kupata utajiri kwa njia kama hizo huku nikimtisha akiendelea nitamshitaki,” alisema Maureen.

Wasanii Milionea wa Bongo

Haya wadau,

nimejaribu kutafakari niliyoyasikia kwenye vyombo vya habari hapa kwetu lakini bado nadhani moyo wangu haujapata jibu kamili…naomba na nyinyi wadau wangu mniambie vipi kuhusu hawa wasanii matajiri hapa kwetu Tanzania?


WASANII HAO NI HAWA HAPA NA THAMANI ZA RASILIMALI ZAO

1; LADY JAY DEE - MILLION 500

2; JUMA NATURE – MILLION 300

3; BANANA ZORRO – MILLION 280

4; MATONYA - MILLION 180

5; FEROOZ - MILLION 140

6; PROFESA JAY - MILLION 130

7; STARA THOMAS -MILLION 80

8; AY -MILLON 60

9; KLYNN -MILLION 45

10; MWANA FA - MILLION 30

HAYA KAZI KWENU

Wednesday, March 5, 2008

Mafisadi Benki Kuu kortini


Na Mwandishi Wetu
Watuhumiwa wote wa ufisadi katika akaunti ya malipo ya nje (EPA), uliohusu shilingi bilioni 133 wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kujipatia fedha hizo kinyume na utaratibu.Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila alipoongea na mwandishi wetu, jijini Dar es Salaam, mwanzoni mwa wiki hii....

YOU ARE WHAT YOU EAT


IJUE UWEZO ZAIDI WA KITUNGUU SAUMU NA TANGAWIZI KATIKA AFYA YAKO!

Wiki iliyopita tulisoma kuhusu orodha ya baadhi ya vyakula venye nguvu ya kuponya matatizo mbalimbali ya kiafya. Katika makala hayo niliorodhesha baadhi ya vyakula kama vile samaki, uyoga na vingine vingi yakiwemo matunda kadhaa.

Baadhi ya wasomaji wetu walinipigia simu na kunitutumia ujumbe wakitaka kujua matumizi ya vyakula hivyo katika kuponya matatizo yao. Kimsingi katika makala hayo sikukusudia kuelezea njia za kuzitumia kuandaa vyakula hivyo ili kujitibu kama dawa.

Hayo nilikwishaeleza kwa utaratibu mwingine katika makala zangu zilizotangulia, lakini hapo nilikusudia kuorodhesha tu vyakula hivyo na faida zake unazozipata kila unapokula, kwa utaratibu wa kawaida na unaoutumia wewe siku zote.

Katika maisha ya sasa, ni vizuri sana kujua kila unachokula kina faida au madhara gani mwilini mwako, kwani unachokula leo, ndicho kitakachokufanya uugue au uwe mzima kesho, tiba au madhara ya chakula hujijenga mwilini kidogokidogo na matokeo yake huonekana baada ya muda mrefu.

Nikurudi kwenye swali la msingi ambalo waliuliza baadhi ya wasomaji kwamba waandae vipi vyakula au matunda niliyoyaeleza iwapo wanataka kutibu ugonjwa fulani. Kimsingi, kama nilivyosema hapo awali, hapa sikukusudia kufanya hivyo, bali nimekusudia kuonesha faida na uwezo wa vyakula hivyo katika miili yetu, hivyo unashauriwa kuvila vyakula hivyo kawaida kama unavyovila siku zote, ukielewa kuwa unajijengea kinga mwilini mwako au unajitibu ugonjwa fulani taratibu.

Katika makala ya leo, tutaangalia kwa kirefu uwezo wa KITUNGUU SAUMU katika uwezo wake wa kutumika kama dawa za anti-biotic. Vile vile tutaangalia kwa kirefu uwezo wa TANGAWIZI kutumika kama dawa ya maradhi mbalimbali, kama ilivyoelezwa na mwandishi Tanushree Podder katika kitabu chake cha You Are What You Eat:

Kitunguu saumu kimekuwa kikitumika kama dawa ya mitishamba, takribani miaka 5,000 iliyopita. Historia inaonesha kuwa wafungwa wa nchini China walikuwa wanatakiwa kula kitunguu saumu kibichi kila siku asubuhi ili kuimarisha afya zao.

Aidha inaelezwa zaidi kuwa nchini Misri, watumwa walikuwa wakilishwa vitunguu saumu na vitunguu maji ili wapate nguvu za kujenga ‘ma piramid’. Vile vile vitunguu vilikuwa vinatumika kama dawa ya kufukuza majini na mapepo wabaya.

Ukiacha ushahidi huo wa kiasili kuhusu uwezo na umuhimu wa kitunguu saumu kiafya, utafiti wa kisayansi umegundua pia kuwa kishina kimoja cha kitunguu saumu kina dawa sawa na uniti 100,000 za vidonge vya Pennicillin ambayo ni karibu ya robo dozi ya vidonge hivyo na havina madhara yoyote katika mwili wa binadamu.

KITUNGUU SAUMU:
kinaaminika kuwa na uwezo wa kuzuia aina mbalimbali za saratani, kama vile saratani ya tumbo, ngozi, matiti, koo na utumbo mkubwa. Aidha kitunguu saumu kina uwezo wa kudhibiti seli zisizaliane vibaya na kuleta madhara mengine mwilini.

Aidha, kitunguu saumu kina uwezo wa kushusha shinikizo la juu la damu, ili kupata matokeo yake katika kuponya maradhi hayo, unahitaji kuwa unakula angalau kitunguu saumu kimoja mpaka vitatu kila siku kwa muda wa miezi mitatu. Lakini hata utakapokula kiasi chochote utakachoweza kwa wale msio na maradhi yoyote, bila shaka mtakuwa mnajijengea kinga katika miili yenu.

Aidha ulaji wa vitunguu saumu vibichi, husaidia kurekeshi kiwango cha sukari kwa wagonjwa wa kisukari na manufaa yanapatikana zaidi kwenye vitunguu vibichi kuliko vya kupika au kukaanga. Vilevile unaweza kuchanganya asali na vitunguu saumu na kula pamoja kama dawa ya kuondoa mafua.

TANGAWIZI

Hii nayo ni dawa ya mitishamba yenye nguvu na maarufu sana nchini China, India na Japan. Imekuwa ikitumika katika nchi hizo kwa karne kadhaa na kuenea hadi Mashariki ya Kati, Spain na West Indies. Kwa mujibu wa historia yake, kwa mara ya kwanza Tangawizi ilitengenezwa nchini Jamaika ili kusaidia tatizo la ukosefu wa choo, kichefuchefu, ugonjwa unaotokana na kutembea kwa muda mrefu na uchovu wa asubuhi.

Tangawizi inaaminika kuwa na uwezo wa kuzuia kuchafuka kwa tumbo, kubana kwa kifua na kuumwa kwa kichwa. Kwa mujibu wa kitabu cha You Are What You Eat, katika bara la Asia, Tangawizi hutumika kuogea ili kuponya tatizo la kuziba kwa pua kutokana na mtu kuwa na ‘aleji’. Tangawizi husagwa na unga wake kutumika kuandaa kinywaji au inaweza kutumika ikiwa bado mbichi kwa kuwekwa kwenye maji ya moto na kunywa.

YOU ARE WHAT YOU EAT


Ijue nguvu ya kuponya ya vyakula-2


Wiki iliyopita tuliona nguvu ya baadhi ya vyakula katika kuzuia na kuponya baadhi ya magonjwa. Vyakula tulivyoangalia vilikuwa ni pamoja na tufaha (apples), ndizi mbivu, maharage, kabichi, karoti, kahawa na nafaka, wiki hii tunaendelea kuangalia orodha hiyo ya vyakula vyenye uwezo wa kutuepusha dhidi ya magaonjwa mengi hatari kama ifuatavyo:


SAMAKI (FISH)

• Huyayusha damu, huifanya kuwa nyepesi

• Huilinda mishipa ya damu isiharibike

• Huzuia damu kuganda

• Hushusha shinikizo la damu

• Hupunguza hatari ya kupatwa na mshituko wa moyo na kiharusi

• Hutuoa ahueni kwa wenye ugonjwa wa kipandauso

• Husaidia kuzuia uvumbe mwilini

• Huendesha mfumo wa kinga ya mwili

• Huzuia saratani

• Hutoa ahueni kwa wenye pumu

• Hupambana na dalili za awali za ugonjwa wa figo

• Huongeza nishati ya ubongo


KITUNGUU SAUMU (GARLIC)

• Hupambana na maambukizi

• Ina kemikali zenye uwezo wa kudhibiti saratani

• Hufanya damu kuwa nyepesi

• Hupunguza shinikizo la damu na kolestro

• Huamsha mfumo wa kinga ya mwili

• Huzuia na kutoa ahueni kwa kikohozi kilaini.

• Huweza kutumika kama dawa ya kifua


TANGAWIZI (GINGER)

• Huzuia ugonjwa wa kutetemeka

• Hufanya damu kuwa nyepesi


ZABIBU (GRAPE)

• Ina uwezo wa kufanya virusi visifanyekazi

• Huzuia meno kuoza

• Ina mchanganyiko wenye uwezo wa kuzuia saratani


PILIPILI HOHO (GREEN CHILLIES)

• Dawa nzuri ya mapafu

• Hutumika kama dawa ya kifua

• Huzuia na kuponya kikohozi kikali

• Husaidia kuyeyusha mabonge ya damu

• Hutoa maumivu

• Huweza kumfanya mtu kuwa na furaha


ASALI (HONEY)

• Huua vijidudu (bacteria)

• Huondoa wadudu kwenye vidonda na malengelenge

• Huondoa dalili za maumivu

• Hutoa ahueni kwa wagonjwa wa pumu

• Hutuliza maumivu ya vidonda vya koo

• Hutuliza mishipa ya damu, humpatia mtu usingizi

• Hutoa ahueni kwa mtu anayeharisha


MAZIWA (MILK)

• Huzuia ugonjwa wa mifupa (osteoporosis)

• Hupambana na maambukizi, hasa kuharisha

• Hurekebisha kuchafuka kwa tumbo

• Huzuia vidonda vya tumbo

• Huzuia kuoza kwa meno

• Huzuia mtu kupatwa na kikohozi

• Huongeza nishati ya ubongo

• Hushusha shinikizo la damu

• Hushusha kiwango cha kolestro mwilini

• Hudhibiti baadhi ya saratani


UYOGA (MUSHROOM)

• Hufanya damu kuwa nyepesi

• Huzuia saratani

• Hushusha kiwango cha kolestro

• Huchangamsha mfumo wa kinga ya mwili

• Hudhoofisha virusi


SHAYIRI (OATS)

• Dawa bora ya moyo

• Hushusha kolestro mwilini

• Hurekebisha sukari kwenye damu

• Ina mchanganyiko wa virutubisho unaodhibiti saratani

• Hupambana na kuvimba kwa ngozi

• Ina uwezo sawa na dawa ya kumpatia mtu choo


KITUNGUU MAJI (ONION)

• Dawa kubwa ya magonjwa ya moyo

• Huimarisha kolestro nzuri (HDL)

• Huifanya damu kuwa nyepesi

• Hushusha kiwango cha kolestro mbaya

• Huzuia damu kuganda

• Hurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu

• Huua vijidudu

• Huzuia saratani

Tuesday, March 4, 2008

SIKU FAMILIA YA MATUMLA ILIPOPATA KICHAPO TENA!




Bondia Francis Cheka (kushoto) akimuangalia Hassan Matumla kwa jicho la Simba wakati akitoa kipigo kikali kilichomtoa knock out katika mpambano mkali uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Diamond Jubilee. Kabla ya kutoa kipigo hiki, Cheka ameshamchapa kaka mtu pia, Rashid Matumla, sasa imedhihirika Cheka hana mpinzani Bongo na familia ya Matumla imeanza kupoteza umaarufu katika ndondi.

Yanga, Adema waingiza mil. 65.2/-

na Dina Zubeiry



WAKATI Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), likizipongeza timu za Simba na Yanga kwa kusonga mbele kwenye michuano ya kimataifa, mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho kati ya Yanga na AS Adema, iliyopigwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, imeingiza sh mil. 65. 2.

Mechi hiyo iliyokwisha kwa Yanga kusonga mbele kwa jumla ya ushindi wa mabao 2-1, katika mechi ya kwanza, Yanga ilifungwa 1-0 kabla ya kushinda 2-0 katika mechi hiyo ya marudiano.

Yanga sasa itakumbana na Al-Qada ya Libya huku Simba iliyoifungasha virago AWASSA City ya Ethiopia, ikikumbana na Enyimba ya Nigeria.

Mechi za kwanza za raundi ya pili ya michuano hiyo (Ligi Mabingwa na Shirikisho), kwa Yanga na Simba, zitafanyika ugenini kati ya Machi 21 na 23, kabla ya kurudiana kati ya Aprili 4 na 6.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Florian Kaijage, kama Simba na Yanga zitajipanga vema katika mechi zao, hakuna kitakachozuia kusonga mbele.

Kuhusu mapato ya mechi ya Yanga na AS Adema, Kaijage alisema, fedha hizo zimepatikana kutokana na watu 12,112 walioingia katika mechi hiyo na kulipa.

Mechi hiyo iliyoisha kwa Yanga kushinda 2-0, hivyo kusonga mbele kwa jumla ya mabao 4-1, viti maalumu ilikuwa ni sh 20,000, jukwaa kuu sh 15,000, sh 8,000 kwa jukwaa la kijani na sh 3,000 kwa mzunguko.

Kwa mapato hayo, Yanga imepata sh mil. 41.6 huku TFF na CAF zikilamba sh 9,591,410, Uwanja sh 6, 394, 410, huku gharama za mchezo zikiwa ni sh 2,186, 000.

Katika hatua nyingine, kutokana na machafuko ya kisiasa yaliyoikumba Cameroon, TFF imelazimika kutuma barua kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kupata uhakika wa mahali itakapofanyika mechi ya Twiga Stars.

Kaijage alisema, TFF imechukua hatua hiyo baada ya CAF kusitisha mechi za klabu, hivyo TFF imetaka kufahamu mahali ambako mechi hiyo ya marudiano itachezwa.

Katika mechi ya kwanza iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Februari 23, Twiga Stars ilifungwa mabao 3-0, hivyo kuhitaji ushindi wa mabao 4-0 katika mechi ya marudiano.

Mshindi wa mechi hiyo, atakuwa amejitwalia nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa Afrika kwa wanawake, zitakazofanyika nchini Equatorial Guinea baadaye mwaka huu.

Alisema, ukiondoa utata huo wa mahali itakapofanyika mechi hiyo, maandalizi mengine ya safari ya kwenda Cameroon, yanaendelea vema kwani Twiga Stars inatarajiwa kuondoka nchini Machi 6.

Aidha, TFF imekata rufaa Mahakama Kuu kupinga uamuzi wa Mahakama ya Kazi kumpa ushindi, aliyekuwa Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Ashery Gasabile.

Gasabile aliyeajiriwa na TFF Julai 16 mwaka 2006, alikuwa akipinga taratibu zilizotumiwa na TFF kusitisha ajira yake Desemba 17, mwaka huo na Mahakama ya Kazi chini ya Jaji Mfawidhi Ernest Mwipopo, kuridhia pasipo shaka kuwa Gasabile, aliachishwa kazi kimakosa.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Florian Kaijage, Shirikisho hilo limekata rufaa kupitia kwa wakili wake, Alex Mgongolwa, kupinga hukumu hiyo.

Monday, March 3, 2008

Happy Bithday ya Jahazi




Birthday ya bendi ya taarabu ya Jahazi ilikuwa funika bovu mwishoni mwa wiki pale Diamond. Kama kawaida picha za vituko hazikukosa...zaidi nenda hapa:

Mambo ya Guta

Mkapa hali mbaya


Wakiongea na mwandishi wetu kwa nyakati tofauti, jijini Dar es Salaam, wikiendi iliyopita, wachambuzi hao walifafanua kwamba ‘ishu’ ambazo zinaelekea kumkaanga Mkapa ni ile ya Akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA) na mikataba yote ambayo ilisainiwa wakati wa utawala wake.

Katika mikataba, kipimo cha kwanza walikielezea kuwa ni kauli ya wafanyakazi wa Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO) ambao walimshushia lawama nzito Mkapa kuwa utawala wake ndiyo umeifanya taasisi hiyo iwe hohe hahe.

“Waswahi wanasema mwehu mtoto akikuvua nguo usimkimbize, ni kweli Mzee Mkapa hataki kukimbizana na watoto, lakini ukimya wake unafanya hali yake izidi kuwa mbaya kisiasa,” alisema Dk. Zaid Kamsa wa Dar es Salaam.

Dk. Kamsa ambaye ni mhitimu wa Shahada ya Uzamivu, Chuo Kikuu cha Arizona Marekani katika masomo ya Sayansi ya Siasa (Political Science), aliongeza: “Kikwete ameshatangaza Mzee Mkapa asibughudhiwe, lakini ni jambo gumu kwa sasa.

“Ni jambo gumu kwakuwa kuna uwezekano watu wakaendelea kumrushia madongo na kwasababu hali ya sasa ni mbaya, itakuwa ngumu kumsafisha kutokana na hili wimbi la ufisadi.”

Ijumaa iliyopita, wafanyakazi wa TANESCO walifanya kikao kujadili mikataba mibovu ya shirika hilo ambapo moja kwa moja walimrushia lawama Rais Mkapa enzi ya utawala wake kwa kuingia mikataba mibovu kama ule wa IPTL na Songas.
Wakati akiwashiwa moto TANESCO, tayari kumekuwa na msukumo kutoka kwa watu wengi, wakitaka rais huyo mstaafu awajibishwe kwenye sakata la EPA ambalo lililomfukuzisha kazi, aliyekuwa gavana wa Benki Kuu, Daud Ballali.

Pointi iliyo nyuma ya shinikizo hilo ni kuwa Mkapa awajibishwe kwakuwa upotevu wa shilingi bilioni 133 katika mfuko wa EPA, ulifanyika enzi ya utawala wake.