Friday, November 30, 2007

AIBU!Amani lilifanikiwa kupata baadhi ya picha hizo kutoka kwa mwanafunzi mmoja wa shule ya sekondari (jina lake na shule vinahifadhiwa) ambapo taarifa za awali zilishindwa kuthibitisha madhumuni ya watu hao kupiga picha hizo chafu.

Aidha uchunguzi uliofanywa na gazeti hili ulibaini kuwepo kwa picha nyingi zisizofaa katika maeneo mengi ya mji ambapo, madai ya kuzifanyia biashara na pengine kuwadhalilisha wanawake mbele ya waume wao yametolewa.

"Kuna wanaotafuta soko la ukahaba na wengine wanawapiga picha wanawake walioolewa kwa lengo la kuwatia aibu kwa waume zao, si unajua inawezekana msichana akawa kaolewa lakini akawa na mwanaume mwingine, bila kujua anaweza kujikuta anapigwa picha chafu na hawara yake.

"Sasa wanapokosana ndiyo inatokea hali kama hii ya kusambaza picha kwa lengo la kumfedhehesha kwa mumewe na jamaa zake," alisema kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Super na kuongeza kuwa, mkasa wa picha za utupu umewahi kumkumba pia mke wa rafiki yake.

Baada ya Gazeti hili kunasa picha kadhaa zikiwemo zilizotumika ukurasa wa mbele, uchunguzi wa kina wa kuwasaka watuhumiwa hao ulifanyika ambapo wanahabari wetu walifanikiwa kupata namba ya simu ya Mpemba, lakini baada ya kuwasiliana naye mtu aliyepokea alikana kuwa yeye sio mtuhumiwa, huku akijitambulisha kwa jina la Shabani Salum.

Aidha, Amani lilifanikiwa kumpata mwanamke aitwaye Flora James ambaye picha zake za utupu hazikuchapishwa, alipoziona alikiri kupiga picha hizo kwa lengo la kuweka kumbukumbu.

"Aaa jamani msizitoe picha hizo, nilipiga na mpenzi wangu kwa lengo la kumbukumbu tu, halafu hiyo ilikuwa ni zamani sana kabla hata sijaolewa, sasa mkizichapisha nitaachika."

Kwa kipindi kirefu Serikali pamoja na vyombo mbalimbali vya habari vimekuwa vikikemea tabia ya baadhi ya watu kupiga picha za utupu kwa kulinda maadili ya nchi yetu lakini, kuna wanaoziba masikio na kuendelea na vitendo hivyo viovu .

Tunaikemea tabia hiyo na tunawaomba wenye nayo kuacha mara moja laa sivyo tutawaanika ili jamii iwabaini na kuwahukumu

No comments: