Friday, February 20, 2009

Picha ya kwanza ya Rihanna baada ya kushambuliwa na Chris Brown


Baada ya picha kadhaa feki kutoka, picha ya kwanza ya kweli inayomwonyesha Rihanna baada ya kupewa mkong'oto na mpenzi wake Chris Brown imetoka ikionyesha jinsi sura yake na mdomo wake ulivyoharibiwa vibaya.
Picha ya kwanza ya Rihanna baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa na mpenzi wake Chris Brown imetolewa hadharani.

Picha hiyo ilitolewa na webiste ya udaku ya TMZ.com. Ingawa hawakutaja jinsi walivyoipata picha hiyo, Picha hiyo inaaminika ndio picha iliyotumika katika ushahidi wa polisi.

Picha hiyo imetoka baada ya picha kibao feki za kujeruhiwa kwa Rihanna kusambaa kwenye mitandao.

Mwanzoni mwa wiki hii Chris Brown aliomba radhi na kusema kuwa amesikitishwa sana na alikuwa anatafuta watu wa kumpa ushauri nasaha.

Mwanamuziki huyo nyota alikamatwa baada ya kumtishia maisha Rihanna baada ya tukio hilo lililotokea masaa machache kabla ya usiku wa Grammy Awards.

Polisi wa Los Angeles wanaendelea na uchunguzi wao na msemaji wa polisi alisema kwamba mwendesha mashtaka wa LA bado hajatoa uamuzi wa kufunguliwa kwa jalada la kesi hiyo.

Rihanna alishambuliwa na mpenzi wake baada ya kutokea mabishano makali baina yao wakiwa kwenye gari wakati wanatoka kwenye sherehe iliyoandaliwa kabla ya Grammy Awards.

Kampuni inayorekodi nyimbo za Chris Brown iko kwenye shinikizo kubwa la watu wanaolaani kupigwa kwa Rihanna wakiitaka kampuni hiyo imtose mwanamuziki huyo.

Wacheza mieleka wa Marekani nao hawakukaa nyuma katika suala hili kwa kumualika Chris Brown aende akashiriki mchezo huo kwakuwa wamegundua ana kipaji cha mchezo huo.

No comments: