Wednesday, February 25, 2009

MWENYEKITI NA KATIBU WAKE


Wiki iliyopita,katika viwanja vya Leaders Club kulianzishwa Shirikisho la Wasanii wa Muziki Wa Kizazi kipya. Shirikisho hilo limepewa jina la Tanzania Flavour Unity.

Kuanzishwa kwa shirikisho hilo kulikwenda sambamba na zoezi la kuchagua viongozi wake ambapo Lady Jay Dee alichaguliwa kuwa Mwenyekiti na Banana Zorro akichaguliwa kuwa Katibu wa umoja huo. TID alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti.

Mojawapo ya malengo makubwa ni pamoja na kujiweka sawa kupokea msaada mkubwa wa Mastering Studio ambao Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliwaahidi wasanii wakati alipozungumza wakati wa sherehe za kutimiza miaka miwili ya kituo cha kulea vipaji cha Tanzania, THT(Tanzania House of Talent).

No comments: