Wednesday, June 4, 2008

Mrembo asukwa akiwa utupu
Picha hizo, baada ya kupigwa ziliingizwa katika mtandao ambao unatangaza shughuli za kitalii za kisiwa hicho ambapo kila mtu anaweza kuziona kwa ‘raha zake’.

Hata hivyo, baadhi ya watu ambao walibahatika kuziona, walisema kuwa wageni wanaofika kwenye kisiwa hicho wanaweza kuharibu mila na desturi za Watanzania kwa kuiga tamaduni zao.

“Ni muhimu kuzingatia dini na tamaduni za nchi husika kwa wanaume na wanawake kuwa na staha kuhusu mavazi,” alisema mmoja wa wakazi wa Zanzibar walioziona picha hizo kupitia mtandao.

Kwa mujibu wa taratibu za visiwa hivyo, mavazi ya ufukweni yanaruhusiwa tu sehemu husika, kutembea uchi au nusu uchi hairuhusiwi licha ya baadhi ya wageni wanaoingia humo kudharau.

Taratibu hizo pia zinakataza kunywa pombe hadharani isipokuwa katika hoteli, baa au migahawa ya kitalii. Aidha, watu kuonyesha mapenzi hadharani kama kupigana busu, kukumbatiana pia hairuhusiwi.

No comments: