Thursday, April 10, 2008

Hii ni Kali


Kitu mbaya kilichofanywa na jamaa huyo aliyejulikana kuwa ni mume wa mtu, ni kucheza muziki bila staha na mcheza shoo maarufu wa Bendi ya Msondo na kulalamikiwa na mkewe ambaye alidai mumewe amemdhalilisha mbele ya kadamnasi.

Tukio hilo, lilichukua nafasi kwenye Ukumbi wa Africenter uliopo Ilala, Dar es Salaam ambako Msondo Music Band, walikuwa wakifanya ‘makamuzi’ yao.

Mwandishi wetu, aliyekuwa shuhuda wa tukio hilo, awali alimuona mwanaume huyo akisakata ‘rhumba’ kwa staili tofauti, huku akionekana kama mtu aliyejitwika ‘glasi’ kadhaa kichwani.

Shabiki huyo ambaye baadhi ya watu walimbatiza jina la ‘Mr. Midadi’, kutokana na kucheza mfululizo nyimbo za Msondo, muda wote wa shoo hiyo, baadaye ‘alidatishwa’ zaidi na miondoko ya mnenguaji wa bendi hiyo kabla ya kujisogeza na kuanza kucheza karibu yake.

Wakiwa wanacheza, mnenguaji huyo alikuwa akibinuka katika staili tofauti na kumchezea ‘kihasara hasara’ Mr. Midadi, kitendo kilichosababisha kushangiliwa na mashabiki ukumbini humo.

Hata hivyo, wakati shoo ikielekea ukingoni, lilizuka zogo baina ya shabiki huyo na mwanamke ambaye baadaye ilibainika kuwa ni mke wake, aliyedai kwamba mume wake hamheshimu, ndiyo maana alithubutu kucheza kihasara na mnenguaji wa Msondo.

Huku akiwa amemkunja mumewe, mwanamke huyo alisikika akifoka: “Wewe mwanaume hovyo kabisa, umenifanyia kitu kibaya sana, yaani unacheza na mnenguaji vile tena mbele yangu?

Baada ya kuambiwa hivyo, mume mtu alianza kumng’ang’aniza mkewe warudi nyumbani ambapo mwanamke huyo alipinga na kusababisha vurumai kubwa kutokea.

Ugomvi baina ya wapenzi hao, uliamuliwa na walinzi wa ukumbi huo pamoja na mashabiki wachache.

No comments: