Taarifa iliyotolewa na viongozi hao jana kwa vyombo vya habari imetoa masharti manne kufuatia kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar. Sharti la kwanza ni kuzitaka mamlaka zinazosimamia Uchaguzi Mkuu huo kuondoa mara moja tangazo la kuufuta Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar. Sharti la pili ni kumtangaza Seif kuwa ni mshindi halali wa nafasi ya urais na hivyo aapishwe kuwa Rais wa nchi ya Zanzibar ambayo ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sharti la tatu, wametoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuingilia kati na kulaani kwa nguvu zote kinachofanyika Zanzibar ambako kwa mara nyingine tena demokrasia inataka kuminywa wazi wazi ili tu kuinusuru CCM isiondoke madarakani kama ambavyo wapiga kura wamekuwa wakiamua. Aidha sharti la nne ni kwa wananchi wa Zanzibar, “tunapenda kuwahakikishia kuwa tuko nao pamoja katika kipindi hiki kigumu cha kupigania mabadiliko . Kura za Urais Aidha wamedai ushindi wa urais umetengenezwa, kwenye taarifa rasmi ya NEC ambayo imetangaza hadharani na kunukuliwa kwenye vyombo vya habari kwamba; wapiga kura walikuwa 15,589,639. Katika uchaguzi huo kura zilizopigwa 15,193,862 na kati ya hizo zilizoharibika ni 402,248:”Kupitia hesabu hizo hapo juu unaweza kushuhudia upikwaji na utengenezwaji wa matokeo uliofanywa ili kuhujumu matokeo ya Lowassa kwa ajili ya kumbeba na kumpatia ushindi Dk. Magufuli ili kuinusuru CCM.” Viongozi hao walisema Ili kuthibitisha kauli yao kwamba wameongoza uchaguzi katika nafasi hiyo kwa Lowassa ndiye Rais aliyechaguliwa na Watanzania walio wengi walioshiriki uchaguzi Mkuu Oktoba 25. “Tunazitaka mamlaka zinazohusika, kwa mujibu wa katiba, sheria na taratibu za uchaguzi, zitengue matokeo batili waliyoyatangaza na zimtangaze mara moja Lowassa kuwa ni mshindi wa nafasi ya urais na Duni Juma Haji kuwa Makamu wa Rais,” walisema viongozi hao.
Saturday, October 31, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment