Friday, October 30, 2009

Waturuki wai 'HACK' website ya microsoft

Kundi hilo linalojulikana kama “Terrorist crew” liliiteka kwa masaa kadhaa website ya Microsoft maalumu kwa nchi ya Ireland na kuwaachia wadau wa website hiyo salamu za idi Mubarak.

Mwaka 2006 kundi jingine la waturuki liliiteka website ya Microsoft ya Ufaransa na kuwaachia wadau wa Microsoft ujumbe huu:
"Hi Master (: Your System 0wned By Turkish Hackers! redLine ownz y0u! Special Thanx And Gretz RudeBoy |SacRedSeer| The_Bekir And All Turkish HacKers next target: microsoft.com date: 18/06/2006 @ 19:06 WE WERE HERE...."

Kundi la vijana wa kituruki limekuwa likishindana na kundi la vijana wengine wa Urusi katika kuziteka tovuti mbali mbali duniani.

Mwaka 2005 kundi hilo lilifanikiwa kuziteka computer za vyombo vikubwa vya habari vya marekani kama vile CNN, New York Times, ABD News na vinginevyo na kufanikiwa kutuma virusi kibao ambavyo vilivuruga mitambo yao.

Mojawapo ya tovuti zilizowahi kutekwa na kundi la waturuki ni tovuti ya aliyekuwa mgombea wa nafasi ya uraisi wa Marekani kupitia chama cha Republican Duncan Hunter,tovuti ya chama cha soka cha Denmark ,tovuti ya NGO moja ya kupambana na ukimwi nchini Ufaransa ya Solydays.

Katika tukio la jana vijana hao waliwashangaza wadau wa Microsoft waliotembelea tovuti hiyo jumanne asubuhi kwa kukuta meseji ya EID MUBARAK na meseji yao ya kujipongeza kwa kuiteka website hiyo.

Hata hivyo wataalamu wa microsoft walifanikiwa kurekebisha tatizo hilo ingawa liliwachukua masaa kadhaa.

Msemaji wa Microsoft Ireland alisema "Hakukuwa na ubadhirifu wowote uliofanyika kutokana na tukio hilo".

"Kulikuwa na mapungufu katika ulinzi wa tovuti yatu ,Wataalamu wetu wanashughulikia tatizo hili ili lisitokee tena " aliongeza msemaji huyo.

No comments: