Monday, June 15, 2009

MSINISEME”-ALI KIBA

Mpaka hivi sasa yeye ndio anashikilia rekodi ya msanii wa Bongo Fleva ambaye amefanya ziara ndefu ya kimuziki nje ya Afrika Mashariki.Hapa tunamuongelea kijana Ali Kiba ambaye jumamosi hii atakuwa Washington D.C katika muendelezo wa ziara zake.

Wakati anaendelea na ziara,Ali Kiba ameachia single yake inayokwenda kwa jina Msiniseme. Tofauti na nyimbo zake nyingi,hii imekaa kwa kuchezeka zaidi ndani ya club au sehemu yeyote ya kujirusha.Lipo pia swali ambalo tumetumiwa na msomaji wetu mmoja.Anataka ufafanuzi kwamba Ali Kiba anatokea wapi.Ni Mkenya au Mtanzania? Anasema amesikia sehemu mbalimbali Wakenya wakisema Ali Kiba ni mtu wa kwao wakati anavyojua yeye Ali Kiba ni Mtanzania.

Kwa faida ya msomaji wetu na wengine wengi,tunavyojua sisi Ali Kiba ni mtanzania.Nyumbani kwao ni Kariakoo jijini Dar-es-salaam.

No comments: