Monday, November 23, 2009

Shoga Katika Skendo la Ngono la Italia Achomwa Moto


Shoga raia wa Brazili mkazi wa Italia ambaye alihusika katika skendo la ngono la nchini Italia ambalo lilisababisha gavana wa jiji la Lazio kujiuzulu, amefariki kwa kuchomwa moto ndani ya nyumba yake katika mji wa Roma.

Vyombo vya habari vya Italia, viliripoti kuwa chupa ya pombe kali aina ya whisky ilikutwa pembeni ya mwili wa shoga huyo aliyejulikana kwa jina la Brenda.

Gavana wa Lazio, Piero Marrazzo, alijiuzulu nafasi yake mwezi uliopita baada ya video ya ngono akijivinjari na shoga huyo kuvuja kwenye vyombo vya habari.

Mwanzoni mwa mwezi huu, Brenda aliwaita polisi na kutoa taarifa kuwa ameshambuliwa na kuporwa mali zake mtaani.

Brenda na shoga mwingine wa kibrazili aliyejulikana kama Natalie walihusika kwenye skendo la ngono lililopelekea gavana Marrazzo ajiuzulu.

Polisi wanne waliochukua video kwa siri wakati gavana huyo akijivinjari na mashoga hao, walijaribu kujipatia pesa toka kwa gavana huyo kwa kutishia kuiweka hadharani video hiyo lakini walikamatwa na kutiwa mbaroni.

Gavana Marrazzo alijiuzulu huku akikiri kuwa na uhusiano na mashoga wanaofanya uhakaba.

Mwanasheria wa gavana huyo amewataka polisi kumpa ulinzi shoga Natalie ili na yeye yasije yakamkuta kama yaliyomkuta rafiki yake.

No comments: