Wednesday, November 10, 2010

Wabunge Viti Maalumu hawa

• CCM 65, CHADEMA 23 na CUF 8


na Chalila Kibuda
TUME ya Taifa ya Uchaguzi imekamilisha kazi ya kuwateua wabunge wa awali wa Viti Maalumu na kuwasilisha orodha ya wateule hao katika vyama husika vya siasa.

Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata kutoka ndani ya NEC na miongoni mwa viongozi wa juu wa vyama vitatu vya siasa vyenye wabunge wa Viti Maalumu wamethibitisha kupokea majina ya wabunge hao.

Kwa mujibu wa habari hizo, Chama cha Mapinduzi (CCM) kimepata wabunge 65 wa Viti Maalumu, kikifuatiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilichopata viti 23 na Chama cha Wananchi (CUF) kikapata viti vinane.

Hata hivyo, habari zaidi zinasema kuwa, idadi hiyo ya viti maalum ambavyo jumla yake ni 96 itaongezeka kwa kila chama baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi ulioahirishwa wa wabunge katika majimbo saba.

Chama cha NCCR Mageuzi kilichopata viti vinne vya wabunge, TLP na UDP kimoja, havikupata kiti hata kimoja cha wabunge wa viti maalumu kutokana na kukosa sifa ya kufikisha asilimia tano ya kura za wabunge wote kwa mujibu wa sheria.

Wabunge wa Viti Maalumu wa CHADEMA ambao majina yao yamepitishwa na mikoa wanayotoka kwenye mabano ni pamoja na Lucy Owenya (Kilimanjaro), Esther Matiko (Mara) Mhonga Luhanywa (Kigoma), Anna Mallac (Katavi), Paulina Gekul (Manyara) na Conchesta Rwalumulaza (Kagera).

Wengine ni Suzan Kiwanga (Morogoro), Grace Kiwelu (Kilimanjaro), Suzan Lyimo (Kilimanjaro), Regia Mtema (Morogoro), Christowaja Mtinda (Singida), Anna Komu (Dar es Salaam), Mwanamrisho Abama (Zanzibar), Joyce Mukya (Arusha), Leticia Mageni Nyerere (Mwanza) na Naomi Kaihula (Dar es Salaam).

Majina mengine ya wateule hao ni Chiku Abwao (Iringa), Rose Kamili (Manyara), Christina Lissu (Singida), Raya Ibrahim Khamis (Zanzibar), Philipa Mturano (Dar es Salaam), Mariam Msabaha (Zanzibar) na Rachel Mashishanga (Dar es Salaam).

Wabunge hao ambao wanatarajia kusafiri kwenda mjini Dodoma kuungana na wenzao, wanafanya idadi ya wabunge wote wa CHADEMA hadi sasa kufikia 45.

Kwa mujibu wa habari hizo idadi hiyo inakifanya chama hicho kiwe na sifa ya kuunda kambi ya upinzani bila kutegemea wabunge wa kutoka vyama vingine vya upinzani.

Kwa upande wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho hata hivyo majina ya washindi hayakuweza kupatikana, kimepata idadi ndogo ya viti tofauti ilivyotarajiwa.

Kundi lililoathirika ni la Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM), iliyotarajiwa kupata viti 10, lakini imepata viti sita, viwili kutoka Zanzibar na vinne kutoka Tanzania Bara.

Kundi lililobahatika ni la wanawake walioomba kupitia asasi zisizo za kiserikali (NGO) ambalo wamo Ritha Mlaki na Anna Abdallah.

Wabunge wa viti maalumu CCM ni pamoja na viongozi wakuu wawili wa jumuiya ya wanawake wa chama hicho (UWT), ambao ni mwenyekiti wake, Sophia Mnyambi Simba na katibu wake, Amina Nassoro Makilagi.

Wengine ni Gaudentia Mugosi Kabaka, Ummi Ally Mwalimu, Agnes Elias Hokororo, Martha Jachi Umbulla, Lucy Thomas Mayenga na Faida Mohamed Bakari.

Walioteuliwa wengine ni Felista Alois Bura, Kidawa Hamid Saleh, Stellah Martine Manyanya, Maria Ibeshi Hewa, Hilda Cynthia Ngoye, Josephine Johnson Genzabuke na Esther Lukago Midimu.

Wengine ni Maida Hamad Abdallah, Asha Mshimba Jecha, Zarina Shamte Madabida, Namalok Edward Sokoine, Munde Tambwe Abdallah, Benardetha Kasabago Mushashu, Vick P. Kamata, Pindi Hazara Chana, Fatuma Abdallah Mikidadi, Gertrude Rwakatare, Betty E. Machangu, Diana Mkumbo Chilolo, Fakharia Shomari Khamis, Zaynabu Matitu Vulu, Abia Muhama Nyabakari, Pudenciana Kikwembe, na Lediana Mafuru Mng’ong’o.

Walioteuliwa wengine ni Sarah Msafiri Ally, Catherine V. Magige, Ester Amos Bulaya, Neema Mgaya Hamid, Tauhida Galos Cassian, Asha Mohamed Omari, Dkt. Fenella E. Mukangara, Terezya Lwoga Huvisa, Al-Shaymaa Kwegir na Margreth Mkanga.

Angellah Jasmin Kairuki, Zainab Rashid Kawawa, Mwanakhamis Kassim Said, Riziki Said Lulida, Devotha Mkuwa Likokola, Christina Ishengoma, Mariam Salum Mfaki, Margreth Simwanza Sitta, Subira Khamis Mgalu, Rita E. Kabati, Martha Moses Mlata, Maua Abeid Daftari na Elizabeth Nkunda Batenga.

Wamo pia, Azza Hillal Hamad, Mary Machuche Mwanjelwa, Josephine T. Chengula, Bahati Ali Abeid, Kiumbwa Makame Mbaraka, Roweete Faustine Kasikila, Anastazia Wambura na Mary Pius Chatanda.

No comments: