Tuesday, August 4, 2009

Kunguru weusi marufuku Dar.


Kunguru weusi waliotapakaa jijini Dar-es-salaam wamepigwa marufuku jijini Dar-es-salaam kwakuwa wameonekana kuwa ni waharibifu na wanahatarisha maisha ya binadamu na wanyama.
Akiongea na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-salaam,William Lukuvi alisema kuwa hapo mwanzo kunguru hao walipelekwa Zenji (Zanzibar) kwa lengo la kula wadudu waliokuwa wanaharibu zao la karafuu visiwani humo lakini tatizo linakuja kuwa wanazaliana kwa haraka bila mpango wowote na sasa wanafanya uharibifu katika maeneo mbalimbali ya mji.
Kutokana na hilo Mkuu huyu wa mkoa ameomba kwa mtu yeyote mwenye uwezo wa kuwaangamiza kunguru hawa afanye hivyo kwasababu ni waharibifu wakubwa

No comments: