Tuesday, July 7, 2009

“MIKIKI MIKIKI”-JUMA NATURE FT CHAMELEON


Mojawapo ya mambo ambayo yanaweza kukufurahisha kama unapenda muziki kutoka Afrika Mashariki ni pale wasanii kutoka nchi zinazounda Afrika Mashariki wanapoamua kushirikiana katika kazi zao. Mifano ipo mingi kuonyesha jinsi gani mipaka iliyowekwa na mtawala wa enzi hizo inaweza kuvukwa japo kwa kutumia muziki.

Nimewahi kuandika siku za nyuma kwamba wakati viongozi wetu wanasuasua katika kukamilisha muundo wa jumuiya ya Afrika Mashariki(ukiniuliza mimi nitakwambia ni kwa sababu kila mmoja anaweka mbele maslahi binafsi badala ya faida nyingi za muungano makini) wasanii wao wameshavuka kizingiti hicho.Wanashirikiana.

Miongoni mwa mifano ya ushirikiano huo ni huu wa Juma Nature akimshirikisha Jose Chameleon(Uganda) katika wimbo unaokwenda kwa jina Mikiki Mikiki. Kama ujuavyo hawa wote ni ‘majina makubwa” katika muziki wa ukanda wetu. Wanaposhirikiana tunategemea kitoke kitu makini.Nakuomba uwe muamuzi.

No comments: