Tuesday, July 10, 2007

KIASI cha Shilingi milioni 49.865,000 kilikusanywa mlangoni katika mechi ya fainali ya Ligi Ndogo baina ya watani wa jadi katika soka nchini, Simba na Yanga, kiwango ambacho kimepita mapato ya mwaka 2005.
Katika marudiano baina ya timu hizo msimu wa mwaka 2005, timu hizo ziliingiza Sh Shilingi milioni 48.3, mechi ambayo Simba iliondoka na ushindi wa mabao 2-1.
Katibu mkuu wa Chama cha Soka cha Morogoro (MRFA), Aristo Nikitas aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mapato hayo yalitokana na watazamaji 9,758 walioingia Uwanja wa Jamhuri kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha Sh 30,000 kwa Jukwaa Kuu, Sh 10,000 kwa sehemu iliyo chini ya paa na Sh 5,000 kwa mzunguko.
Nikitas alisema kutokana na mapato hayo ya mechi hiyo ambayo Simba ilishinda kwa penati 4-3 baada ya timu hizo kufungana bao 1-1 katika muda wa dakika 120, kila timu imepata Shilingi milioni 12,367,145 huku Shirikisho la Soka (TFF) likipata Sh milioni 9,608,194. MRFA imejipatia Shilingi milioni 1.8, uwanja Sh milioni 4,178,780 na gharama nyingine za mchezo zikiwa Sh milioni 4,178,780.
Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi mkoani hapa linawashikilia watu wawiliwakituhumiwa kukutwa wakiuza tiketi feki za kuingilia katika mchezo huo.
Kamanda wa polisi mkoani hapa, Thobias Andengenye aliwataja watu wanaoshikiliwana jeshi hilo kuwa ni Omari Kwasa (32) mkazi wa mji mpya mkoani hapa na Dotto Malenda (25), ambaye ni muuza mitumba na mkazi Kichangani mkoani hapa.

No comments: