Sunday, March 1, 2009

IJUMAA SEXIEST GIRL: NANI KUIBUKA MSHINDI?

1.Irene Uwoya


Wema Sepetu
Kwa muda sasa jamaa wa Global Publishers,kupitia gazeti lao la Ijumaa,wamekuwa wakiendesha shindano lililojulikana kama Ijumaa Sexiest Girl.Kilichokuwa kinafanyika ni kwamba kila wiki mrembo mmoja alikuwa anatolewa baada ya kupata kura za chini kushinda wengine.Wapiga kura walikuwa ni wananchi,wasomaji wa gazeti la Ijumaa.Kulikuwa na namba ya simu +255 784 275 714 ambapo wananchi walikuwa wanatuma ujumbe mfupi wa maneno(SMS) wakimpendekeza msichana ambaye kwa mujibu wao anastahili kushinda.Jumla ya warembo 12 walishirikishwa katika shindano hili.Unaweza kusoma zaidi kuhusu shindano hilo kwa kutembelea tovuti ya Global Publishersna kisha katika Search andika Ijumaa Sexiest Girl.

Sasa baada ya mchakamchaka mzima,warembo wawili, Irene Uwoya na Wema Sepetu(pichani) ndio wamebakia na mshindi anatarajiwa kutangazwa Ijumaa ijayo. Inawezekana hukupata nafasi ya kupiga kura wakati shindano lilipokuwa linaendelea.Pamoja na hayo,hapa una nafasi ya kutoa maoni yako.Nani unadhani ataibuka mshindi?Kwanini?

No comments: