Friday, March 28, 2008

Dunia ya Tatu


Baada ya kutamba kwa muda mrefu,wasanii wa muziki wa kizazi kipya,Mandojo na Domokaya au ukipenda “wazee wa magitaa” wameamua kuongeza nguvu kwa kumuingiza kundini msanii ajulikanaye kama Squiza. Na kutokana na ongezeko hilo,wameamua pia kubadili jina lao kutoka Mandojo na Domokaya na sasa watajulikana kama Dunia ya Tatu au D3 wakiwa ni wasanii watatu kama wanavyoonekana pichani.
Wengi mtakuwa mnatambua jinsi ambavyo Mandojo na Domokaya waliwahi kutamba na vibao vyao kama vile Dingi,Wanok nok,Niaje na nyinginezo nyingi.


Wakiwa pamoja hivi karibuni wasanii hao wameiambia BC kwamba wameamua kuongeza nguvu na kubadili jina kwani wameamua kutoka kivingine huku wakiendelea kuweka nakshi miziki yao kwa kutumia magitaa na vyombo vingine.Mpaka hivi sasa wameshatoa single inayokwenda kwa jina We Nenda ambayo hivi sasa wako mbioni kutengeneza video yake.
D3 wanasema hayo yote ni katika maandalizi ya kutoa albamu yao ya kwanza wakiwa kama D3.Kazi zao nyingi hivi sasa wanazifanyia ndani ya studio za 41 Records.BC inawatakia kila la kheri D3.

No comments: