Saturday, March 22, 2008

Mchina afumwa!


Sao Tong alikamatwa nyumbani kwake akiwa na viumbe kadhaa wakiwemo kaa na kamba walio hai wakiwa tayari kusafirishwa kwenda nje ya nchi.

Kwa mujibu wa mtoa habari wetu ambaye alishuhudia tukio hilo (jina tunalihifadhi), baada ya kutiwa mbaroni, Mchina huyo alipelekwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay kabla ya kufikishwa katika Mahakama ya Kisutu kujibu tuhuma zinazomkabili.

Akiwa katika Mahakama hiyo, Mchina huyo aliwaacha hoi wananchi waliokuwepo baada kuangua kilio kama mtoto akiomba msaada wa dhamana.

Hatua ya Sao Tong kulia mahakamani hapo, ilitokana na Mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi Nassoro Sisiwayah aliyekuwa akiendesha kesi hiyo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo John Msafiri kumuwekea pingamizi la dhamana.

Ndugu wa Mchina huyo waliokuwa wameongozana naye mahakamani hapo walikuwa na wakati mgumu kutokana na kutojua Kiswahili wala Kiingereza hivyo, kushindwa kuifuatilia kesi hiyo.

Hata hivyo, Sao Tong alikanusha kutenda kosa hilo na kutupwa rumande hadi Aprili 9, mwaka huu kesi yake itakapotajwa tena.

No comments: