Friday, November 30, 2007

FUMANIZI


Kwa mujibu wa shuhuda aliyekuwepo eneo la tukio ambaye alifanikiwa kupiga picha kibao (tumezipachipisha ukurasa wa mbele), Mwarabu huyo akiwa na mwenzake aliyefahamika kwa jina la Hassan waliopoa machangudoa wawili akiwemo Ester kwa ajili ya kufanya nao mapenzi.

Mnyetishaji wetu alisema kuwa watu hao huku kila mmoja akiwa na mwenza wake walikubaliana kupeana mapenzi kwa usiku mzima kwa malipo ya shilingi 100,000 kwa kila changudoa.

Habari zaidi zilidai, Waarabu hao walikwenda hadi Holiday Inn na kukodi chumba kilichokuwa na vitanda viwili (double) ambako walijipumzisha na machangudoa wao hadi asubuhi.
Ilidaiwa kuwa mapema asubuhi mmoja kati ya wanaume hao ambaye alikuwa na Ester aliaga kuwa anakwenda kunywa chai kwenye mgahawa wa hoteli hiyo.

Aidha baada ya kuagwa, changudoa huyo alimwambia njemba wake asiondoke mpaka amlipe kwanza fedha walizokuwa wamekubaliana.

“Ester hakukubali, alitaka alipwe shilingi 100,000 yake kabla jamaa hajatoka chumbani humo, wakati akidai hivyo Mwarabu huyo akachomka ghafla, jambo lililomfanya changudoa huyo amkimbize,” kilisema chanzo chetu.

Aliongeza kuwa wakati wakifukuzana, Mwarabu mwenzake aliamka na kutoweka huku akimwacha changudoa aliyekuwa naye akiwa usingizini kutokana na pombe aliyokunywa.

Chanzo hicho kilisema kuwa changudoa aliyeachwa chumbani alipoamka hakuwakuta wenzake na ndipo alitoka chumbani na kumkuta Ester akiwa katika mshikemshike wa kudai ujira wake.

Habari zaidi zilidai, vurumai kubwa ilitokea hadi katika lango la kuegeshea magari ambapo ngumi ziliendelea kupigwa hatua iliyofanya taulo alilokuwa amevaa Ester kudondoka na kumwacha mtupu.

Tukio hilo lilikusanya watu wengi wakiwemo walinzi wa hoteli hiyo ambao walikuwa wakishangilia kwa kusema “hii ni sinema ya bure.”

Aidha wakati ugomvi huo ukiendelea, changudoa huyo alisikika akisema “huwezi kuni**** bure, nilipe laki moja yangu,” alitoa kauli hiyo huku akimng’ata meno mgomvi wake sehemu mbali mbali za mwili.

Kufuatia vurugu hizo, walinzi wa hoteli hiyo walitoa taarifa polisi ambapo walifika na kumkamata Ester na Mwarabu huyo, pamoja na changudoa mwingine waliyekuwa naye na kuwapeleka Kituo cha Polisi Gymkhana ambapo walihojiwa.

Wakati wakihojiwa, Ester alifanya fujo kituoni hapo hatua iliyowafanya askari wawahamishie Kituo Kikuu cha Polisi ‘Central Police” ambapo katika maelezo yake changudoa huyo alidai kuwa kabakwa, hatua iliyomfanya Mwarabu afunguliwe kesi kwa jalada namba CD/RB/10818/07 KUBAKA.

Aidha, Mwarabu huyo alitiwa rumande hadi Jumapili iliyopita alipopewa dhamana ambapo alitarajiwa kupelekwa mahakamani wakati wowote baada ya upelelezi kukamilika.
Akiongea na mwandishi wetu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Masindoki Masindoki alisema hajapelekewa kesi hiyo katika ofisi yake.

“Unasema kosa lenyewe ni kutolipa ngono? Sijawahi kuona chaji kama hiyo, lakini kama kulikuwa na shambulio, basi itakuwa ni kosa dogo sana na ndiyo maana halijafika mezani kwangu hadi sasa, acha nilifanyie kazi,” alisema Masindoki.

No comments: