Saturday, March 29, 2008

Nakaaya msagaji?


Nakaaya kupitia kipindi cha Friday Night Live cha Luninga ya EATV, Ijumaa iliyopita alisema kuwa uzuri wake unawadatisha watu wa jinsia tofauti, hivyo hashangai wanawake wenzake kumtongoza.

Kabla ya kauli hiyo ya Nakaaya, mtazamaji mmoja mwanamke, alituma ujumbe wa simu ya mkononi (sms) na kusomwa na mtangazaji wa kipindi hicho, Denis Busulwa ‘Sebo’, akieleza jinsi anavyovutiwa na msanii huyo.

Kwa mujibu wa ujumbe huo wa maneno na jinsi ulivyosomwa na Sebo ni kwamba mtazamaji huyo wa kike, alikuwa akivutiwa na Nakaaya kimapenzi.

Mara baada ya kuiona sms hiyo, Sebo alimuuliza Nakaaya kuwa iweje awavutie mpaka wanawake wenzake?
Hata hivyo, msanii huyo alijibu kwamba yeye anawavutia watu wote, kauli ambayo ilitafsiriwa na baadhi ya watazamaji kuwa pengine anapenda ‘hako kamchezo’ ndiyo maana hakuchukia kutongozwa na mwanamke mwenzake.

“Huyu dada naye yumo nini katika mambo hayo, maana jibu lake linaonesha anaona poa tu kutongozwa na wanawake wenzake!” Alisema mtazamaji mmoja, katika baa moja iliyopo Sinza, jijini Dar es Salaam, huku mwandishi wetu akimsikia.

Katika kipindi hicho, Nakaaya alialikwa akiwa na mwenzake Jacqueline Ntuyabaliwe ‘K-Lyn’ pamoja na wanamuziki nguli wa R&B duniani, Wamarekani KCI & Jojo.

Wasanii hao wote, walikuwa wakizungumzia ‘shoo’ ya KCI & Jojo, iliyoandaliwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo ambapo Nakaaya na K-Lyin waliisindikiza katika Ukumbi wa Hoteli ya Movenpick jikjini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita.

Aidha, siku moja baada ya kipindi hicho, habari tulizozipata kutoka kwa rafiki wa Nakaaya zilisema kuwa msanii huyo amekuwa akipigiwa simu na wakati mwingine kutumiwa ujumbe na idadi kubwa ya wanawake wakimtongoza.

Rafiki huyo alisema: “Wanawake wengi wamekuwa wakijieleza eti wanavutiwa na Nakaaya kwa sura yake halisi (natural), umbo, mtindo wake wa kukata nywele fupi na sauti yake.”

Nakaaya ambaye ni dada wa Miss Tanzania na Miss World Africa mwaka 2005-06, Nancy Abraham Sumari kwa sasa ‘anafunika’ katika anga ya burudani kupitia kibao chake cha Mr. Politician kilichobeba jina la albamu yake yenye jumla ya nyimbo 10.

Nyimbo hizo zinazopatikana katika albamu hiyo inayogombewa vilivyo sokoni ni Nervous Conditions, Mr. Politician, Matatizo, New day, Malaika, Iyeyo, Love me, Nyimbo za Uhuru, A town girl na I’m Free

1 comment:

maishamema said...

Jamani mimi ninasikitika sana kuona mabinti wa kitanzania nao wanaanza kujiingiza katika suala la mapenzi ya kisagaji huku vyombo vya habari vikishabikia suala hilo.Ukweli ni kwamba kiasili na kiuhalisi hakuna wala hayupo mwanamke yoyote yule duniani aliyeumbwa na Mungu Baba wa Mbinguni ambaye anaweza kuwa nahisia za kimapenzi au kuvutiwa na kingono na mwanamke mwenzake.Kama hiyo haitoshi kuna SIRI MOJA NZITO SANA iliyopo NYUMA YA KUWEPO KWA MAPENZI YA KISAGAJI!.Kwa utafiti wangu wa kina na kitaalamu ambao nimeufanya kuanzia mwaka 2005 nimegundua k,uwa kuna SIRI NZITO SANA iliyopo NYUMA YA MAPENZI YA KISAGAJI.Nime andaa kitabu kinachoitwa SIRI NZITO SANA NYUMA YA MAPENZI YA KISAGAJI! ambacho nina uhakika watanzania na ulimwengu wote watakapo kisoma kitabu hicho wataigundua siri hiyo nzito sana na bila shaka suala la mapenzi ya kisagaji na yale ya kisenge halitakuwwepo ten a tanzania.Ni siri moja nzito sana ambayo ulimwengu unapaswa kuifahamu, kwani hata hao mabinti wasagaji na wasagwaji hawajui chochote kuhusu siri hiyo.Taratibu za kukipeleka kitabu mtamboni zinakamishwa na uhaba wa pesa.Hivyo ninatafuta wafadhili amabo wapo tayari kushirikiana na mimi ili kazi hiyo iweze kutoka na hatimaye kuufikia umma.
NYINYI MABINTI WA KITANZANIA ACHENI UPUMBAVU! MWANAMKE HAWEZI KUWA NA MATAMANIO YA KINGONO KWA MWANAMKE MWENZAKE HATA SIKU MOJA! KINACHOTOKEA NI ADMIRATION TU NA WALA SI VINGINEVYO.
MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI AFRIKA AMEEEEEN.