Monday, August 25, 2008

Mtoto wa mwanaume aliyejifungua huyu hapa


Hatua hiyo imekuja huku kampuni moja ya Filamu ya nchini Uingereza iitwayo September Films ikiwa na haki ya kutengeneza ‘dokumentari’ ya maisha ya mwanaume huyo na mwanae baada ya kutoa mamilioni ya fedha.

Picha hiyo (iliyopo ukurasa wa mbele), inamuonesha mtoto huyo akiwa na afya nzuri tofauti na baadhi ya watu walivyobashiri kuwa, asingeweza kuzaliwa salama.

Aidha,Thomas amekuwa akikaririwa mara kwa mara na vyombo mbalimbali vya habari akielezea furaha aliyonayo kwa kujifungua mtoto huyo wa kike.

“Mwanangu Suzan ni mzuri mno, hakika sichoki kumtazama kila wakati,” alikaririwa akisema Thomas.

Awali, Thomas alikuwa na jinsia ya kike akiitwa Tracy Lagondin lakini alipofikisha umri wa mika 20 alijibadilisha na kuwa mwanaume kisha kumuoa mwanamke aitwae Nancy huku akiacha viungo vyake vya uzazi kama vilivyo.

Hata hivyo, baadae alijipandikiza mbegu za kiume kwa njia ya kitaalamu na kufanikiwa kubeba ujauzito kisha kujifungua salama salimin.

No comments: