Friday, March 14, 2008

Nora azua kasheshe


Shuhuda wetu alisema, Nora alianzisha vurugu hizo mara baada ya kurejea kutoka matembezini saa 10 alfajiri huku akiwa amefuatana na mwanaume aliyedaiwa ni mchumba wake na alipogonga mlango ili afunguliwe mtoto wa mwenye nyumba ambaye ndiye anayemfungulia kila mara aligoma kufanya hivyo.

Chanzo chetu kilisema, baada ya kukataliwa kufunguliwa ndipo Nora alipoamua kwenda kumgongea mama mwenye nyumba huku akiporomosha matusi mazito na kudai iwapo hawataki kumfungulia wamrudishie kodi yake ili akapange kwingine.

Shuhuda wetu alisema, baada ya kuona juhudi zake za kutaka kufunguliwa mlango zinazidi kugonga mwamba, alizidi kupiga kelele huku akianza kuvua blauzi aliyovaa na kubaki tupu, hivyo kusababisha baadhi ya majirani kumshangaa kwa kitendo hicho.

Mwenye nyumba kwa kuepusha shari aliamua kufungua mlango, lakini hiyo inadaiwa kumpa nafasi mwanaume aliyefuatana na Nora kumtwanga chupa mtoto wa mwenye nyumba ambaye awali ndiye aliyegoma kuwafungulia mlango. Rafiki huyo wa Nora amefunguliwa mashitaka na anasakwa na polisi kwa hati na. MK/RB/63/08.

Mwandishi Wa habari hizi ilibidi aende katika nyumba anayoishi Nora ambapo mama mwenye nyumba aliyejulikana kwa jina la Mama Hilda, alikiri kumfukuza msanii huyo kutokana na vurugu zake ambazo alidai zimevuka mpaka.

No comments: