Wednesday, March 5, 2008

YOU ARE WHAT YOU EAT


Ijue nguvu ya kuponya ya vyakula-2


Wiki iliyopita tuliona nguvu ya baadhi ya vyakula katika kuzuia na kuponya baadhi ya magonjwa. Vyakula tulivyoangalia vilikuwa ni pamoja na tufaha (apples), ndizi mbivu, maharage, kabichi, karoti, kahawa na nafaka, wiki hii tunaendelea kuangalia orodha hiyo ya vyakula vyenye uwezo wa kutuepusha dhidi ya magaonjwa mengi hatari kama ifuatavyo:


SAMAKI (FISH)

• Huyayusha damu, huifanya kuwa nyepesi

• Huilinda mishipa ya damu isiharibike

• Huzuia damu kuganda

• Hushusha shinikizo la damu

• Hupunguza hatari ya kupatwa na mshituko wa moyo na kiharusi

• Hutuoa ahueni kwa wenye ugonjwa wa kipandauso

• Husaidia kuzuia uvumbe mwilini

• Huendesha mfumo wa kinga ya mwili

• Huzuia saratani

• Hutoa ahueni kwa wenye pumu

• Hupambana na dalili za awali za ugonjwa wa figo

• Huongeza nishati ya ubongo


KITUNGUU SAUMU (GARLIC)

• Hupambana na maambukizi

• Ina kemikali zenye uwezo wa kudhibiti saratani

• Hufanya damu kuwa nyepesi

• Hupunguza shinikizo la damu na kolestro

• Huamsha mfumo wa kinga ya mwili

• Huzuia na kutoa ahueni kwa kikohozi kilaini.

• Huweza kutumika kama dawa ya kifua


TANGAWIZI (GINGER)

• Huzuia ugonjwa wa kutetemeka

• Hufanya damu kuwa nyepesi


ZABIBU (GRAPE)

• Ina uwezo wa kufanya virusi visifanyekazi

• Huzuia meno kuoza

• Ina mchanganyiko wenye uwezo wa kuzuia saratani


PILIPILI HOHO (GREEN CHILLIES)

• Dawa nzuri ya mapafu

• Hutumika kama dawa ya kifua

• Huzuia na kuponya kikohozi kikali

• Husaidia kuyeyusha mabonge ya damu

• Hutoa maumivu

• Huweza kumfanya mtu kuwa na furaha


ASALI (HONEY)

• Huua vijidudu (bacteria)

• Huondoa wadudu kwenye vidonda na malengelenge

• Huondoa dalili za maumivu

• Hutoa ahueni kwa wagonjwa wa pumu

• Hutuliza maumivu ya vidonda vya koo

• Hutuliza mishipa ya damu, humpatia mtu usingizi

• Hutoa ahueni kwa mtu anayeharisha


MAZIWA (MILK)

• Huzuia ugonjwa wa mifupa (osteoporosis)

• Hupambana na maambukizi, hasa kuharisha

• Hurekebisha kuchafuka kwa tumbo

• Huzuia vidonda vya tumbo

• Huzuia kuoza kwa meno

• Huzuia mtu kupatwa na kikohozi

• Huongeza nishati ya ubongo

• Hushusha shinikizo la damu

• Hushusha kiwango cha kolestro mwilini

• Hudhibiti baadhi ya saratani


UYOGA (MUSHROOM)

• Hufanya damu kuwa nyepesi

• Huzuia saratani

• Hushusha kiwango cha kolestro

• Huchangamsha mfumo wa kinga ya mwili

• Hudhoofisha virusi


SHAYIRI (OATS)

• Dawa bora ya moyo

• Hushusha kolestro mwilini

• Hurekebisha sukari kwenye damu

• Ina mchanganyiko wa virutubisho unaodhibiti saratani

• Hupambana na kuvimba kwa ngozi

• Ina uwezo sawa na dawa ya kumpatia mtu choo


KITUNGUU MAJI (ONION)

• Dawa kubwa ya magonjwa ya moyo

• Huimarisha kolestro nzuri (HDL)

• Huifanya damu kuwa nyepesi

• Hushusha kiwango cha kolestro mbaya

• Huzuia damu kuganda

• Hurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu

• Huua vijidudu

• Huzuia saratani

No comments: