Monday, February 2, 2009

HAINA NGWASU-INSPEKTA HARUNI


Bila ubishi Inspekta Haruni ni miongoni mwa wasanii wa Bongo Flava ambao wanastahili na wana haki kabisa ya kujiweka katika lile kundi la “wakongwe katika fani”.Pia Inspekta anadumu katika lile kundi la “wataalamu wa vina(mashairi) na tunzi ambazo baada ya kutoka hewani hugeuka zikawa misemo ya mitaani.


Kama hukubaliani name,basi jaribu kuusikiliza kwanza wimbo mpya kutoka kwa Inspekta unaokwenda kwa jina la Haina Ngwasu kwa kubonyeza player hapo chini.


Na kama jadi mpya ya wasanii wa bongo flava mashairi ya wimbo huu yanaelekea kuwa “ujumbe” kwenda kwa mtu fulani au watu fulani?Mawazo yangu.Sikiliza na wewe utuambie.Pata burudani

No comments: