Friday, July 1, 2011

Sh 700 milioni kutumika kwa maji Muheza

Thursday, 30 June 2011 20:04
0digg

Steven William, Muheza

HALMASHAURI ya Wilaya ya Muheza kwa mwaka 2011/12 inatarajia kutumia Sh 700 milioni kwa ajili ya miradi ya maji.Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Ummy Ally Mwalimu alitoa taarifa hiyo katika ukumbi wa Tarecu wakati wa hafla ya kuchangia ujenzi wa mradi wa kisima kirefu cha maji uliobuniwa na vijana wa Kanisa la Elimu Pentecoste Mtaa wa Masuguru.

Mwaimu alisema Serikali kupitia halmashauri ya wilaya hiyo imepanga kuchimba visima virefu vitatu, kununua pump nne na kujenga matanki ya kuhifadhia maji, kulaza mabomba kilomita tatu hapa mjini ikiwa ni jitihada za kuboresha upatikanaji maji.

Alisema mpango wa Serikali wa muda mrefu ni kutoa maji ya mtiririko kutoka Mto Derema umbali wa kilomita 22 hadi Muheza mjini na kwamba mipango imekamilika na taarifa zipo wizarani za maradi huo.

Naibu Waziri huyo alisema kuwa yeye kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Muheza atahakikisha mradi huo wa Derema unaanza kama ulivyopangwa kwani hiyo ni ilani ya CCM kutatua matatizo ya wananchi wake.

Mwalimu alisema kuwa kuna mpango wa upatikanaji maji vijijini pia kuna mradi wa kuchimba visima virefu katika vijiji tisa na kazi tayari imeshaanza.

No comments: