Saturday, November 21, 2009

Wamefanya filamu Danguro


Aliyekuwa mwanamuziki na sasa kageukia tasnia ya filamu Joan amesema kuwa baadhi ya wasanii wa kike wamegeuza filamu kama sehemu ya kufanyia umalaya na mambo yao machafu ambayo ni kinyume na maadili.


"Ukiangalia hali ilivyo, inatisha sana. Yaani katika kipindi cha karibuni watu wa ajabu ajabu wamevamia kwenye filamu na kuvuruga mambo kabisa," anasema msanii huyo ambaye amewahi kuwa mwanamuziki ingawa hakufanikiwa sana.

"Wameingia watu ambao kazi yao ni kuuza sura, kufanya umalaya na mambo machafumachafu ambayo hayafai kabisa kwenye jamii.

"Mtu anafikiri kuwa akiwa na sura nzuri ndio tiketi ya kuwa msanii wa filamu matokeo yake wakiingia ndio wanatumia hiyo hali kufanya uchafu wao na wenyewe wanaona sawa tu na wanafurahia.

"We angalia kila siku ya Mungu lazima utaona kwenye gazeti au utasikia msanii wa filamu kafanya upuuzi ambao unatia aibu mara huyu kachukua mme wa mtu, mwingine kafanya fujo akigombea mwanaume.

Ni juzi tu maneno kama haya yaliongelewa na muigizaji mwengine Yvonne Cherry maarufu kama Monalisa

No comments: