Friday, October 29, 2010

Mtaji Azania wafikia bilioni 18.4

MTAJI wa benki ya Azania imefikia Sh bilioni 18.4 kutoka Sh milioni 700 wakati ilipoanzishwa mwaka 1995.

Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa tawi jipya mjini Kahama mkoani Shinyanga, uliofanyika mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Charles Singili
alisema, kupanda kwa mtaji ni dalili za wazi za benki hiyo kuzidi kujiimarisha.

Alisema, pamoja na mafanikio hayo hawajabweteka na kwamba wana mikakati ya kuhakikisha kuwa huduma zao zinaendelea kuimarika kadri miaka inavyosonga mbele.

Singili alisema, mafanikio waliyofikia ni matokeo ya kazi na usimamizi mzuri wa menejimenti ya benki hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa kibenki wakiwemo wateja wanaounga mkono huduma zao.

Benki hiyo iliyoanzishwa na Watanzania, kwa saa ina wanahisa wengi wakiwamo NSSF asilimia 35, PPF asilimia 30, PSPF asilimia 12, NAPF asilimia 14, EADB asilimia 6 na wadau wengine wa kawaida wa kitanzania wanaomiliki asilimia 3.

Singili alisema, wanaendelea na mipango ya kupanua huduma zao katika maeneo mbalimbali nchini ambapo kwa sasa wametoa kipaumbele katika miji ya Geita, Katoro na
Kagongwa ili yaweze kupata huduma za benki hiyo kwa lengo la kufungua matawi mengine katika ukanda wa Ziwa.

"Sanjari na maeneo hayo ya Kanda ya Ziwa lakini pia benki hiyo inatarajia kufungua matawi mengine katika mikoa ya Dodoma, Morogoro, Ruvuma na Mbeya katika mji wa Tunduma", alisema Singili.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Yohana Balele ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo alisema, serikali inaunga mkono jitihada zinazofanywa na benki ya Azania katika msingi wa kuelekea mafanikio ya kiuchumi kwa watanzania na taifa kwa ujumla.

Balele aliongeza kwa kusema kuwa mbali na huduma nyingine zinazotolewa na benki hiyo ni mikopo kwa wajasiriamali wadogowadogo ambao wanatumia huduma hiyo kama msingi wa kujiletea maendeleo na kukuza

No comments: