Wednesday, March 19, 2008

MWALIMU AFUMANIWA


Fumanizi hilo ambalo lilishuhudiwa na mwandishi wetu, lilitokea Ilala Bungoni eneo la Shariff Shamba saa 8.30 usiku baada ya mwalimu huyo kuwekewa mtego na mchumba wake huyo bila kufahamu.

Habari zilizopatikana katika eneo la tukio kutoka kwa jirani na mwalimu huyo, zilidai kuwa ticha huyo alikuwa na mchezo wa kumuingiza mjeshi huyo chumbani humo kwa muda mrefu.

“Bila kujali kuwa chumba hicho alikuwa amepangiwa na mchumba wake huyo, mwalimu alikuwa akimuingiza mwanajeshi huyo na kulala naye hadi asubuhi pindi mchumba wake anapokuwa hayupo,” alisema mtoa habari wetu.

Kutoka na hali hiyo, habari zinasema kuwa, baada ya kuchukizwa na tabia ya mwalimu huyo, wasamaria wema walimtonya mchumba wake ambaye anaishi mbali na eneo hilo.

Siku hiyo mchumba huyo alikwenda na kuweka mtego eneo hilo ambapo ulizaa matunda na kumfumania mwanajeshi huyo akiwa chumbani kwa mwalimu huyo, hivyo alichomoa funguo mlangoni na kufunga kwa nje.

Baada ya kufunga mlango, mwanaume huyo alikwenda kuita polisi na kumwamsha mwenye nyumba ili ashuhudie fumanizi hilo.

Wakati mfumaniaji huyo na wapambe wake wakiwa katika pilikapilika za kuwafuata polisi katika Kituo cha Pangani, Ilala huku nyuma mjeshi huyo alichukua chuma ambacho kilikuwepo chumbani humo na kuvunja kitasa cha mlango, kisha kutoweka.

Mwanaume huyo na wenzake waliporudi kutoka polisi, walipigwa na butwaa kukuta kitasa cha mlango kimevunjwa na mwanajesi aliyekuwa amemfungia ndani hayupo.

Aliyebaki chumbani humo alikuwa ni mwalimu ambaye alikuwa amejilaza kitandani huku akilia.

Majirani ambao walijazana kwa wingi eneo hilo walimwambia mwandishi wetu kuwa walishindwa kumzuia mjeshi huyo baada ya kutoka chumbani kwa sababu aliwatisha kuwapiga na chuma endapo ‘wangemtilia kiwingu’.

Hadi mwandishi wetu anaondoka eneo la tukio, mwanaume huyo na mchumba wake walikuwa wakizozana, huku mwanamke akiomba msamaha.

Wakati huohuo, Richard Bukos anaripoti kuwa mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Mussa hivi karibuni alipewa kipigo kikali na mkewe baada ya kufumaniwa akiwa na kimwana mwingine.

Tukio hilo lilitokea Machi 9 mwaka huu, ndani ya Ukumbi wa New Msasani Beach Club uliopo jijini Dar es Salaam ambapo kulikuwa na Bonanza la Bendi ya Akudo Impact 'Wana Pekechapekecha'.

Katika tukio hilo ambalo lilishuhudiwa na mwandishi wetu, mke wa mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina moja la Mayasa, alivamia ukumbini saa 6.15 usiku na kuanza kuangaza meza moja hadi nyingine kama vile mtu aliyeelekezwa kitu.

Baada ya dakika chache mwanamke huyo alifanikiwa kumbamba 'laivu' mumewe na kimwana mwingine wakiwa kwenye mwanga hafifu wakipeana raha za dunia.

Kufuatia tukio hilo, mwanamke huyo alikuwa kama Mbogo aliyejeruhiwa kwani alizusha vurumai la nguvu kisha kumwaga chipsi, nyama za mbuzi na vinywaji vilivyokuwa vimetapakaa mezani. Vyakula hivyo vilikuwa vikiliwa na wawili hao, (kama anavyoonekana ukurasa wa mbele akidhibitiwa asiendelee kufanya fujo.)

Wakati mume akishushiwa kipigo, kimwana aliyefumwa akitesa na mume huyo alifanikiwa kutoroka kwa kutambaa chini ya meza za ukumbi huo na kutokomea nje ya ukumbi.

Baada ya varangati kukolea, wapambe wa mume huyo walitokea na kutaka kulizima lakini ilishindikana baada ya mwanamke huyo kuwatuhumu wapambe hao kuwa ndiyo makuwadi wakubwa wa mume wake.


Sakata hilo lilitulizwa na mtunisha misuli maarufu aliyewahi kuwa mshindi wa shindano la Mr. Dar, Coster Siboka ambaye alimdhibiti mwanamke huyo.

No comments: