Tuesday, July 10, 2007

JAJI Mkuu, Barnabas Samata, amesema kila mkoa nchini utakuwa na jengo la Mahakama Kuu ili kusogeza huduma zake kwa wananchi.
Akizungumza na wakazi wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro juzi baada ya kuzindua jengo jipya la Mahakama ya Wilaya hiyo, Samata alisema kuwa, tayari viwanja vya kujenga majengo hayo kwenye mikoa husika vimepatikana na kinachosubiriwa ni fedha kutoka serikalini.
Jaji Mkuu alisema ujenzi huo, utaambatana na ya Mahakama Kuu na kufanyiwa ukarabati yaliyochakaa ili ili yasiendelee kuwa magofu.
Samatta aliipongeza Kampuni ya Ujenzi ya Jeshi la Kujenga Taifa ya Suma-JKT(NSCD) kwa utalaamu mkubwa iliyoutumia katika ujenzi wa mahakama hiyo ya wilaya ya Hai.
?Napenda niipongeze Kampuni ya ujenzi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), imefanya kazi nzuri na ya kitaalamu katika ujenzi wa jengo hili la mahakama? kumbi za kuendeshea kesi na vyumba vya mahabusu, pamoja na ofisi za mahakimu na makarani zinapendeza, ? alisema Samata.
Hata hivyo alisema ili sifa ya jengo hilo jipya iendelee kuwa na maana ni lazima watumishi wa mahakama hiyo wakiwamo mahakimu, watende haki kwa washtakiwa na walalamikaji.
Mapema Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Moshi, Njengafibile Mwaikugille, akimkaribisha Jaji Mkuu, alisema ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Hai, umegharimu zaidi ya Sh205milioni.
Jaji Mwaikugille, alisema hivi sasa jengo la mahakama hiyo linahitaji kuzungushiwa uzio, jengo la kupumzika wateja wa mahakama na ujenzi wa mgahawa kwa watumishi wake.

No comments: