Monday, August 25, 2008

Mke wa kigogo 'agawa utamu' kweupe


Christopher Lissa na Richard Bukos
Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Lucy, huku mume wake akijitambulisha kuwa ni Kigogo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wikiendi iliyopita, alijikuta akigawa utamu (kukaa uchi) kweupe katika tukio la fumanizi, Ijumaa Wikienda lilishuhudia...
Lucy, aligawa utamu huo, Jumamosi (Agosti 23), saa nane usiku, wakati alipotwangana na mgoni wake ambaye jina lake, halikupatikana mara moja, katika Ukumbi wa Africentre, Ilala, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa ushuhuda wetu, chanzo cha varangati ni Lucy, kubaini uwepo wa mawasiliano ya kimapenzi kati ya mume wake na mwanamke mwingine, aliyekuwa ameketi kwenye meza jirani yao.

Mke huyo wa kigogo ambaye alikuwa amekwishajitwika ‘glasi’ kadhaa, alibaini kwamba mumewe na mgoni wake, walikuwa ‘wakichati’ kwa namna fulani, iliyoashiria kwamba kama angezubaa, angeibiwa.

Timu yetu ambayo ilikuwa ikifuatilia ‘mkanda’ huo kwa ukaribu, baadaye ilimshuhudia Lucy akimpiga maswali mumewe, kuhusu mazungumzo yake na mwanamke huyo wa meza jirani yao.

Hata hivyo, katika kile ambacho kilionekana kutoridhishwa na majibu ya mume wake, mke huyo wa kigogo, aliinuka kwa hasira na kumpiga chupa ya bia mgoni wake, ingawa ilimkosa.

Tukio hilo la kurusha chupa, liliamsha varangati zito, kwani mwanamke aliyekusudiwa kupigwa, aliamka na kumrudi vilivyo Lucy, huku mumewe akishindwa kufanya lolote.

Baadaye, walinzi wa ukumbi huo, waliingilia kati na kuamulia ugomvi huo, kwa kumtoa nje mwanamke ‘mfumaniwa’.
Pamoja na hilo, mke huyo wa kigogo hakuridhika, alimfuata nje ya ukumbi mgoni wake ili waendelee kutwangana, jambo ambalo liliwaudhi vijana wanaohusika na ulinzi katika eneo hilo ambao waliamua kumchapa makofi kwa kumgombania ili kumtuliza.

Ugomvi huo ulidumu kwa takriban saa mbili na dakika kadhaa, kwani mwanamke aliyetolewa nje, alifuata ‘kampani’ yake na kurudi kufanya fujo ukumbini hapo, ingawa jitihada za mabaunsa’, zilizima sekeseke hilo mnamo saa 10:15 usiku.

Kuzuka kwa varangati hilo, kuliwafanya wanamuziki, Joseph Haule ‘Prof Jay’, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ na Ambwene Yesaya ‘AY’ kukosa uzalendo wa kuendelea kumuenzi aliyekuwa galacha wa Hip Hop nchini, Marehemu Simon Sayi ‘Complex’.

Wanamuziki hao, mara tu ugomvi huo ulipoanza, walianza kuondoka mmoja baada ya mwingine na kuacha shughuli nzima ya kumkumbuka Complex ikiendelea.

Prof Jay, FA, AY na wasanii wengine, walikutana Africentre katika Tamasha la Remember August ambalo lilikuwa ni maalumu kwa ajili ya kumkumbuka Complex na wasanii wengine waliotangulia mbele ya haki. Picha zaidi kuhusu tukio hilo, zipo ukurasa wa sita.

No comments: