Friday, October 29, 2010

CUF kulia na mafisadi

na Bakari Kimwanga




MGOMBEA udiwani wa Kata ya Makurumla kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Chomeka Hamisi, ameapa kupambana na ufisadi katika kata hiyo.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa sisi kwa sisi, alisema akichaguliwa atawasilisha hoja binafsi ya kuomba maelezo ya fedha za miradi ya maendeleo zilizotolewa na manispaa.

Alisema katika uongozi wake atahakikisha kunakuwapo na utaratibu wa kufanya mikutano ya wananachi na kujua matatizo yao kila baada ya miezi mitatu na kuonyesha tofauti na kiongozi aliyemtangulia.

“Nina dhamira ya dhati ya kuleta maendeleo katika kata yangu na kila baada ya miezi mitatu nitakuwa nikifanya mikutano ya wakazi katika mitaa yangu, na nitahakikisha nawasilisha hoja binafsi na kuhoji fedha za miradi ya mendeleo na kama kuna ufisadi tutashughulika nao,” alisema Chomeka.

Aidha, alisema katika siku chache zilizobaki amewataka wananchi wa kata hiyo kuwa makini na watu wanaonunua shahada za kupigia kura, ili waweze kutumia haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi bora na si bora kiongozi.

No comments: