Tuesday, August 4, 2009

Nipo fiti…Banza Stone!Banza Stone mwana wa Masanja achonga na Mafia Kisiwani na kudai kuwa yupo fiti na atarudi hivyo mashabiki wake wasichoke kumsubiri. Haya ni maswali mafupi aliyohojiwa na Mafiakisiwani.

Mafiakisiwani: Banza mashabiki wako wanakuuliza upo wapi na unafanya nini?

Banza: Nipo ila kuna mambo fulani yalikuwa yananiweka vibaya ila siku si nyingi nitaweza kusikika tena na mashabiki wangu.

Mafiakisiwani: Vipi madai ya kuwa unaumwa na uzushi wa kifo?

Banza: Kwakweli ndio maana naitwa Makaveli kwakuwa kila siku nazushiwa kifo lakini kama unavyoniona,mimi ni mzima wa afya njema.

Mafiakisiwani: Banza unasumbuliwa na nini hasa kwasababu tunaona tu kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuwa unaumwa,nini hasa kinachokusumbua?

Banza: Nasumbuliwa na kichwa pamoja na malaria na si kinginecho.

Ma: Je mashabiki wako wategemee nini kutoka kwako?

Banza: Wategemee kitu special,nitatoa wimbo maalumu kwa wale wote wanaonisema vibaya.

Mafiakisiwani: Asante Banza

No comments: