Saturday, November 21, 2009

Busta Rhymes Kuinogesha Fiesta Jioni Hii


Tamasha hilo ambalo tayari limeshaanza, na kuandaliwa na Clouds FM linafanyika kwa mara ya 10 na linashirikisha wasanii mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Ruge Mutahaba amesema Rhymes ametua nchi akiwa na kundi lake lenye wasanii tisa tayari kwa kuwapa burudani mashabiki.

Tamasha hilo linafanyika kwenye viwanja vya kilichokuwa Chuo cha Kampuni ya Simu Tanzania, Kijitonyama, Dar es Salaam.

Mutahaba alisema nyota wa hip hop atatumbuiza kwa muda wa saa moja na nusu bila mapumziko lengo ni kuwapa burudani ya kutosha mashabiki wake na kwamba mwaka huu tamasha hilo litakuwa la aina yake.

Alisema litakuwa majukwaa matatu ambayo yote yatakuwa bize na hakutakuwa na muda wa kupumzika kwa wasanii.

"Rhymes ni msanii mahiri ambaye amewahi kupata tuzo mbalimbali za billboard, ni msanii anayebadilika kulingana na mazingira anakubalika kwa vijana na wazee,"alisema mratibu huyo.

Baadhi ya nyimbo ambazo anatamba nazo msanii huyo ni pamoja na Arab money, Turn it Up, Woo Hah, Make it Clap ambao kamshirikisha Spliff Star, Hey Ladies, I ever saw on.

Msanii huyo wa kimataifa atashirikiana na wasanii wa wazawa wakiwamo Ali Kiba, Marlow, Barnabas, Daz Nundaz, Bushoke, TMK Famili, Juma Nature na Wanaume Halisi, Profesa Jay, Belenine, Hussein Machozi, Lady Jaydee na Ray C

No comments: