Saturday, November 21, 2009

Mwanamke Aliyezini Auliwa Kwa Kupigwa Mawe


Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 20 mkazi wa mji mmoja kusini mwa Somalia alihukumiwa adhabu ya kifo kwa kitendo chake cha kuzini na mahakama ya kiislamu katika maeneo yanayotaliwa na kundi la wanamgambo wa Al Shabbab.

Mwanamke huyo ambaye alipata mimba baada ya kuzini na baadae kujifungua mtoto mfu, alifukiwa nusu ya mwili wake na kisha kupigwa mawe hadi alipofariki.

Katika tukio hilo lililofanyika mbele ya hadhara, lilishuhudiwa na takribani watu 200.

Mwanaume mwenye umri wa miaka 29 aliyezini na mwanamke huyo naye aliadhibiwa kwa kucharazwa bakora 100 mbele ya hadhara kwakuwa yeye alikuwa hajaoa.

Kwa mujibu wa sheria za kiislamu, mtu anayetoka nje ya ndoa yake na kwenda kuzini hufukiwa nusu ya mwili wake na kupigwa mawe hadi atakapofariki, lakini iwapo atafanikiwa kujinasua kutoka katika shimo alilofukiwa na kutoka nje adhabu hiyo husitishwa na hataendelea kupigwa mawe.

Mtu ambaye hajaoa au kuolewa anayetembea na wake au waume za watu huadhibiwa kucharazwa bakora 100 mbele ya hadhara.

Jumla ya watu wanne waliuliwa mwaka jana nchini Somalia kwa kupigwa mawe kwa makosa ya uzinifu.

No comments: