Sunday, March 1, 2009

INAFRIKA BAND ZIARANI EUROPEBila shaka unawatambua wana Inafrika Band.Hivi sasa bendi hiyo machachari wapo katika ziara ndefu ya nchi za Ulaya.Wakiwa huko huko ziarani,Inafrika wamekamilisha albamu yao ya pili ambayo imekuwa mastered nchini Ujerumani. Wanatarajia kuitoa rasmi watakaporejea nchini Tanzania mwezi Aprili.Albamu itakwenda kwa jina Mbeleko.

Sisi hapa MK hatuna la zaidi bali kuwatakia Inafrika Band ziara njema. Endeleeni kutuwakilisha huko.Ni matumaini yetu kwamba mtatutumia japo single moja kutoka ndani ya Mbeleko ili nasi tuiweke hapa ili wapenzi wa muziki wapate nafasi ya kusikia vionjo vilivyomo.

No comments: