Monday, December 3, 2007

WAZIRI AUNDA TUME NYINGINE


Profesa Mwakyusa alitoa kauli ya kuundwa kwa tume yake hiyo mpya alipoitisha mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ofisini kwake jana (Ijumaa).


Waziri huyo alihidi kuwa angetoa taarifa ya ripoti ya tume ya Profesa Maseru jana ambapo wananchi walikuwa wakiisubiri kwa shauku kubwa.

Akizungumzia tume ya awali iliyoundwa na Profesa Maseru, Waziri Mwakyusa alisema kuwa kulikuwa na mambo ya msingi yaliyokosekana na yaliyohitaji ufafanuzi ili kuwezesha serikali kutoa uamuzi sahihi.

"Kuna baadhi ya mambo ya msingi ambayo yalihitajika yapatiwe ufafanuzi ili kuiwezesha serikali kutoa uamuzi ulio sasa hii," alisema Waziri Mwakyusa.

Waziri huyo alisema kuwa kutokana na umuhimu wa suala hilo ameamua kuuunda tume yake ya watu watano ambayo itaongozwa na Profesa William Mahalu kutoka Hospitali ya Bugando, Mwanza.

Alisema tume hiyo inatakiwa kuanza kazi yake Novemba 26, na kumaliza Desemba 2, mwaka huu. "Tume hiyo imejumuhisha wataalamu wa afya, menejimenti na sheria," alisema waziri.

Novemba Mosi mwaka huu, Emmannuel Mgaya alifanyiwa upasuaji wa mguu badala ya kichwa na Emmanuel Didas alifanyiwa upasuaji wa kichwa badala ya mguu.

Hata hivyo, wakati tume hiyo ya Waziri Mwakyusa inaundwa mgonjwa Emmanuel Mgaya ameshafariki dunia juzi (Alhamisi) na Emmanuel Didas anatarajiwa kupelekwa nchini India kwa matibabu zaidi kwani hali yake bado ni mbaya.

No comments: