Wednesday, March 19, 2008

AIBU KUBWA


Kukamatwa kwa warembo hao kumefuatia msako mkali uliofanywa na jeshi hilo la polisi kufuatia amri la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro ambapo aliwaagiza askari hao kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria makahaba wote wanaozurula usiku kusaka wateja.

Taarifa zilizopatikana ndani ya jeshi la polisi zimeeleza kuwa, warembo hao walikamatwa usiku wa manane wakiwa katika mawindo maeneo ya Ocean Road na katikati ya jiji.

Aidha, taarifa hizo zilidai kuwa warembo hao wamekuwa wakijipanga pembezoni mwa barabara huku wengine wakifanya mawindo katika kumbi za starehe kwa lengo la kuwanasa wanaume ili wafanye nao mpenzi.

Habari zaidi zinadai kuwa kitendo cha wanawake kuzurula ovyo nyakati za usiku ni hatari kwa usalama wa mkoa na wao wenyewe.

Imeelezwa kuwa tabia ya kujiuza ni hatari kwa kuwa hivi sasa kuna janga la ugonjwa wa Ukimwi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi, Ilala Bw. Faustine Shilogire alipohojiwa na mwandishi wetu alikiri kukamatwa kwa warembo hao na kudai kuwa hilo litakuwa ni zoezi la kudumu kwani wanawake hao wamekuwa na tabia ya kurudi katika maeneo ya biashara yao siku chache baada ya kuachiwa.

Aliendelea kusema kuwa zoezi hilo huwa gumu kutokana na ukweli kuwa makahaba hao wakipelekwa mahakamani huwa wanatozwa faini ndogo, jambo linalowafanya warudi katika maeneo yao kuendelea na biashara hiyo haramu.

“Unajua kwa sasa hakuna sheria ya uzembe na uzurulaji, hivyo, wanapofikishwa mahakamani kwa kipengele hicho huwa wanapewa adhabu ndogo ndogo ambapo wanalipa na kurejea katika biashara hizo,” alisema Kamanda Shilogire.

Aliongeza kuwa jeshi lake halitakata tamaa bali litaendelea na msako wa kusaka makahaba na ataelekeza nguvu zake maeneo ya Buguruni hasa karibu na baa ya Kimboka, Sewa na vichochoro vya hapo ambapo warembo hao wanajiuza.

Alisema vibaka pia watakamatwa kwani hutumika kuwapora pesa, simu na saa wateja wa makahaba hao au hata raia wema wanaokumbana nao mitaani.

No comments: