Saturday, March 28, 2009

Masikini Chenge!


Mbunge wa Bariadi Mashariki,Andrew Chenge “Mzee wa Vijisenti” yupo matatani…tena.Safari hii ni kwa kupata ajali ya barabarani(kugonga) na kusababisha vifo vya watu wawili ambao walikuwa ndani ya usafiri maarufu kama “Bajaji”.Waliofariki inasemekana ni wanawake wawili ambao ndio walikuwa abiria katika Bajaj hiyo.Dereva wa Bajaj hajulikani alipo.

Tukio hilo limetokea alfajiri ya leo katika maeneo ya Oysterbay(karibu na nyumbani kwake).Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Kanda Maalumu ya Polisi Dar-es-salaam, Afande Kova, Chenge alikuwa akiendesha gari aina ya Pick Up-Hilux yenye namba ya usajili T512 ACE.Bajaj iliyohusika kwenye ajali ina namba za usajili T736 AXE na imeorodheshwa kama mali ya Zuwena Feith Nassoro wa SLP 2595 Dar-es-salaam.

Baada ya tukio hilo,Mheshimiwa Chenge alijisalimisha katika kituo cha Polisi Oysterbay na anaendelea kuisaidia polisi.Habari hii bado inaendelea…

No comments: