Saturday, October 31, 2015

DALILI ZA DEMU MWENYE UCHI WENYE MAJI MENGI NA KINA KIREFU,KIDUME FAHAMU USIVAMIE TU!!,GONGA HAPA

MAPENZI 18+::: Dalili ni chache sana. Kuna watu wanasema mara nyingi mwanamke mwembamba ana uchi wenye kina kirefu sana kwa hiyo wanawake wengi wa sampuli hiyo wamebarikiwa. Lakini wanene wamenyimwa zawadi ya kina kirefu.Pia wengine wanadai kuwa ukiangalia mwanya uliopo kati ya dole gumba la mguuni na kidole kinachofuatia, utagundua kitu. Mwanamke mwenye mwanya mkubwa ana uchi mpana na mwenye kina sana na mwenye mdogo ana uchi mdogo.Tatu ni urefu wa kiganja pamoja na vidole vya mwanamke akivinyoosha. Kama virefu sana jua basi na kina cha uchi wake ni kirefu sana. Lakinikama kiganja na vidole vya mikononi ni vifupi, ujue kina ni kifupi pia!

UKAWA watoa tamko zito lenye masharti manne.

Taarifa iliyotolewa na viongozi hao jana kwa vyombo vya habari imetoa masharti manne kufuatia kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar. Sharti la kwanza ni kuzitaka mamlaka zinazosimamia Uchaguzi Mkuu huo kuondoa mara moja tangazo la kuufuta Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar. Sharti la pili ni kumtangaza Seif kuwa ni mshindi halali wa nafasi ya urais na hivyo aapishwe kuwa Rais wa nchi ya Zanzibar ambayo ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sharti la tatu, wametoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuingilia kati na kulaani kwa nguvu zote kinachofanyika Zanzibar ambako kwa mara nyingine tena demokrasia inataka kuminywa wazi wazi ili tu kuinusuru CCM isiondoke madarakani kama ambavyo wapiga kura wamekuwa wakiamua. Aidha sharti la nne ni kwa wananchi wa Zanzibar, “tunapenda kuwahakikishia kuwa tuko nao pamoja katika kipindi hiki kigumu cha kupigania mabadiliko . Kura za Urais Aidha wamedai ushindi wa urais umetengenezwa, kwenye taarifa rasmi ya NEC ambayo imetangaza hadharani na kunukuliwa kwenye vyombo vya habari kwamba; wapiga kura walikuwa 15,589,639. Katika uchaguzi huo kura zilizopigwa 15,193,862 na kati ya hizo zilizoharibika ni 402,248:”Kupitia hesabu hizo hapo juu unaweza kushuhudia upikwaji na utengenezwaji wa matokeo uliofanywa ili kuhujumu matokeo ya Lowassa kwa ajili ya kumbeba na kumpatia ushindi Dk. Magufuli ili kuinusuru CCM.” Viongozi hao walisema Ili kuthibitisha kauli yao kwamba wameongoza uchaguzi katika nafasi hiyo kwa Lowassa ndiye Rais aliyechaguliwa na Watanzania walio wengi walioshiriki uchaguzi Mkuu Oktoba 25. “Tunazitaka mamlaka zinazohusika, kwa mujibu wa katiba, sheria na taratibu za uchaguzi, zitengue matokeo batili waliyoyatangaza na zimtangaze mara moja Lowassa kuwa ni mshindi wa nafasi ya urais na Duni Juma Haji kuwa Makamu wa Rais,” walisema viongozi hao.

NEC YAMTANGAZA DKT MAGUFULI WA CCM KUWA RAIS WA TANZANIA 2015

Lubuva: Kwa kuwa mheshimiwa Dr. Magufuli, John Pombe Joseph wa CCM amepata kura nyingi zaidi kuliko mgombea mwingine yeyote, kwa niaba ya tume ya taifa ya uchaguzi na kwa mujibu wa vifungu vya 35(e), 35(f) na 81(b) vya sheria ya taifa ya uchaguzi sura 343. Ninatangaza rasmi matokeo ya uchaguzi ya urais wa mwaka 2015 kwamba Mheshimiwa Magufuli John Pombe Joseph amechaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Hassan Suluhu amechaguliwa kuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Asanteni kwa kunisikiliza. Matokeo ya Urais: DK. Magufuli atangazwa mshindi kwa asilimia 58.46 MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ( NEC), Jaji Mstaafu, Damian Lubuva, leo jioni amemtangaza mshindi wa kiti cha urais wa Tanzania wa mwaka 2015 kuwa ni Ndugu John Pombe Magufuli kutoka Chama cha Mapinduzi(CCM). Matokeo hayo ya uchaguzi huo, yametangazwa leo ambapo mwenyekiti huyo amemtangaza Dk. Magufuli kama rais wa Serikali ya awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere Dar es Salaam. Kabla ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Jaji Mstaafu, Lubuva alisema kwa mujibu wa Ibara ya 41(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwaka 1977 mgombea wa kiti cha urais atatangazwa kuwa amechaguliwa kuwa rais iwapo tu amepata kura nyingi kuliko mgombea mwingine yeyote. Aidha Lubuva, amesema kwa mujibu wa ibara ya 47(2) ya Katiba hiyo, mgombea wa kiti cha urais akichaguliwa basi na mgombea mwenza wake atakuwa Makamu wa Rais. ?Kwa kuwa Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli wa CCM amepata kura yingi kuliko mgombea yeyote, kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kwa mujibu wa vifungu vya 35E, 35F (8) na 81 B vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura 343, ninatangaza rasmi matokeo ya uchaguzi wa urais wa 2015. ?Mheshimiwa Mheshimiwa John Pombe amechaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Samia Hassan Suluhu amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,? alikaririwa na FikraPevu mwenyekiti huyo. Aliongeza kuwa idadi ya wapigakura waliojiandikisha ni 23, 161, 440, waliopiga kura ni 15, 589, 639 sawa na asilimia 67.31 ya wapiga kura wote waliojiandikisha. Alizitaja idadi ya kura halali kuwa ni kura halali 15, 193, 862 sawa 97.46% kura zilizokataliwa 402, 248 sawa 2.58% hivyo Magufuli amepata kura ambazo ni 8, 882, 935 sawa na 58.46% ya kura zote halali. Matokeo ya wagombea wengine akiwemo, Anna Mghwira wa (ACT-Wazalendo) 98,763 sawa 0.65%, Chifu Lutalosa Yemba (ADC), 66, 049 sawa na 0.435 huku Edward Lowassa (Chadema) akimfuatia kwa kura Dk. Magufuli kwa kupata kura 6, 772, 848, sawa 39.97% na Hashim Rungwe wa (CHAUMMA) aliyepata kura 49, 256, sawa na 0.32%. Wagombea akiwemo Janken Kasambala (NRA) 8, 028 sawa 0.03% na Maximilian Lyimo (TLP) 8, 198 sawa na 0.05% Fahmy Dovutwa (UPDP), 7, 785 sawa 0.05%. Hata hivyo, Vyama 6 vimesaini matokeo ya urais ambapo wagombea wawili wa vyama vya CHADEMA na CHAUMMA, hawajasini karatasi ya matokeo ya nafasi hiyo ya urais. Mkurugenzi wa Uchaguzi (NEC), Kailima Ramadhani amesema majimbo 6 hayajafanya uchaguzi na sababu mbalimbali ikiwemo vifo, wakati majimbo 5 hayajafanya uchaguzi kutokana na mapungufu mbalimbali.

Wednesday, August 19, 2015

Mafia yetu

Monday, August 3, 2015

Manji, Fella washinda Mbagala

By Waandishi Wetu, Mwananchi Dar es Salaam. Wadau wawili wa michezo na burudani nchini; Yusuf Manji na Said Fella wameibuka kidedea katika kinyang’anyiro cha udiwani katika jimbo jipya la Mbagala jijini hapa. Manji ambaye ni Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Quality Group, alishinda katika udiwani katika Kata ya Mbagala Kuu wakati Fella ambaye ni msimamizi wa kazi za wasanii na muasisi wa Kundi la Mkubwa na Wanawe, alishinda katika Kata ya Kilungure. Fella ni Meneja wa mwanamuziki maarufu nchini, Diamond Platnumz, TMK Family na Yamoto Band. Kaimu Katibu CCM Wilaya ya Temeke, Rutami Masunu alisema uchaguzi huo ulikwenda vizuri katika maeneo mengi isipokuwa changamoto kidogo katika kata moja ambayo itafanya uchaguzi huo leo. Alisema tayari matokeo ya kata 28 kati ya 32 za wilaya yake yamewasilishwa ofisini kwake na baada ya kuyapitia na kukusanya taarifa zinazowahusu madiwani na wabunge na muda wowote leo atatoa taarifa kamili. Vurugu Jangwani, Buguruni Uchaguzi wa kumteua mgombea wa udiwani Kata ya Jangwani wilayani Ilala, umeingia dosari baada ya kikundi cha vijana wanaosadikiwa kutokea Kinondoni kuvuruga upigaji kura na kuvunja hema jambo lililosababisha polisi kuingilia kati. Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Ramadhan Manda alisema jana kuwa kundi hilo linadaiwa kutumwa na watoto wa mmoja wa wagombea kutokana na dalili za wazi za kushindwa uchaguzi huo. Mkazi wa Mtaa wa Mtambani B, Suleiman Maarufu alisema: “Saa nne asubuhi nilisikia vurugu nje, nikatoka na kuona kikundi cha vijana kutoka Tawi la Mkombozi kikivutana na mmoja wa makada ninayemfahamu. Wale vijana wakapiga teke masanduku, wakavunja hema… sasa wakati naingia kuamulia, wakanipa misukosuko na kipigo na baada ya kuamka nikakuta nimeumia unyayoni na kwenye goti.” Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Ernest Chale alisema ni makundi matatu ya wagombea yaliyochangia kuibuka kwa vurugu hizo na kusababisha uchaguzi kutomalizika. “Kutokana na haya yaliyotokea tutakaa vikao vya siasa kujadili, kwa maana hiyo hii kata itaendeshwa kama eneo maalumu. Kinachoonekana hapa mtu anatafuta uongozi kwa nguvu lakini uongozi unatolewa na Mungu, mimi naona ni bora akatulia kama anaona haki haitatendeka ni bora angesubiri akate rufaa.” Mmoja ya wagombea wa udiwani, Abdul Faraji alisema: “Uchaguzi ilibidi ufanyike jana (juzi) na maeneo mengine lakini uliahirishwa kutokana na matatizo ya kwenye matawi… sasa tena unaahirishwa lakini hapa inaonekana bayana ni vigumu haki kutendeka.” Katika Kata ya Buguruni wilayani Ilala, baadhi ya wanaCCM ambao tangu juzi walikesha kwenye ofisi cha chama hicho kulinda kura za wagombea udiwani, wanadaiwa kumshambulia Mjumbe wa Kamati ya Siasa, Tawi la Madenge, Ramadhani Mfinanga. Tangu juzi saa tano usiku, wanaCCM hao wanaofikia 40 waliweka kambi katika ofisi hizo wakipinga matokeo ya kura za maoni zilizopigwa katika Tawi la Kisiwani. Mfinanga alifika jana katika ofisi hizo na kusema matokeo hayatabadilishwa kauli iliyowakera na kuanza kumshambulia hadi alipojinasua baada ya kujichanganya na wafanyabiashara walioko katika Soko la Buguruni. Mmoja wa wagombea wa udiwani katika Kata ya Buguruni, Barua Mwakatanga alisema walibaini kwamba kura zilizopigwa katika Tawi la Kisiwani zilikuwa 411 wakati idadi ya wapigakura ilikuwa 337. Alisema walimweleza Katibu wa CCM, Kata ya Buguruni ambaye ndiye msimamizi wa uchaguzi, Abdul Kinogozi aliyewata wapeleke masanduku kwenye Ofisi za Kata ya Buguruni kwa ajili ya uhakiki. “Tulipeleka lakini ilipofika saa tano usiku alisema amechoka na uhakiki utafanyika kuanzia saa mbili asubuhi leo (jana),” alisema. WanaCCM hao waliamua kukesha ili kulinda kura hizo zisibadilishwe wakidai kuna njama za ‘kumbeba’ mgombea mmoja. Kinogozi alisema matokeo hayajatangazwa kwa sababu ya malalamiko ya mmoja wa wagombea na kwamba yatatangazwa baada ya uhakiki utakaofanywa na wagombea wote. Wanaowania nafasi za udiwani ni Musolo Pazi, Magina Lufungulo, Barua Mwakilanga, Abdallah Jaza na Mushokeli Mandali. Imeandikwa na Nuzulack Dausen, Julius Mathias na Raymond Kaminyoge

Mawaziri watano waanguka kura za maoni

Kwa ufupi Ni Chikawe, Makalla, Silima, Ole Telele na Mahadhi Pia yumo Katibu wa NEC CCM Muhamed Seif Khatib Profesa Muhongo, Muradi, Mwakalebela, Nape wapita By Waandishi Wetu, Mwananchi Dar/mikoani. Kishindo cha kura za maoni ndani ya CCM kimeendelea kuwakumba baadhi ya vigogo wa chama hicho baada ya jana mawaziri wengine watano kuanguka. Miongoni mwao ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe aliyekuwa akiwania kupitishwa tena kugombea tena ubunge wa Nachingwea. Chikawe ambaye pia alishindwa katika kinyang’anyiro cha urais kupitia chama hicho, alidondoshwa na Hassan Masala aliyepata kura 6,494 akifuatiwa naye akipata 5,128. Wagombea wengine ni Steven Nyoni (1,438), Amandus Chinguile (1,274), Fadhili Liwaka (1,171), Benito Ng’itu (797), Greyson Francis (671), Albert Mnali (763), Issa Mkalinga (466), Mustafa Malibiche (427) na Ali Namnjundu (319). Mbali ya Chikawe pia manaibu waziri wanne wameangushwa katika kura hizo. Hao ni Mahadhi Juma Maalim (Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa), Perera Ame Silima (Mambo ya Ndani), Amos Makala (Maji) na Saning’o ole Telele (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi). Mahadhi alianguka katika Jimbo la Paje, Zanzibar kwa kupata kura 1,785 huku Jaffar Sanya Jussa ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) Mkoa wa kusini akiibuka mshindi kwa kura 3,368. Silima aliyepata kura 1,218 katika Jimbo la Chumbuni alibwagwa na mpinzani wake, Ussi Pondeza aliyepata kura 1,952. Katika Jimbo la Mvomero, Suleiman Murad alishinda kwa kura 13,165 dhidi ya Makalla ambaye alikuwa anatetea jimbo hilo akipata 10,973. Ole Telele alipata kura 5, 126 huku William ole Nasha akiibuka mshindi kwa kura 23, 563 akifuatiwa na Elias Ngolisa aliyepata 11, 442 na Dk Eliamani Lalkaita 7,135. Matokeo hayo hayakujumlisha kura za matawi matano ambayo Katibu wa CCM Wilaya ya Ngorongoro, Elihudi Shemauya alisema hayawezi kubadili matokeo. Katika Jimbo la Uzini, Katibu wa Oganizesheni wa CCM, Muhammed Seif Khatib ameshindwa baada ya kupata kura 1,333 huku mpinzani wake Salum Mwinyi Rehani akiibuka kidedea kwa kura 1,521. Kigogo mwingine wa CCM, Nape Nnauye ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi, ameshinda kura hizo Jimbo la Mtama kwa kura 9,344 dhidi ya mpinzani wake Selemani Methew aliyepata kura 4,766. Jimbo la Chwaka mbunge wa jimbo hilo kwa miaka 20, Yahya Kassim Issa aliangushwa baada ya kupata kura 1,572 dhidi ya mpinzani wake, Baguwanji Mensuriya Baguwanji aliyepata kura 1,951. Wakati mawaziri hao wakianguka, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya alishinda katika jimbo jipya la Welezo huku Waziri wa Ulinzi, Hussein Mwinyi akishinda katika Jimbo la Kwahani. Aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM, Masauni Hamad Masauni ameshinda Jimbo la Kikwajuni kwa kura 2,222 dhidi ya mpinzani wake, Mussa Shaali Choum aliyepata kura 461. Katika Jimbo la Jang’ombe, Ali Hassan Omar ameibuka mshindi kwa kupata kura 879 dhidi ya mpinzani wake Abdullah Hussein Kombo (639). Aliyekuwa Waziri Kiongozi Zanzibar na waziri wa zamani wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha aliibuka mshindi katika Jimbo la Kijito Upele. Jimbo la Malindi Abdullah Juma Abdulla alishinda kwa kura 558 dhidi ya mpinzani wake, Kombo Mshenga Zubeir aliyepata kura 241. Jimbo hilo nafasi ya uwakilishi, Mohammed Ahmada Salum alishinda kwa kura 336 na dhidi ya Abdulrahman Hassan (271). Majimbo mengine Liwale: Faith Mitambo (7,238), Zainabu Kawawa (3,126). Ruangwa: Naibu Waziri (Tamisemi), Kassim Majaliwa (11,988), Bakari Nampenya (2,678). Kilwa Kaskazini: Murtaza Mangungu alishinda kwa kura 7,140. Kilwa Kusini: Hasanain Dewji ameshinda kwa kura 3,859. Lindi Mjini: Hassani Kunje (3,428) Mohamedi Ulthali (2,314). Jimbo la Mchinga: Said Mtanda ameshinda kwa kura 3,101, Riziki Lulida (2,217). Serengeti: Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Kebwe Steven Kebwe aliibuka mshindi kwa kura 29,268 akiwashinda, Dk James Wanyancha (5,980) na Mabenga Magonera (1,638). Nyamagana: Aliyekuwa Meya wa Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula ameibuka mshindi kwa kura 9,553, Joseph Kahungwa (3,947) na Raphael Shilatu (894) na kufuatiwa na wenzao 17. Ukerewe: Christopher Nyandiga aliongoza kura 8,077, Gerald Robert (142), Laurent Munyu (197), Emmericiana Mkubulo (242), Bandoma Kabulule (414), Bigambo Mtamwega (477), Dk Elias Missana (648), Hezron Tungaraza (693), Dk Deogratias Makalius (727), John Mkungu (775), Osward Mwizalubi (1,098), Maliki Malupu (1,443), Deogratias Lyato (1,824), Sumbuko Chipanda (2,016) na Magesa Boniphace (2,552). Morogoro Mjini: Abdulaziz Abood amepata kura 20,094 na Simon Berege (429). Mikumi: Jonas Nkya alipata kura 947 ameshinda dhidi ya Abdulsalum Sas (544). Kilombero: Mbunge wa jimbo hilo, Abdul Mteketa alianguka baada ya kushika nafasi ya tatu kwa kupata kura 2,646 nyuma ya Abubakar Assenga aliyepata kura 6,629 na Abdul Liana 3,999. Mlimba: Godwin Kunamba ameshinda kwa kura 6,233 Dk Fredrick Sagamiko (2,203), Jane Mihanji (2,073). Gairo: Mbunge wa sasa, Ahmed Shabiby alishinda kwa kura 15,920 akifuatiwa na Omari Awadhi 886. Morogoro Kusini Mashariki: Omary Mgumba alishinda kwa kura 3,393 akifuatiwa na Jamila Taji (2,914) na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Dk Lucy Nkya (1,710). Msoma Vijijini: Profesa Sospeter Muhongo aliibuka mshindi kwa kura 30,431 waliofuatia ni Anthony Mtaka (3,457), Evarest Mganga (2,556), Profesa Edson Mjungu (898), Mafuru Mafuru (421), Wits Onyango (392) na Nelson Semba (186). Butiama: Nimrodi Mkono ameshinda kwa kupata kura 19,366, Chirstopher Siagi (2,457), Samweli Ndengo (745), Jacob Thomas (502), Mwita Wariuba (1,346), Moringe Magige (317), Godfrey Wandiba (303), Joseph Nyamboha (262) na Samweli Gunza (73). Musoma Mjini: Vedastus Mathayo alishinda kwa kura 6,691 akifuatiwa na Paul Kirigini (1,174), Dk Msuto Chirangi (1,082), Juma Mokili (681), Deus Mnasa (378), Nicodemus Nyamajeje (183), Emmanuel Mwita (155), Felix Mboje (131) na Zerulia Mneno (61). Kyela: Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Harrison Mwakyembe ameshinda kwa kupata kura 15,516, George Mwakalinga (4,905) na Martin Kipija (2,301). Njombe Kusini: Edward Mwalongo (3,870), Romanus Mayemba (2,153), Daniel Msemwa (1,976), Arnold Mtewele (1,136), Alfred Luvanda (978), Hassan Mkwawa (152), Vitalis Konga (76) na Mariano Nyigu (86). Makambako: Deo Sanga (7,643) Alimwimike Sahwi (499). Ludewa: Deo Filikunjombe kabla ya kata tatu alikuwa na kura18,290 akiwaacha Kapteni Jacob Mpangala (205) na Zephania Chaula (770). Wanging’ombe; Gerson Lwenge kabla ya kata tatu alikuwa na kura 11,322, Thomas Nyimbo (1,871), Yono Kevela (1,819), John Dugange (466), Richard Magenge (417), Abraham Chaula (382), Kennedy Mpumilwa (332), Hoseana Lunogelo (322), Malumbo Mangula (304), Nobchard Msigwa (216), Abel Badi (106) na Eston Ngilangwa (47). Kiteto: Mjumbe wa NEC, Emmanuel Papian ameshinda kwa kupata kura 40,636 mbunge aliyemaliza muda wake Benedict Ole Nangoro (21,461), Amina Said Mrisho (2,118), Ally Lugendo (287) na Joseph Mwaseba (250). Bunda Mjini: Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira ameshinda kwa kupata kura 6,429 dhidi ya kura 6,206 alizopata mshindani wake wa karibu, Robert Maboto. Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Christopher Sanya alipata kura1,140, Exavery Lugina (846), Simon Odunga (547), Magesa Mugeta (446), Peres Magiri (385) na Brian Bitta (263). Handeni na Bumbuli Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda pamoja na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January Makamba wameshinda katika mchakato wa kura za maoni katika majimbo ya Handeni na Bumbuli. Imeandikwa na Mwanja Ibadi, Christopher Lilai, Nachingwea, Anthony Mayunga, Jovither Kaijage, Juma Mtanda, Lilian Lucas, Salma Said, Florence Focus, Juma Mtanda, Christopher Maregesi, Joseph Lyimo, Burhani Yakub na Shaban Lupimo na Lilian Lucas

Binti wa Sokoine atwaa mikoba ya Lowassa

Kwa ufupi Namelock ambaye ni mbunge wa Viti Maalumu (CCM) alipata kura 29,582 akifuatiliwa na Loota Sanare aliyepata kura 8,809 na nafasi ya tatu, ilichukuliwa na Lolinyu Mkoosu aliyepata kura 235 na Payani Leyani akipata kura 226. By Waandishi Wetu, Mwananchi Arusha. Binti wa Waziri mkuu wa zamani, Edward Sokoine, Namelock Sokoine ameshinda kura za maoni kugombea ubunge Jimbo la Monduli kupitia CCM huku mkwe wa Lowassa, Siyoi Sumari akishindwa Jimbo la Arumeru Mashariki. Namelock ambaye ni mbunge wa Viti Maalumu (CCM) alipata kura 29,582 akifuatiliwa na Loota Sanare aliyepata kura 8,809 na nafasi ya tatu, ilichukuliwa na Lolinyu Mkoosu aliyepata kura 235 na Payani Leyani akipata kura 226. Arumeru Mashariki: Sumari aliyewania jimbo hilo kwa mara ya kwanza baada kifo cha baba yake Jeremia Sumari na kushindwa na Joshua Nassari wa Chadema alipata kura kura 3,664 dhidi ya 12,071 za John Pallangyo. Mshindi wa tatu alikuwa ni William Sarakikya ambaye alipata kura 3,552 na wagombea hao waliwaacha mbali wapinzani wao wengine wanne. Arusha Mjini: Katika Jimbo la Arusha Mjini, mfanyabiashara Philemon Mollel ameshinda kwa kura 5,320, akifuatiliwa na mfanyabiashara mwingine Justine Nyari aliyepata kura 1,894 na nafasi ya tatu, ilichukuliwa na Moses Mwizarubi aliyepata kura 1,205. Karatu: Dk Willibrod Lorry alishinda baada ya kupata kura 17,711, Rajabu Malewa (911), John Dado (745) na Joshua Mwambo (67). Masele ambwaga Mlingwa Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Steven Masele amembwaga waziri mwingine wa zamani, Dk Charles Mlingwa baada ya kupata 70,900 dhidi ya 669 za mpinzani wake. Wagombea wengine Abdallah Seni alipata kura 391, Erasto Kwilasa (232), Hassan Athuman (164), Mussa Ngangala (116), Hatibu Malimi (69), Wille Mzava (65) na Tara Omari (43). Ushetu: Elias Kwandikwa (11,554) Isaya Sino (5,241) na Elfaidi Sikuli (2,007). Kahama Mjini: Jumanne Kishimba (9,754), Kintoki Godwin (433), Nkuba Charles (389), Bundala Maiko (284), Sazia Robert (257), Kapela Robert (135), Ngalawa Adamu (126), Luhende Jerard (106), Malele Charles (91), Tunge John kura (78), Mpangama Deogratias (57), Machunda Eliakimu (56), Masanja Andrew (48) na Kambarage Masusu (28). Msalala: Ezekiel Maige (11,575), Emmanuel Kipole (1,197), John Sukili (962), Nicholas Mabula (668), Maganza Mashala (597), John Lufunga (29) na Wankia Welema (14). Solwa: Mbali ya matokeo ya kata moja ambayo imerudia uchaguzi, Ahamed Salum alikuwa akiongoza kwa kura 17,485 akifuatiwa na Amos Mshandete (2,028), Cyprian Mhoja (1,586), Luhende Richard (1,273), Kasile Paul (637), Gabriel Shija (361), Renatus Chokala (357) na Hosea Somi (255). Kishapu: Kabla ya matokeo ya kata tatu, Suleiman Nchambi alikuwa akiongoza kwa kura 13,443, William Bonda (6,143), Kishiwa Kapale (500), Limbe Moris (393), Heke Bulugu (356) na Timoth Ndanya (193). Mawaziri watamba Kanda ya Ziwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Titus Kamani ameshinda kura za maoni Jimbo la Busega baada ya kupata kura 10,697 dhidi ya mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Dk Rafael Chegeni aliyepata kura 9,661. Buchosa: Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba ameibuka mshindi kwa kupata kura 26,368 dhidi ya Eston Majaliwa aliyepata 9,213. Misungwi: Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga ameibuka mshindi kwa kura 26,171, akimwangusha Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Jacob Shibiliti aliyepata kura 7,009. Shomari Chalamila alipata kura 1,840, Dk Makene Doshi (1,339), Cleophace Jerome (1,051). Ilemela: Mkuu wa Wilaya ya Iringa Angelina Mabula ameibuka mshindi katika Jimbo la Ilemela kwa kupata kura 6,324 mbele ya Barnabas Mathayo (3,562), John Buyamba (1,167) na wagombea wengine 16. Tabora Kaskazini: Almasi Maige (9,466), Shaffin Sumari (6,392) na Joseph Kidawa (5,965). Bariadi: Andrew Chenge (20,200), Masanja Kadogosa (2,986) na Cosmas Manula (270). Meatu: Salum Mbuzi (13,180), Oscar Maduhu (2,988), Romano Thomas (358) na Donard Jinasa (350). Itilima: Njallu Daudi (44,486), Simon Ngagani (2,759) na Danhi Makanga (814).

Monday, January 21, 2013

Gesi kuiangusha CCM

• WABUNGE WAKAMIA MJADALA BUNGENI na Mwandishi wetu NEEMA ya gesi iliyovumbuliwa Mtwara, na wananchi kutaka ibaki mkoani humo badala ya kuisafirisha kwenda jijini Dar es Salaam, imegeuka laana, na sasa inaweza kukiangusha Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2015 baada ya wananchi kuanza kupoteza imani nacho, Tanzania Daima Jumapili limebaini. Mbunge wa Mtwara Mjini, Hasnain Murji (CCM) na Mwenyekiti wa CCM Manispaa ya Mikindani, Ali Chinkawene ndio vinara wa kampeni za kupinga gesi hiyo kusafirishwa kwenda Dar es Salaam, na wamejitokeza hadharani kupinga kauli ya Rais Jakaya Kikwete kwamba wakazi wa Mkoa wa Mtwara hawapaswi kuzuia. Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa wiki nzima sasa, umebaini kuwa wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara ambao wengi ni wafuasi wa CCM, wamepoteza imani na chama hicho. Baadhi ya wabunge wa mikoa ya Mtwara na Lindi ambao wako jijini Dar es Salaam wakihudhuria vikao vya kamati za Bunge, waliliambia Tanzania Daima Jumapili kwamba wana-CCM katika mikoa hiyo, wamepoteza imani na chama hicho kutokana na kauli za viongozi wao wanaotumia vitisho kutaka gesi hiyo isafirishwe kwenda Dar es Salaam. Mbunge wa Mtwara Mjini, Murji, alisema juzi kuwa msimamo wake wa kupingana na Rais Kikwete uko pale pale na kusisitiza kuwa yuko tayari kutimuliwa ubunge kuliko kuachia mradi huo wa gesi upelekwe Dar es Salaam. Rais Kikwete katika salamu zake za mwaka mpya wa 2013, alisema Mtwara hawana haki kuzuia gesi hiyo kwani rasilimali inayopatikana popote katika nchi hii ni mali ya taifa, na hutumika kwa manufaa ya taifa na si mali ya watu wa pale ilipogundulika au pale shughuli inapofanyika. Akionesha dhahiri kupingana na Rais Kikwete, Murji alisema serikali inapaswa kujenga mitambo ya kuzalisha umeme mkoani Mtwara badala ya Dar es Salaam. Alisema: “Tulipoona hali inakuwa tete, niliitisha kikao cha Kamati ya Siasa kujadili nini msimamo wa chama katika hili. Kamati ya Siasa wakasema hawawezi kukisemea chama kwa sababu chama ni wanachama, hivyo nikaitisha kikao cha Halmashauri Kuu ambapo pia tuliwaalika mabalozi wa mitaa. “Katika kikao hicho, wajumbe walipinga kwa nguvu zote suala la gesi kupelekwa Dar es Salaam. Wakaniambia niseme msimamo wao kuwa hawataki gesi iende Dar es Salaam hadi pale masilahi ya wana-Mtwara yatakapowekwa wazi na serikali na huo ndio msimamo.” Alisema msimamo huo si wake binafsi, bali ni maazimio ya vikao halali vya chama hicho vinavyowakilisha wanachama, na kwamba historia ya mikoa ya kusini jinsi ilivyonyimwa maendeleo, ilitumiwa na wajumbe kujenga hoja hiyo. “Wakati sisi hatuna umeme, hakuna aliyefikiria kutuunganisha kwenye gridi ya taifa… Barabara ya kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam miaka 51 ya uhuru sasa haijakamilika. Lakini bomba wanataka kujenga kwa miezi 18. Hivi kuna Watanzania muhimu zaidi ya wengine?” alihoji mbunge huyo. Duru za siasa zilidokeza kuwa, kauli za viongozi hao ndio msimamo wa wana CCM ambao baadhi wameapa kwamba kama serikali haitabadilisha msimamo wake, chama hicho kisahau kushinda uchaguzi wowote katika mikoa hiyo. Wabunge wengine ambao waliomba majina yao yahifadhiwe, walisema wanasubiri kwa hamu mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza hivi karibuni mjini Dodoma, kwani wamepanga kuzungumzia msimamo wao kuhusu suala hilo. “Sisi wengine mtatusikia Dodoma. Tumeamua kutetea maslahi yetu na kizazi chetu kijacho kwani kusini hatukuwa na cha kuwaachia, lakini leo tuna gesi. Haitoki Mtwara,” alisema mbunge huyo. Wakati wabunge hao wakiweka msimamo huo, jana na juzi, wananchi wa wilaya zote za Mkoa wa Mtwara walifanya maandamano kwa lengo la kuendeleza kilio chao cha kupinga gesi yao kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam. Akizungumzia suala hilo, Mbunge wa Kigamboni, Dar es Salaam, Faustine Ndungulile, alisema kuwa lilionekana dogo, lakini kadiri muda unavyokwenda, badala ya kuwa kipele linaekelea kuwa jipu na mwisho linaweza kusababisha kansa itakayosambaa mwili mzima. Alisema: “Nimefuatilia kwa makini kuhusu hoja ya wananchi wa Mtwara, lakini vile vile nimefuatilia kwa makini majibu yanayotolewa na viongozi mbalimbali. Kinachoonekana ni kwamba, viongozi hawajipanga vizuri. Kila mtu anasema lake na kila mtu anafanya lake. “Kwa mtazamo wangu, katika sakata hili kuna mambo mawili makubwa ya msingi. Mosi, maendeleo duni katika mikoa ya kusini ikiwa ni pamoja na Mtwara. Pili, tatizo la ajira kwa vijana,” alisema Ndungulile. Mbunge huyo alishauri elimu itolewe kuwashibisha wananchi wa Mtwara jinsi gani watanufaika kimaendeleo na kwa upande wa ajira kwa vijana. “Kubeza na kutumia hoja za nguvu havitasaidia, badala yake tunahitaji nguvu za hoja zitakazowaelimisha na kuwashawishi wananchi wa Mtwara katika maeneo yafuatayo: “Ni vigezo gani vilitumika kufikia uamuzi wa kujenga bomba la gesi toka Mtwara hadi Dar es Salaam? Kwanini mtambo wa kuzalisha umeme usijengwe Mtwara na kusambazwa kuja Dar es Salaam? Je, mchanganuo wa gharama ukoje? “Je, upatikanaji wa gesi hii utakuwa na manufaa gani kwa wananchi wa eneo husika? Je, kutakuwa na viwanda vya kusindika gesi vitakavyojengwa huko Mtwara? Je, mikoa inayozalisha itapata asilimia ya mapato ya gesi inayozalishwa katika eneo hilo? “Je, ajira ngapi zitakazozalishwa na sekta hii, na asilimia ngapi ya ajira zitakuwa kwa ajili ya wakazi wa eneo hili?” Mbunge huyo alisema suala hili linapaswa kushughulikiwa mapema na kwa haraka wakati likiwa bado ni kipele kwani likishakuwa jipu au kansa, gharama za kulishughulikia zitakuwa kubwa. Alisema wananchi kuhoji si dhambi wala uhaini kwani uelewa wao umekua na wanahitaji kushirikishwa na kupewa majibu ya kina.

Dk. Slaa alipua bomu

• ADAI SERIKALI IMEAGIZA MTAMBO WA KUHUJUMU MAWASILIANO YA WAPINZANI na Abdallah Khamis KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema kuwa amebaini kuwapo mpango wa serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuingiza mtambo wa kuingilia mawasiliano ya wapinzani kwa ajili ya kuhujumu uchaguzi mkuu mwaka 2015. Dk. Slaa ambaye ni mara yake ya pili kutoa tuhuma za CCM kuingiza mtambo wa kuingilia mawasiliano ya CHADEMA, alisema tayari ameshapata e-mail yenye kuonyesha thamani ya mtambo huo na kwamba utagharimu dola 850,000 za Marekani, karibu sawa na sh bil. 1.3. Dk. Slaa alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua kongamano la vijana wa vyuo vikuu wa CHADEMA (Chaso), jijini Dar es Salaam, lililokuwa na lengo la kujitathmini na kupanga mikakati ya kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2015 pamoja na kuwaapisha viongozi wapya wa shirikisho hilo. Alisema tayari ameshaandika barua kwa mamlaka husika kuwajulisha hilo, lakini hadi sasa hawajajibu. “Tuna ‘details’ na nyaraka nyingi zinazoonesha namna mtambo utakavyotumika kwa ajili ya kuwahujumu wapinzani na kwa kuwa tumeshaandika barua kwa mamlaka husika na hawajatujibu, kwa sasa sitaenda kwa undani zaidi juu ya hili. Subirini siku ifike nitaweka kila kitu hadharani,” alisema Dk. Slaa. Alisema CCM kwa kushirikiana na Idara ya Usalama wa Taifa, wamekuwa wakitengeneza propaganda mbalimbali za kutaka kumchafua yeye pamoja na CHADEMA, lengo likiwa kuwaondoa Watanzania katika ajenda za msingi za kupigania ukombozi. Aliongeza kuwa, awali mahasimu wake kisiasa walikuja na propaganda kuwa amechukua mke wa mtu, kisha wakasema amedhulumu viwanja huko Mabwepande na sasa wameanzisha suala la kukopa sh milioni 140 ambalo alifafanua kwamba halina ukweli wowote. “Wanawalisha maneno wale wanaokubali kununulika, msifikiri yale yanatoka midomoni mwao hapana, lakini watambue leo hakuna Mtanzania atakayehangaika na uongo unaotengenezwa kwa ajili ya kuwafanya wazidi kutawaliwa,” alisema Dk. Slaa. Akizungumzia tuhuma za CCM na serikali kushirikiana kuingiza mtambo wa kuhujumu mawasiliano ya wapinzani, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye alisema madai hayo ni ya uongo. Akizungumzia vita dhidi ya ufisadi nchini Dk Slaa, alisema wanaojidanganya kwa kusema kwamba kwa sasa siyo agenda ya Watanzania, wamefilisika kimawazo kwa kuwa suala hilo halitanyamaziwa na CHADEMA mpaka wahusika watakapotiwa mbaroni. “Kama wanataka tunyamaze kuhusu ufisadi basi waturudishie twiga waliowatorosha, fedha za EPA, mabilioni ya Uswisi na pia watuambie ni kina nani wanawaua tembo walio katika hifadhi zetu na kisha kusafirisha pembe kupitia bandari zinazolindwa na watu wanaolipwa kwa kodi za Watanzania… vinginevyo hakuna wa kutunyamazisha zaidi ya Mwenyezi Mungu,” alisema Dk. Slaa. Akielezea sera ya majimbo na mafanikio ya mikutano ya chama hicho kwa mwaka 2012, Dk. Slaa, alisema imekuwa na mafanikio makubwa hasa baada ya wananchi kuzinduka na kuamua kudai haki za kutaka kunufaishwa na rasilimali zinazowazunguka. Alisema miaka minane iliyopita wakati CHADEMA waliposema rasilimali za nchi zianze kunufaisha eneo husika kwanza, watu wengi hawakuelewa, lakini leo baada ya kufikiwa na ufahamu kupitia Operersheni za CHADEMA, maarufu kwa jina la M4C, kila eneo limezinduka na sasa serikali inaanza kuwaona watu hao kuwa maadui kwa kuwa wanadai kuthaminiwa. “Nchi yetu kila eneo kuna rasilimali na hatusemi ziwanufaishe watu wa eneo husika tu, bali tunataka waanze wao na ziada ndiyo iende maeneo mengine, leo mnawaona Mtwara na Lindi wanapigania haki hiyo na maeneo mengine hivyo hivyo, kwa hiyo tuna haki ya kujivunia mafanikio ya kuwaelewesha wananchi juu ya kudai haki zao,” alisema Dk. Slaa. Aliongeza kuwa, mwaka huu watahakikisha suala la mauaji holela ya raia wasio na hatia, halijirudii ikiwa ni pamoja na kuishinikiza serikali iunde tume huru ya kimahakama kufuatilia matukio yote ya mauaji yenye utata yanayohusishwa na harakati za kisiasa mwaka 2012. Akizungumzia suala la kufukuzana ndani ya CHADEMA, Dk Slaa alisema hawataogopa kumfukuza mwanachama yeyote msaliti anayeenda kinyume na katiba ya chama hicho na kutolea mfano madiwani waliofukuzwa mkoani Arusha na wanachama wengine. Alisema licha ya madiwani wa Arusha kujua walifukuzwa kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA, waliamua kwenda mahakamani kutaka kukisumbua chama, hali aliyosema mahakama haikuweza kukubaliana nao na sasa wanawajibika kulipa gharama za kesi na wakishindwa wataenda gerezani. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, John Mnyika, aliitaka CCM imshauri Rais Jakaya Kikwete aunde tume huru kuchunguza mauaji mbalimbali ya kisiasa yanayotokea nchini badala ya kupanda jukwaani na kusema CHADEMA ndio wauaji. Alisema kuwa kila siku Nape Nnauye, Mwigulu Nchemba na viongozi wengine ndani ya chama chao wamekuwa wakitaka kuwaaminisha wananchi kuwa CHADEMA inahusika na mauaji ya kisiasa. “Nape anasema CHADEMA wanahusika na mauaji ya kisiasa, Mwigulu naye hivyo hivyo, viongozi wengine ndani ya chama chao nao wanapiga kelele hizo hizo, sisi CHADEMA tunasema iundwe tume huru ya kimahakama wao wanaogopa, wanajua wataumbuka juu ya ufedhuli wao,” alisema Mnyika. Aidha, alisema wamebaini CCM inachapisha kadi za CHADEMA na kisha kuwagawia wanachama wao ili kuwahadaa wananchi kuwa chama hichi kinakimbiwa. “Unajua ukiona mtu anajidanganya mwenyewe, huyo inabidi umsikitikie kwa kuwa kila njia ya udanganyifu wao sasa imeshabainika katika mioyo ya Watanzania, na sasa wameona wajaribu kujiridhisha katika nafsi zao wakiwa katika mikutano ya hadhara kwa kupeana kadi walizochapisha wenyewe huku wakishangiliana,” alisema Mnyika.

Wednesday, November 16, 2011

Wabunge: Chadema wanachochea vurugu

SIKU moja baada ya wabunge wa Chadema, kutoka nje ya Bunge na kutoshiriki mjadala wa Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba wa mwaka 2011, wabunge wa CCM na CUF wamepinga hatua hiyo na kusema wenzao hao wana kusudio la kuchochea vurugu na kuvunja Muungano.

Pia wengi wa wabunge hao waliochangia wamemnyooshea kidole Msemaji wa Kambi ya Upinzani, Tundu Lissu, kuwa amewapotosha Watanzania na ni mwanasheria na mwanaharakati anayepaswa kurudi shule kusoma na pia ni mchochezi wa kutotaka Muungano na Wazanzibari.

Sambamba na hilo, wabunge hao waliochangia Muswada huo juzi na jana, walitetea madaraka aliyonayo Rais wakisema si makubwa na anastahili kuwa nayo kama kiongozi wa nchi.

Tofauti na wabunge hao wa CCM na CUF, Mbunge wa NCCR-Mageuzi wa Kasulu Mjini, Moses Machali, alikuwa pekee aliyewatetea Chadema kwa uamuzi wao wa kususia majadiliano hayo akisema wametekeleza matakwa ya wananchi.

Miongoni mwa waliochangia mjadala huo ni Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohammed (CUF) aliyesema “ni dhambi isiyosameheka kudharau Wazanzibari waliopiga kura ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa halafu unajifanya wewe (Chadema) ni mkombozi wa watu, Lissu anasema Bunge la kikatiba halitakuwa na haki kwa sababu wabunge wa Zanzibar watashiriki !

“Mna ajenda yenu (Chadema) ya siri, mnaleta ubaguzi ndani ya Bunge, sisi (CUF) ndio tuliandamana kudai Katiba na tulipeleka rasimu ya Katiba, Watanzania wenzangu tusishawishike, maoni ya mabadiliko ya Muswada yametokana na wananchi, taasisi na Kamati ya Bunge, tuaminiane na tupendane,” alisema na kupinga wananchi kuandamana nchi nzima kupinga Muswada huo.

Alihoji kauli ya maoni ya Kambi ya Upinzani kuwa Rais ni dikteta wakati Rais huyo ndiye aliyeleta Katiba hiyo na kufafanua kuwa tangu mwaka 1977 hakuwahi kuona Muswada ulioshirikisha wananchi kama huo.

Alisema madaraka ya Rais yameshapunguzwa vya kutosha kama rasimu ya Katiba kupelekwa kwa wananchi kujadiliwa kabla ya kupitishwa, pamoja na hadidu za rejea kutotungwa na Rais isipokuwa zimeshawekwa kwenye Muswada kitendo ambacho Rais amekikubali.

Kwa upande wa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu, alilalamikia wanasheria na wanaharakati bungeni kwamba ndio wanapotosha ukweli kwa makusudi na kuwataka kuacha kupinga madaraka ya Rais kwa kumwangalia kama Mwenyekiti wa CCM, bali kama taasisi yenye madaraka na Katiba ya sasa na kuacha kumwita Rais dikteta.

“Mimi nimekuwa mwanaharakati, najua siasa za uanaharakati, waseme huko nyuma kuna maslahi ya nani...wakasome tena wanasheria hawa, si kuleta uchochezi katika nchi yetu,” alisema. Alisema Rais amefanya uungwana kuwaheshimu na kuleta Muswada huo bungeni kwa ajili ya kuunda Tume hiyo, vinginevyo Katiba iliyopo inamruhusu kuunda Tume bila hata kushirikisha wabunge.

Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka (CCM) pamoja na kutaka mamlaka ya Rais yasiingiliwe, alimtaka Lissu anayejiita mwanasheria na mwanaharakati kurudi darasani kuelimika kutokana na kupotosha historia ya nchi kwamba Mwalimu Julius Nyerere alihusika kumomonyoa Muungano kwa kutofuata haki za binadamu, wakati kipengele hicho kiliingizwa kwenye Katiba wakati wa utawala wake na Zanzibar kushirikishwa.

Mbunge wa Gando, Khalifa Suleiman Khalifa (CUF), alisema Chadema wakipata Dola hawatautaka Muungano wala Wazanzibari. Mbunge wa Viti Maalumu, Angela Kairuki (CCM), alishauri wajumbe wa Tume itakayoundwa walipwe kwa mujibu wa kanuni na malipo ya Serikali na si Waziri wa Katiba apange.

Pia Mwenyekiti wa Tume awasilishe ripoti bungeni na si Waziri wa Katiba na misingi na gharama za Bunge la Katiba ziainishwe kwa uwazi kwenye sheria.

Mbunge wa Tabora, Ismail Aden Rage (CCM) alisema wasiokubaliana na Muswada huo wanatafuta mwanya wa kuleta vurugu na kuongeza: “Wanaotaka kuhoji madaraka ya Rais ni wahuni … nimekerwa na kauli ya wenzetu wa Chadema, taarifa ya Lissu inalenga kuvunja Muungano”.

Hata hivyo, Mbunge Machali tofauti na wenzake, aliwatetea akisema “watakaopitisha Muswada huu laana za Watanzania ziwe juu yenu kwa sababu hamkutaka usomwe mara ya pili”.

Alisema wabunge kujikita katika malumbano kunazidi kujenga chuki na aliwatetea Chadema kutoka ukumbi wa Bunge kutokana na kushindwa kuvumilia na walifanya hivyo kupinga mwenendo mzima wa kuwasilishwa Muswada huo.

Katika hatua nyingine, Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi (CCM), aliomba mwongozo wa Spika wa kitendo cha Chadema kutoka nje na kama vyama vingine vitatoka nje, mjadala wa Bunge utaendeleaje. Spika, Anne Makinda alijibu:

“Tumekubaliana mikutano yote ya vyama ifanyike saa 7 mchana na watakaotoka katikati ya mjadala waombe ruhusa, Katibu wa Chadema hajaniomba wakutane baada ya kipindi cha maswali, nami nilivyowaona nimewachukulia kama wengine wanavyokwenda kunywa chai”.

Mfanyabiashara kigagula!


Mfanyabiashara maarufu wa mjini Iringa, Mama Mbilinyi akiingizwa ndani ya gari la Polisi kabla ya wananchi wenye hasira kali hawajamjeruhi kwa tuhuma za kufuga misukule. (Picha na Frank Leonard).

Tanzania Yafungwa na Chad, Yapita Kwa Goli la Ugenini


Taifa Stars ambayo wiki iliyopita iliizamisha Chad 2-1 kwenye uwanja wake nchini Chad, imeshindwa kuwika nyumbani na kukubali kipigo cha bao 1-0.

Katika mechi iliyochezwa jioni hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar esa Salaam, Taifa Stars ilifanikiwa kusonga mbele kwa faida ya goli la ugenini.

Chad walipata goli lao la ushindi kwenye kipindi cha pili dakika ya 48, mfungaji akiwa ni Mahamat Labbo ambaye ndiye aliyeipatia Chad goli lake la kufutia machozi kwenye mechi ya awali mjini N'Djaména.

Kwa matokeo haya, Taifa Stars imefanikiwa kuingia hatua ya makundi ambapo itashiriki katika kundi C lenye jumla ya timu nne zikiwemo Ivory Coast, Morocco na Gambia.

Fainali za Kombe la Dunia zinatarajiwa kufanyika mwaka 2014 nchini Brazil.

Friday, November 11, 2011

MMEONA VIJUNGU






HAYA YETU MACHO

KAFARA NZITO



Na Luqman Maloto
VIONGOZI wakuu wa Dini ya Shetani, Freemasons, wamefanya kafara nzito kuadhimisha kukamatwa, kuteswa kisha kuuawa kwa aliyekuwa Kiongozi wa Libya, Muammar Gaddafi.

Vyanzo vimesema kuwa ni kawaida kwa Freemasons kufanya sherehe yenye mrengo wa kafara kila mara, mpango wao unapofanikiwa sehemu yoyote ile.

Kwa mujibu wa mitandao kadhaa inayojihusisha na utoaji wa habari za jamii ya Freemasons, kafara ambayo hufanywa ni ile ya mnyama hususan mbuzi mwenye pembe zinazofanana na zile za jini anayeitwa Lucifer (jini mkuu) ambaye huabudiwa na wafuasi wa Dini ya Shetani.

Mnyama huyo huchinjwa kisha damu na kichwa chake huhifadhiwa kwenye chombo chochote chenye muundo wa ndoo ili pembe zitokeze kwa juu na kutengeneza alama maarufu ya Freemasons ambayo wafuasi wake huitumia kwa njia ya vidole kutoa salamu.

Habari zinasema Freemasons walifanya kafara hiyo usiku wa manane kwenye hekalu moja kubwa lililojengwa kwenye eneo la jangwa lililopo ndani ya Jiji la Misrata, Libya.

Inabainishwa kuwa viongozi mbalimbali wakubwa kwenye nchi zilizoendelea kiuchumi ambao wana vyeo vikubwa ndani ya jamii ya Freemasons, walihudhuria kafara hiyo.

MKAKATI HATARI
Habari zinabainisha kuwa Freemasons ipo kwenye mkakati thabiti wa kuitawala dunia kabla ya Desemba 2012.
Kutokana na mkakati huo, imebainishwa kuwa Freemasons wamekuwa wakiratibu sera zao kwa kuangusha utawala wa nchi mbalimbali ambao viongozi wake wameshindwa kuendana na matakwa yake.

Inaelezwa kuwa Gaddafi alikuwa kiongozi mwenye mrengo wa Kiislam japo alikuwa haweki wazi kwenye utawala wake na kwamba alikuwa anapingana vikali na Freemasons.

Kwa mujibu wa mnajimu msomi, Maalim Hassan Yahya Hussein, Jeshi la Kujihami la Umoja wa Nchi za Magharibi (Nato), hutekeleza mipango ya Freemasons kama lilivyofanya Libya kumng’oa Gaddafi.

Maalim Hassan ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mnajimu maarufu barani Afrika, marehemu Sheikh Yahya Hussein, alisema kuwa dhumuni kuu la Freemasons ni kuzipiga vita dini za Kiislam na Kikristo.

“Ipo wazi kuwa wao lengo lao ni kuitawala dunia, kwa hiyo wanahakikisha hilo linawezekana kwa kudhoofisha Uislam na Ukristo ili ufe kisha Shetani ashinde hapa duniani,” alisema Maalim Hassan ambaye ni mrithi wa kazi za unajimu za marehemu Sheikh Yahya.

Aliongeza: “Mkakati mkubwa zaidi ni kuhakikisha dunia inaabudu Dini ya Shetani, wanataka kila mtu awe chini ya mamlaka ya jini mkuu (Lucifer). Dunia nzima itawaliwe na serikali moja na iwe na sarafu moja.”

Kauli ya Maalim Hassan inashabihiana na ile iliyopo kwenye maandiko kwamba zama za Dini ya Shetani kuishika dunia, kutakuwa na mfumo ambao utazuia mtu yeyote kupata huduma za kijamii mpaka awe mwanachama na atatambulika kwa chapa 666.

Habari zaidi zinaeleza kuwa Freemasons wanatumia njia mbalimbali kuhakikisha ulimwengu mzima hakuna anayeamini dini za Mungu na wanapambana kuhakikisha hata Yesu (Nabii Isa) atakaporejea akute hakuna aliye tayari kukombolewa.

Katika kuhakikisha wanapambana na nguvu ya Yesu, Freemasons wamekuwa wakitumia damu ndiyo maana hutoa kafara kwa kuchinja mnyama hasa mbuzi au kondoo wenye pembe kwa imani kwamba huwaongezea nguvu ya kuishika dunia.

Kutokana na tishio la Freemasons, viongozi wa kidini hususan wale wa Mashariki ya Kati, wamekuwa wakiwataka Waislam na Wakristo kwa imani zao, kufunga na kusali ili Dini ya Shetani isipate mafanikio inayoyataka.

SAKATA LA USHOGA
Habari zinasema kuwa Serikali ya Uingereza imekuwa ya kwanza kutumiwa na Freemasons katika kuhakikisha nchi zote zinazounda Jumuiya ya Madola zinapitisha sheria zinazokinzana na maandiko matakatifu yanayoaminiwa na waumini wa Dini za Kiislam na Kikristo.

Ushoga na usagaji ni vitendo ambavyo vinakemewa na dini hizo lakini hivi sasa, Freemasons wanadaiwa kuchochea mabadiliko ili watu wanaojihusisha na hulka hizo wawe huru kikatiba duniani.

Hivi karibuni, Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, alitangaza kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Madola ili apate misaada inabidi kwanza aruhusu ndoa za jinsi moja (ushoga na usagaji) kwenye katiba ya nchi yake.

Tanzania ikiwa moja ya wanachama wa Jumuiya ya Madola, inapitiwa kwenye rungu hili, ingawa Balozi wa Uingereza nchini, Diana Corner alisema nchi yetu haihusiki.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alishatoa tamko kwamba Tanzania haipo tayari kuruhusu ndoa za mashoga na wasagaji kisha akaonya kuwa kauli ya Cameron inaweza kuivunja Jumuiya ya Madola.

SIYO FREEMASONS PEKE YAKE
Mbali na Freemasons, dini nyingine zenye mrengo wa Shetani ni Illuminati na Skull & Bones ambazo zinavuma zaidi Marekani.

VIGOGO WA FREEMASONS
Viongozi wanaotajwa kuwa vigogo wa jamii hiyo ni marais wa 43 na 44 wa Marekani, Barack Obama na George Bush, Rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy ambao wanaonesha alama za vidole ukurasa wa kwanza. Yupo pia Cameron na wengine wengi.

Malema 'avuliwa gamba' ANC

Friday, 11 November 2011



Mashirika ya habari, JOBURG, Afrika Kusini
KIONGOZI wa Umoja Vijana wa chama cha ANC kinachotawala nchini Afrika Kusini, Julius Malema (30) amesimamishwa wadhifa huo kwa miaka mitano .
Hatua hiyo imefikiwa jana, baada ya kamati ya nidhamu ya chama hicho kutoa hukumu dhidi ya kiongozi huyo mwenye ushawishi mkubwa kwa vijana wa chama hicho.

Malema ambaye siku za nyuma alikuwa mshirika mkubwa wa kisiasa wa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma lakini baadaye akamuasi, amekuwa katika malumbano makali na uongozi wa chama hicho na rais wake (Zuma).

Hata hivyo, katika kile kinachoonekana ni hatua mahususi ya kuzima uasi unaoweza kufanywa na Malema ndani ya ANC kutokana na nguvu na ushawishi aliyonayo kwa vijana, kiongozi huyo amesimamishwa na kuonywa kuwa iwapo ataonyesha kwenda kinyume na adhabu hiyo anaweza kufukuzwa katika chama hicho.

Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya ANC, Derek Hanekom alisema tabia ya Malema imekishushia hadhi chama hicho na kwamba tabia yake siyo njia sahihi ya kuelezea hisia za kutoridhika na sera za chama.

Katika tuhuma hizo, Malema alishtakiwa pamoja na maofisa wengine watano, akishutumiwa kuchochea mgawanyiko na kuvunjia heshima ya chama hicho.

Habari zaidi zilizopatikana jana zilidai kuwa, huenda Malema akaondolewa katika chama cha ANC.
Hata hivyo, inasemekana kuwa iwapo Malema atatimuliwa huenda ushawishi wake kuhusu atakayekuwa kiongozi wa nchi hiyo mwakani ukadidimizwa.
Malema ambaye hakuwepo kwenye makao makuu ya chama chake wakati hukumu hiyo ilipotolewa, amepewa siku 14 kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Kamati hiyo ya ANC imempata Malema na hatia ya kuvuruga mkutano wa ANC, kukivunjia hadhi chama hicho kwa kudai mageuzi ya utawala nchini Botswana na kuchochea migawanyiko ndani ya chama hicho.

Viongozi wengine wa Umoja wa Vijana wa ANC, akiwemo msemaji wake Floyd Shivambu, wamesimamishwa katika nyadhifa zao kwa muda wa miaka mitatu.

Hata hivyo, kamati hiyo haikumpata Malema na hatia kwenye kosa la kuchochea ubaguzi wa rangi.

Stars leo mashambulizi mwanzo mwisho Inakamuana na Chad


*Inakamuana na Chad
Na Edo Kumwembe, N’djamena, Chad

TAIFA Stars leo itacheza staili ya kushambulia mwanzo-mwisho dhidi ya wenyeji wao timu ya taifa ya Chad katika pambano muhimu la awali kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia. Mechi inapigwa kwenye Uwanja wa Idriss Mahamat Ouya jijini N’Djamena.

Kocha wa Stars, Jan Poulsen amekumbushia falsafa yake ya kucheza kwa kushambulia, ambapo atawatumia viungo wawili na kujaza washambuliaji mbele Abdi Kassim, Nizar Khalfan, Mrisho Ngassa na Mbwana Samata.

Stars iliyoingia jijini N’dJamena saa saba usiku juzi kwa ndege ya shirika la ndege la Kenya itaingia uwanjani ugenini kusaka matokeo bora katika pambano hilo la awali kabla ya kurudiana na wenyeji wao katika uwanja wa taifa Jumanne jioni.

Kabla ya pambano la leo, jana Stars walifanya mazoezi yao jioni katika uwanja wa Idriss Mahamat Ouya huku wakimkosa mlinzi wa kulia wa timu hiyo, Erasto Nyoni ambaye alianza kusumbuliwa na malaria tangu alipotua jijini N’Djamena.

Kwa mujibu wa Poulsen, kiungo chipukizi, Shomari Kapombe anatazamiwa kuziba nafasi ya Nyoni huku winga mahiri Mrisho Ngassa akitazamiwa kuanza pambano hilo baada ya kukosekana katika vikosi vya kwanza vya kocha Poulsen katika mechi za karibuni.
Kurudi kikosini kwa Ngassa kunatokana na kujitoa kwa mshambuliaji Danny Mrwanda ambaye amekuwa akianza katika mechi za karibuni kama mshambuliaji anayesaidia mashambulizi kuanzia upande wa kushoto.
Poulsen ameimbia Mwananchi, haifahamu timu ya Chad lakini akaahidi kubadili fomesheni ya Stars dakika kadhaa baada ya kuanza kwa pambano hilo kutokana na jinsi atakavyowasoma wapinzani wake.
“Siijui vizuri Chad. Nitawaangalia katika dakika 20 za mwanzo na kama kuna uwezekano wa kubadili fomesheni basi nitafanya hivyo. Lakini kama ilivyo kawaida yangu, asilimia 95 ya mchezo wa timu yangu unategemea zaidi na jinsi tunavyocheza wenyewe kuliko ambavyo mpinzani wetu anacheza.” alisema Poulsen.
Hata hivyo, Poulsen alisema atafurahi zaidi kucheza soka la kushambulia kwa ajili ya kupata matokeo mazuri badala ya kucheza soka la kujihami ambalo haliisaidii timu.
Naye kocha wa Chad ambaye kikosi chake kilifanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa Idriss Mahamat Ouya, Mohamed Omary alisema dakika tisini ndio zitaaamua mshindi wa leo na si vinginevyo.
“Sichezi mpira nje ya uwanja. Nacheza ndani ya uwanja. Dakika tisini ndio zitaamua matokeo ya mechi ya kesho (leo).” Alisema Omary
Endapo Stars itapata matokeo mazuri katika mechi zake mbili dhidi ya Chad ambazo zinachezwa ndani ya siku nne, itapata nafasi ya kucheza kundi la kufuzu kwenda kombe la dunia ikipangwa pamoja na Gambia, Ivory Coast na Morocco
Mwamuzi wa pambano la leo ni Ogunkolade Bunmi wa Nigeria akisaidiwa na Abidoye Tunde na Baba Abel ambao wote pia ni Wanigeria.
Kwa mujibu wa Poulsen kikosi kamili cha Stars leo ni Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Juma Nyoso, Idrisa Rajab, Shaabani Nditi, Henry Joseph,
Abdi Kassim, Nizar Khalfan, Mrisho Ngassa na Mbwana Samata

Mamlaka ya rais yagawa Kamati ya Katiba


KAMATI ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala imeshindwa kufikia mwafaka kuhusu muswada wa Sheria ya Mapitio na Marekebisho ya Katiba wa mwaka 2011 unaotarajiwa kuwasilishwa bungeni Jumatatu ijayo.

Habari kutoka ndani ya kikao cha kamati hiyo, jana zinasema wajumbe hao bado wamegawanyika kuhusu suala la sheria inayokusudiwa kutungwa kumpa Rais mamlaka makubwa katika mchakato huo wa kupatikana kwa katiba mpya.

Habari hizo zinaeleza kwamba wanabishania wanachodai kuwa ni muswada huo kumpa Rais madaraka makubwa ambayo ni pamoja na kuteua wajumbe wa tume ya Kukusanya Maoni, sekretarieti ya Tume hiyo na wabunge 116 kuingia katika Bunge la Katiba.

“Kwa hali hii Katiba inaweza kuwa ni mali ya Rais, maana hata wajumbe wa sekretarieti anatakiwa kuteua yeye! Hii ni 'too much' (imezidi). Kwa maana hiyo, mchakato mzima unashikwa na Rais mwenyewe,” alisema mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo.

Taarifa zaidi zinasema kutokana na mvutano huo, suala hilo sasa limechukua mtizamo wa itikadi za vyama, na kwamba wajumbe ambao ni wabunge wa CCM katika kamati hiyo wameanza kulegeza msimamo na kukubaliana na mapendekezo ya Serikali, huku wabunge wa upinzani wakitaka kufanywa kwa marekebisho.

Kwa mujibu wa habari hizo, wajumbe hasa wale kutoka upinzani wanataka madaraka ya Rais yapunguzwe kwa kuipa Tume ya Kukusanya Maoni kutoka kwa wananchi ndiyo ipewe mamlaka ya kuteua sekretarieti yake badala ya suala hilo kufanywa pia na Rais.

Juzi, Waziri wa Katiba na Sheria, Celine Kombani aliliambia Mwananchi kuwa tatizo la wanaodai kuwa Rais ana madaraka makubwa hawatoi mapendekezo mbadala na jinsi ya kurekebisha pendekezo hilo.

“Sasa Rais ndiye aliyepo, kwa nini hawataki kumwamini wakati alipigiwa kura na wananchi wengi? Lakini, basi waseme wao wanatakaje,” alisema Kombani.

Mmoja wa wajumbe alisema: “Mahali tunapofika, ni kama kila mmoja ataondoka na msimamo wake kwenda nao bungeni. Hata leo, mbele ya Waziri (Kombani) tumeshindwa kufikia mwafaka, sasa hiyo siyo dalili njema."

Hali hiyo ya kutoafikiana miongoni mwa wajumbe wa kamati hiyo inatoa ahueni kwa Serikali kuweza kupitisha mapendekezo yake bila kupata upinzani mkubwa kutoka kwa kamati hiyo kama ilivyokuwa awali.

Vikao vya Kamati hiyo vimekuwa vikivuta wabunge wengi hata ambao si wajumbe wake, ili kufuatilia kinachoendelea kwenye meza ya majadiliano baina ya wajumbe husika kwa upande mmoja, kamati na Serikali kwa upande mwingine.

Kutokana na unyeti wa suala la katiba, Spika wa Bunge Anne Makinda aliongeza wajumbe watano katika Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala ili kupanua wigo wa mjadala wa suala hilo.

Makinda aliliambia Mwananchi mwanzoni mwa wiki hii kuwa wabunge hao watano wanaruhusiwa kupiga kura kwenye uamuzi. “Kikanuni hawa niliowateua mimi wanaruhusiwa kupiga kura na nimefanya hivyo kutokana na unyeti wa suala lenyewe,” alisema Makinda.

Wajumbe hao ni Mwanasheria Mkuu wa zamani na Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge, Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR Mageuzi), David Kafulila, Mbunge wa Simanjiro (CCM) Christopher Ole Sendeka, Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed pamoja na Deogratius Ntukamazina ambaye ni Mbunge wa Ngara (CCM).

Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Marekebisho ya Katiba wa mwaka 2011, sasa utasomwa bungeni kwa mara ya pili na umetengewa siku tatu kwa ajili ya kujadiliwa kabla ya kupitishwa na Bunge.

Muswada huo ulisomwa kwa mara ya kwanza Bungeni Aprili 5, mwaka huu, lakini, ukarejeshwa Serikalini ili kufanyiwa marekebisho kadhaa na kuandikwa kwa Kiswahili kabla ya kurejeshwa tena Bungeni.

Kutokana na hali hiyo Serikali ilipata upinzani mkali kutoka kwa wabunge na wanaharakati ambao walidai kwamba muswada huo ulipaswa usomwe kwa mara ya kwanza kutokana na kufanyiwa marekebisho makubwa tofauti na ule wa awali.

Hata hivyo Kombani alisema juzi kuwa: “Muswada huu uliposomwa kwa mara ya kwanza haukuondolewa, bali ulipelekwa kwa umma ili ukajadiliwe”.

“Mabadiliko mengi yanayolalamikiwa yalitokana na hoja za wananchi, hii ni ishara kwamba tulizingatia hizo hoja, sasa kwa mujibu wa taratibu za miswada ni kwamba utasomwa kwa mara ya pili, kama mnavyoona kwenye ratiba,” alisema Kombani.

Mkurugenzi wa Huduma za Bunge, John Joel aliliambia Mwananchi kuwa kwa mujibu wa taratibu, muswada huo hauwezi kutangazwa tena katika Gazeti la Serikali wakati ulishatangazwa Machi mwaka huu.

Ratiba ya Mkutano wa Tano wa Bunge inaonyesha kuwa Muswada huo utasomwa kwa mara ya pili Jumatatu, Novemba 14 mwaka huu na kuendelea kujadiliwa na Jumanne, Novemba 15 na Jumatano Novemba 16 mwaka huu.

Hatua ya muswada huo kupangwa kusomwa kwa mara ya pili, inatafsiriwa kuwa ni “ushindi” kwa Serikali dhidi ya waliokuwa wakipinga hatua hiyo kutokana na sababu mbalimbali, kubwa ikiwa ni wananchi kupewa muda zaidi kwa ajili ya kuujadili.

Mjadala wa muswada huo utatanguliwa na semina kwa wabunge wote itakayofanyika kesho Jumamosi hatua inayotafsiriwa kuwa ni kujaribu kupunguza hoja ambazo zinaweza kujitokeza na pengine kuukwamisha.

Baadhi ya wanaharakati wanaopinga muswada huo kusomwa kwa mara ya pili ni Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Jukwaa la Katiba ambao wameenda mbali na kudai kuwa Waziri Kombani, amechakachua muswada huo.

Mbowe apandishwa kizimbani


PINDA ASEMA MAANDAMANO CHADEMA YANATUNYIMA USINGIZI
MWENYEKITI wa Taifa Chadema, Freeman Mbowe, amepandishwa kizimbani katika Mahakamani ya Hakimu Mkazi Arusha na kusomewa mashtaka mawili ya kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria na kukataa kutii amri halali ya polisi iliyowataka kutawanyika.

Kutokana na mashitaka hayo, Mbowe ameunganishwa na washtakiwa wengine 27 wanachama wa chama hicho, waliofikishwa mahakamani hapo Jumanne iliyopita wakikabiliwa na mashtaka kama hayo, akiwemo Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu .

Mbowe ambaye pia Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzania Bungeni, ameunganishwa kwenye kesi hiyo ya jinai namba 454/2011 ambapo watuhumiwa wote kwa kwa pamoja, wanadaiwa kufanya kusanyiko isivyo halali katika viwanja vya NMC, eneo la Unga Ltd, Manispaa ya Arusha Novemba 7 mwaka huu.

Hata hivyo Mbowe ambaye anakuwa mshitakiwa wa 28 kwenye kesi hiyo, alikana mashitaka yote mawili yaliyosomwa mahakamani hapo na Wakili wa Serikali Haruna Matagane akisaidiwa na mwenzake, Agustino Kombe.

Upande wa utetezi ukiongozwa na mawakili Method Kimomogoro na Issa Rajabu, uliiomba mahakama hiyo kumpa dhamana mteja wao kwa masharti sawa na wenzake.


Hakimu Devotha Kamuzora anayesikiliza kesi hiyo, alikubaliana na maombi hayo na kumpa dhamana Mbowe, kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili wenye vitambulisho na barua ya utambulisho kutoka kwa Ofisa Mtendaji wa Kata ambao walitia saini hati ya dhamana ya Sh milioni tano kila mmoja.

Mwenyekiti huyo aliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti . Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 22, mwaka huu itakapotajwa.


Maelezo ya wakili

Katika maelezo ya hati ya mashitaka, Wakili Matagane alidai washitakiwa wote kwa pamoja walikusanyika isivyo halali kwenye viwanja vya NMC usiku wa Novemba 7 hadi Novemba 8 mwaka huu saa 12.00 asubuhi kwa lengo la kutenda kosa wakati shtaka la pili, ni kukataa kutii amri halalii ya polisi iliyotolewa na Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Peter Mvulla, kuwataka watawanyike.

Mbowe aliyejisalimisha mwenyewe polisi saa 5:45 juzi baada ya kutakiwa kufanya hivyo na Kaimu Kamanda wa Polisi, Akili Mpwapwa, alifikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi akiwa ndani ya gari namba PT 1844 aina ya Toyota Land Cruiser, lililosindikizwa na gari jingine lililojaa askari waliovalia sare za jeshi hilo huku wakiwa wakiwa wamebeba silaha.


Mwenyekiti huyo aliyefika eneo la viwanja vya Mahakama Saa 3:45 asubuhi, aliongozwa moja kwa moja kwenye chumba maalumu cha kusubiria kabla ya kufikishwa mbele ya hakimu kusomewa mashtaka yake saa 4:00 huku umati mkubwa wa wafuasi wa Chadema ukiwa umefurika ndani na nje ya mahakama hiyo.


Kauli ya Pinda kuhusu Chadema

Wakati hayo yakiendelea Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ametoboa siri kuhusu maandamano ya mara kwa mara yanayofanywa na Chadema kwa kutamka kwamba yanaiumiza kichwa serikali.


Akijibu maswali papo kwa papo bungeni jana, Pinda alisema ; "Staili yenu hiyo (Chadema) ya maandamano, inatupa shida sana, tunapata taabu kila wakati kufikiria maandamano badala ya mambo ya msingi.”

Waziri mkuu alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, aliyetaka kujua, pamoja na mambo mengine dhamira na msimamo wa serikali ya kutatua mgogoro wa umeya wa Arusha.

Mnyika alisema tatizo kubwa la mgogoro wa Arusha ni uchaguzi wa meya ambao Chadema imeonyesha dhamira ya dhati kutafuta suluhu hivyo, akataka msimamo Pinda kwa maelezo kuwa mgogoro huo umesambaa nchi nzima na kama haiwezekani kupatikana suluhu Chadema watajua cha kuwaeleza wanachama wao.

Katika jibu lake Pinda aliitaka Chadema kutokuza jambo hilo kwa namna Inavyolichukulia ,“Tusikuze sana mambo kwamba mgogoro huo sasa umesambaa, wapi Mnyika? Wapi? Kwa staili yenu (Chadema) ya maandamano kila mahali, sisi serikalini tuna mengi ya kufanya, hatuwezi kila siku tuwe tunashughulikia matatizo yenu tu. 'People's Power' kila kukicha, haileti suluhu ya matatizo yenu, mnahitaji kubadilika,” alisema Pinda

Alisema wakati mwingine serikali inaacha kufikiria mambo ya maendeleo kwa wananchi na kujikuta inafikiria maandamano ambayo yamekuwa yakishinikizwa mara kwa mara na Chadema nchi nzima.

Pinda alisema staili hiyo ya Chadema kufanya maandamano kwa kile inachoiita, kutegemea nguvu ya umma, imekuwa ikimuuza zaidi yeye binafasi, "kwa kweli mimi naumizwa na hili".

Aliongeza kwamba, maandamano hayo wakati mwingine yanaonyesha namna chama hicho kisivyo na dhamira ya kweli katika kupata suluhu ya matatizo mbalimbali ikiwemo ya mgogoro wa umeya wa Jiji la Arusha.

“ Staili yenu ya 'People's Power, People's Power !' kila kukicha, inatunyima usingizi. Tunashindwa kufanya shughuli nyingine kwa sababu ya kuifikiria Chadema,” alisema Pinda.

Alisema katika suala la Arusha, imeonekana ni jambo la kisiasa ambalo alimweleza Msajili wa Vyama awasiliane na pande zote mbili ikiwemo CCM ili kuona namna ya kukaa meza moja na kulimaliza .

Awali, Waziri Mkuu akijibu swali kama hilo kutoka kwa Mbunge wa Korogwe, Stephen Ngonyani, aliitaka Chadema kujitathmini ili kuona kama kweli kinahitaji suluhu katika mgogoro wa Arusha badala ya kuilaumu serikali.

Katika swali lake la msingi, Ngonyani alionesha wasiwasi wake kwamba mgogoro wa umeya wa Arusha hivi sasa unatishia hata biashara ya utalii katika jiji hilo na kutaka Mbunge wa Arusha Lema apewe dhamana kama njia ya kupunguza mvutano.

"Mheshimiwa Waziri Mkuu, siku hizi kila kukicha ni vurugu na migogoro Arusha. Sasa hivi Arusha utalii hakuna na biashara hazifanyiki. Kwa nini serikali inazuia dhamana ya Lema?”

Akijibu swali hilo, mbali na kukiri kwamba migogoro jijini Arusha inaathiri sekta ya biashara na utalii, Waziri Mkuu Pinda, alikanusha fikra kwamba serikali inahusika kwa namna yoyote katika kupalilia vurugu hizo, ikiwamo kuzuia dhamana ya mbunge huyo wa Arusha Mjini.

“Ni kweli Arusha kuna migogoro mingi lakini, bado ni tulivu. Ila kama Watanzania, lazima tuzingatie unalolisema. Sio kweli kwamba serikali inazuia dhamana ya Mheshimiwa Lema. Vurugu zote hizo, mara nyingi zinazaa kesi,” alisema Pinda na kuendelea;

“Tarehe Oktoba 28, 2011 Lema na wenzake kadhaa walikamatwa, wakafikishwa mahakamani na kupewa dhamana hadi Oktoba 31, 2011 walipotakiwa kufika tena mahakamani. Kimsingi mashtaka yale yote, yanastahili dhamana na mahakama ilikubali watuhumiwa wote wadhaminiwe.”

“Kilichotokea kwa Lema kwa sababu ambazo mimi sizijui, alikataa dhamana, akisema anataka kubaki gerezani. Wenzake walidhaminiwa na Lema alipelekwa gerezani kama alivyotaka hadi Novemba 14.”

“Ilipofika Novemba 7 (2011), Chadema walikubaliana na mawakili wao kupeleka maombi maalumu mahakamani ili wakamtoe Lema. lakini hakimu akawaambia kesi tumeiahirisha hadi Novemba 14. Sasa hii ni Mamlaka ya Mahakama sio serikali. Tutegemee tu kwamba siku hiyo yanaweza kutoka maamuzi ya kumtoa Lema garezani.”

Pinda alisema kwa mazingira yalivyo, hayuko tayari kutoa maagizo mapya juu ya mgogoro wa Arusha kwa kuwa haoni nia ya dhati ya Chadema kutaka suluhu.

Maandamano Dar

Jijini Dar es Salaam, maandamano yaliyopangwa kufanywa na Baraza la Vijana la Chama hicho (Bavicha) Mkoa, kupinga kile walichokiita kukamatwa na kunyanyaswa kwa viongozi wao wa kitaifa, yamesitishwa.

Mwenyekiti wa Bavicha, John Heche alitangaza kusitishwa maandamano hayo baada ya kuwasili eneo lililopangwa kufanyika maandamano hayo.

Katika utekelezaji wa kusitisha maandamano hayo, viongozi wengine wa chama hicho waliwasili eneo hilo na nakulazimika kuwaomba wafuasi wa chama hicho kutawanyika kutokana na kwamba mpango huo umesitishwa.


Mnamo saa 3:00 asubuhi, umati mkubwa wa wafuasi wa chama hicho ulitanda eneo la Kimara Kona pamoja na Ubungo, yalipopangwa kuanzia maandamano hayo.

Akizungumzia kusitishwa kwa maandamano hayo, Heche alisema wamefikia uamuzi huo baada viongozi wakuu wa chama hicho kufanya majadiliano na maofisa wa Jeshi la
Polisi kuhusu madai ya kero zao.

“Tumepata maelekezo kutoka kwa Mwenyekiti wetu Mbowe na Katibu Mkuu Dk Slaa ya kwamba tusitishe maandamano kwa sababu kuna majadiliano yanaendelea kati yao na maofisa wa Jeshi la Polisi,” alisema Heche.

Aliongeza kuwa kama hakutakuwa na muafaka katika majadiliano hayo, wataingia tena mtaani na kuandamana mpaka kero zao zitakapopatiwa ufumbuzi.

Hali ya ulinzi

Hata hivyo, Jeshi la Polisi liliimarisha ulinzi katika maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam huku kamatakamata ikiwakumba baadhi ya wafuasi wa chama hicho waliovalia mavazi ya chama hicho.

Saa 5: 10 katika eneo la Ubungo gari la polisi lenye namba PT 1818 ambalo lilikuwa limebeba askari waliokuwa na silaha za moto, walikuwa wakiwatangazia wananchi waliokuwa wamekaa katika makundi kutawanyika .

Watu saba waliokuwa wamevalia mavazi ya chama hicho walikamatwa na kufikishwa katika kituo kidogo cha Polisi Urafiki, huku wengine wakiwa wamekamatwa na kubebwa kwenye magari ya polisi ambayo yalikuwa yakizunguka mitaani .

Baadhi ya viongozi wa chadema, walifika katika kituo cha polisi urafiki ambako wafuasi hao saba waliokuwa wamewekwa rumande kwa muda wa saa mbili.
Viongozi hao walifanikiwa kuwatoa kwa dhamana na walitakiwa kubadilisha mavazi hayo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Suleimani Kova alisema hali ya usalama katika jiji la Dar es Salaam ni shwari na hakuna tukio lolote la uvunjivu amani ambalo limejitokeza.

“Jeshi la Polisi limeimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam na kwamba hakuna tukio lolote la uvunjifu amani ambalo limejitokeza “ alisema Kova.

Kova alisema jeshi hilo limejipanga kuhakikisha linaimarisha ulinzi katika maeneo yote ya jiji.

Sunday, July 24, 2011

Nishati wafanya ufisadi kwa miaka minne

YABAINIKA JAIRO ALIHUSIKA MIAKA MIWILI, KAFULILA AWASHTAKI KWA JK
Neville Meena, Dodoma
IMEBAINIKA uchotaji wa mamilioni ya fedha katika Idara na taasisi za umma zilizoko chini ya Wizara ya Nishati na Madini kugharamia shughuli zinazohusiana na gharama za bajeti ya wizara hiyo, ulianza mwaka 2004.

Kuanzia Julai 2008, kila mwaka Ofisi ya Katibu Mkuu katika wizara hiyo imekuwa ikiandika barua kwa wakuu wa taasisi hizo kutaka fedha ambazo kwa namna moja au nyingine zinahusishwa na shughuli za bajeti ya wizara kusomwa bungeni au kughramia sherehe ambazo hufanyika baada ya kupitishwa kwa bajeti husika.

Fedha hizo kwa mujibu wa nyaraka husika, zimekuwa zikitumika kugharamia tafrija mara baada ya bajeti kupitishwa na bunge, posho za vikao, posho za kujikimu, vyakula, vinywaji na mafuta ya magari.

Hata hivyo mmoja wa watumishi wa idara ambazo zimekuwa vinara wa kudaiwa fedha wakati wa bajeti alilithibitishia Mwananchi Jumalipi kwamba, wakati wa vikao vyote vya Bunge kila taasisi huwagharamia watumishi wake wanaokwenda Dodoma.

"Mara nyingi wakati wa vikao vya bajeti huwa nakuja hapa Dodoma, lakini utaratibu wa kukaa hapa lazima nijaze fomu ofisini na ipitishwe kwa mabosi wangu ndipo napewa fedha za kuishi, wizara hawawezi kukupa hela," alisema mtumishi huyo na kuongeza:

"Sana sana hapa tukiwa na kazi huwa tunakunywa chai na luch (chakula cha mchana) na hii siyo kila siku, ni kama tuna kazi zinazotuunganisha na wenzetu kutoka ofisi nyingine na maofisa wa wizara."

Matumizi mabaya ya fedha hizo za umma yamebainika kipindi ambacho Katibu Mkuu wa sasa wa Wizara hiyo, David Jairo, amesimamishwa na Ikulu kwa kupewa likizo ya malipo, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zilizotolewa bungeni dhidi yake.

Jairo anakabiliwa na tuhuma za kuwaandikia barua wakuu wa idara zote zilizoko chini ya wizara yake, ili watoe fedha kwa ajili ya kusaidia kupitishwa kwa bajeti ya wizara hiyo, fedha ambazo zinatafsiriwa kwamba zilikuwa ni kwa lengo la kutoa rushwa kwa wabunge.

Kafulila ashtaki kwa JK
Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila(NCCR - Mageuzi), jana aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa amemwandikia barua Rais Jakaya Kikwete akitaka uchunguzi utakaofanywa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali katika Wizara ya Nishati na Madini uanzie miaka ya mitano iliyopita.

"Nimemwandikia barua Rais Kikwete, maana inaonekana kuwa huu mchezo wa kuchota fedha za Umma katika wizara hii umeanza tangu 2008," alisema Kafulila ambaye pia aliwahi kuwalipua baadhi ya wabunge wenzake, akiwatuhumu kwamba waliomba rushwa katika
Halmashauri ya Handeni, mkoani Tanga.

Kafulila katika barua yake ambayo pia Mwananchi limeiona, alisema anakubaliana na hatua za awali za kumchunguza Jairo, lakini anapendekeza ufanyike uchunguzi mpana kwani mtindo si kwa mwaka huu pekee bali hata miaka iliyopita katika wizara hiyo na nyingine nchini.

"Napenda kupendekeza kwako kuwa suala hili lifanyiwe uchunguzi mpana kwa kuwa upana wa kashfa hii ni zaidi ya mwaka mmoja wa fedha 2011/2012, ni zaidi ya Katibu Mkuu mmoja, David Jairo na pengine ni zaidi ya wizara moja ya Nishati na Madini, katika hicho kinachoelezwa kuwa ni kusaidia uwasilishaji wa bajeti," inaeleza sehemu ya barua hiyo.

Katika barua yake kwa Rais na kutoa nakala kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Spika wa Bunge, Anne Makinda, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Uttoh na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru), Kafulila anasema ana ushahidi unaothibitisha baadhi ya tuhuma hizo.

Uzoefu wa Jairo
Kwa mujibu wa nyaraka ambazo Mwananchi limeziona, hii ni mara ya pili kwa Jairo akiwa Katibu Mkuu katika wizara hiyo kuandika waraka wa kuomba fedha kutoka kwenye idara husika kwa ajili ya kusaidia mchakato wa maandalizi na uwasilishaji wa bajeti bungeni.

Kwa mujibu wa nyaraka hizo, Mei 12, mwaka jana Jairo akiwa Katibu Mkuu, aliandika waraka kwenda kwa aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Stephen Mabada akitaka lichangie Sh20 milioni ili kusaidia kile alichokiita, ‘Gharama za kukamilisha mpango na bajeti ya wizara 2010/2011 na uwasilishaji wake bungeni."

Barua kama hiyo pia iliandikwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati (Ewura), Haruna Masebu, ambaye taasisi yake iliombwa kuchangia Sh25 milioni, wakati Yona Killagane ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC), taasisi yake ilitakiwa kuchangia Sh20 milioni.

Kwa mujibu wa barua hizo, gharama husika kwa ajili ya kazi hiyo ya kibajeti ilikuwa ni Sh186.6 milioni hivyo kuzitaka idara zote kwa pamoja kuchangia kiasi cha Sh90 milioni, wakati wizara ilibaki na jukumu la kuchangia kiasi cha Sh96.6 milioni.

Hata hivyo jumla ya fedha zilizoombwa kutoka Ewura, Tanesco na TPDC ni Sh65 milioni, ikimaanisha kuwa ipo idara au taasisi nyingine ambayo pia iliombwa kuchangia kiasi kilichobaki cha Sh25 milioni.

"Gharama hizi kubwa zimesababishwa na kupanda kwa gharama za posho kutoka Sh60,000 mpaka Sh200,000, Sh50,000 hadi Sh150,000 na Sh30,000 hadi Sh100,000 kwa wenyeviti na makatibu, wajumbe na sekretarieti sawia," inaeleza sehemu ya waraka huo uliondikwa na Jairo na kuongeza:

"Kwa kuwa bajeti ya wizara ya 2009/2010 ilikadiriwa kwa viwango vya zamani, ni dhahiri wizara haiwezi kubeba gharama hizi peke yake. Hivyo inashauriwa Wizara igharamie 96,626,000 na wadau muhimu wa wizara wagharamie 90,000,000".

Barua hiyo haifafanui kuhusu wenyeviti, makatibu, wajumbe na sekretarieti ambao wanapaswa kulipwa posho hizo.

Miaka iliyopita
Mwananchi limethibtisha kuwa "utaratibu" huo wa kuchota fedha umekuwepo kwa muda mrefu, kwani mwaka 2008 na 2009 Wizara hiyo iliandika barua kwa ajilia kutaka "ichangiwe" ili kughramia shughuli za kibajeti.

Julai 5, 2008 aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Arthur Mwakapugi, aliandika wakara kwa Dk Idris Rashid, aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Lutengano Mwakahesya na Killagane wa TPDC akitaka mchango wa kile alichoeleza kuwa ni
"Kuchangia gharama za hafla fupi baada ya mawasilisho ya bajeti ya wizara bungeni Dodoma".

Katika waraka wake huo, Mwakapugi alitaka kila taasisi kuchangia kiasi cha Sh5 milioni, hivyo kufanya jumla yake kuwa Sh15 milioni kwa lengo la kugharamia tafrija husika.

Juni 19, 2009 Mwakapugi aliandika waraka mwingine kwenda Tanesco, REA na TPDC akitaka michango kwa ajili ya kile alichokieleza katika barua yake kuwa ni "Fedha kwa ajili ya kuwezesha uwasilishaji wa hotuba ya bajeti ya 2009/2010 bungeni Dodoma, kazi ambayo anasema katika barua hizo kwamba, gharama zake ni Sh170,461,500.

"Kama ilivyo desturi, maofisa, taasisi na mashirika yaliyo chini ya wizara hujumuika katika kutoa michango yao hasa katika hoja zote zinazojitokeza katika maeneo husika. Ili kufanikisha zoezi hilo, gharama mbalimbali huhitajika zikijumuisha, posho za vikao, uchapishaji wa vitabu, uchapishaji kwenye magazeti, vyakula na vinywaji posho za safari na mafuta kwa washiriki," inaeleza sehemu ya barua.

Barua hiyo inabainisha kuwa msingi wa kutaka kuchangiwa ni kutokana na hali mbaya kifedha katika wizara hivyo na kuwataka Tanesco kuchangi Sh40 milioni, REA Sh30 milioni na TPDC Sh40 milioni.

Likizo ya Jairo
Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo ambaye ni Mkuu wa Utumishi wa Umma aliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma Alhamisi wiki hii kuwa Jairo ambaye yuko chini yake, analazimika kwenda likizo kuanzia juzi ili kupisha uchunguzi wa awali ambao unalenga kubaini iwapo ametenda kosa la kinidhamu kwa mujibu wa sheria zinazoongoza Utumishi wa Mmma.

Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo ndiye aliyemlipua Jairo Bungeni Julai 18, 2011 wakati akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini akisema amekusanya fedha kiasi cha Sh1 bilioni kutoka idara 21 zilizopo chini ya Wizara yake, fedha zisizo na maelezo.

"Nimeanzisha uchunguzi wa awali kwa lengo la kupata ukweli kuhusu tuhuma hizo. Wakati uchunguzi huo ukiendelea, Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini amepewa likizo ya malipo kupisha uchunguzi wa awali," alisema Luhanjo na kuongeza:

"Hatua zitakazochukuliwa hapo baadaye zitategemea matokeo ya uchunguzi wa awali".

Licha ya mchakato wa hatua dhidi ya mtumishi huyo wa umma ambaye ni mteule wa Rais kupitia katika mchakato mrefu, mwishoni mwa mchakato huo anaweza kushushwa cheo, kupunguzwa mshahara, kufukuzwa kazi, kuachishwa kazi au kurejeshwa kazini kwa kutegemea matokeo ya taratibu zitakazofuatwa.

Luhanjo alisema Jairo analazimika kwenda likizo kwa kuwa tuhuma dhidi yake ni nzito. "Zingekuwa tuhuma nyepesi ningeruhusu aendelee na kazi wakati uchunguzi huo wa awali ukifanyika, lakini tuhuma hizi ni nzito mno. Hivyo lazima aende likizo ili kupisha uchunguzi huo," alisema Luhanjo.

Alisema uchunguzi dhidi ya Jairo kwa kuwa unahusu masuala ya fedha, utafanywa na Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambayo inatakiwa kikamilisha kazi yake katika muda wa siku kumi kisha kuiwasilisha kwake kwa hatua zaidi.

Taarifa ya Luhanjo ambayo ni taarifa rasmi ya Serikali inatofautina na kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwamba suala la kuchukua kwa hatua dhidi ya Jairo linamsubiri Rais Kikwete ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi nchini Afrika ya Kusini.

Seneta wa Marekani aahidi kusaidia wafugaji


Joseph Lyimo,Simanjiro
SENETA wa Jimbo la Oregon, nchini Marekani, Jacks Winter, ameahidi kuboresha miundombinu katika Kijiji cha Lengasti, wilayani Simanjiro,ili kuziwezesha jamii za wafugaji kuondokana na matatizo yanayowakabili.

Seneta Winter alitoa ahadi hiyo juzi alipokuwa akizungumza na wakazi wa kijiji hicho, kilichoko katika Kata ya Naisinyai.

Alisema kwa kushirikiana na watu wa jimbo lake, atahakikisha kuwa wananchi wa Lengasti wengi wao wakiwa ni jamii ya wafugaji, wanapiga hatua za kimaendeleo.

Winter alisema lengo la ziara yake katika Wilaya ya Simanjiro, lilikuwa ni kujifunza mambo mbalimbali ya jamii na kutambua matatizo yanayowakabili wananchi wake.

Alisema tayari ameshajifunza mambo mengi ikiwa ni pamoja na namna ya kuwasaidia wananchi wa eneo hilo, kuondokana na matatizo.Seneta Winter alisema kwa kushirikiana na watu wa Jimbo la Oregon, atahakikisha wananchi wa Lengasti wanatengenezewa miundombinu bora.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Naisinyai, Kilempu Ole Kinoka, alimshukuru seneta huyo kwa kuwachimbia wananchi mabwawa mawili yanayoyatumiwa kwa shughuli za jamii na mifugo.

Alisema kwa sasa wakazi wa kijiji hicho, wanakabiliwa na tatizola ukosefu wa nishati ya umeme kwa ajili ya kuendeshea mtambo wa kuvutia maji ya kunywa na matumizi mengine.

"Huko nyuma wanawake katika kijiji hiki walikuwa wanasafiri kwa umbali wa kilometa 15 wakitafuta maji, lakini sasa maji tatizo hio limepungua hasa baada ya kuchimbiwa mabwawa mawili,"aisema.