Friday, February 1, 2008

Ugonjwa wa Aisha Madinda ‘ngoma nzito’


Aisha, hivi karibuni alinukuliwa na gazeti moja la michezo nchini akisema kuwa, hali yake bado sio nzuri licha ya kufanyiwa uchunguzi wa awali.

Mnenguaji huyo aliongeza kuwa, kushindikana kuonekana ugonjwa wake kumesababisha madaktari bingwa wa moyo kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam juzi (Jumatatu) mchana kuanza kumfanyia uchunguzi wa kina.

“Uchunguzi wa awali umeshindwa kubainisha ugonjwa wangu ndio wamenirudisha kwa madaktari bingwa wanifanyie uchunguzi zaidi, miguu imevimba na sijisikii vizuri, lakini kinachonisikitisha zaidi ni kutoonekana kwa maradhi yanayonisumbua.

“Nawaachia wataalam, nina imani kama kuna kitu hawawezi kushindwa kwani nitapona tu, Mungu ni wa wote,

naamini atanisaidia na hii ni hali ya kawaida tu kwenye maisha wala siamini maneno ya watu kuwa nimepigwa juju,” alisema Aisha.

Mnenguaji huyo mwenye watoto wawili wanaosoma sekondari, amekuwa nje ya jukwaa kwa zaidi ya miezi mitatu sasa kutokana na kusumbuliwa na maradhi.

Aisha amewaomba wadau mbalimbali na mashabiki wa muziki nchini kuendelea kumsaidia kwa hali na mali ikiwa ni pamoja na kugharamia matibabu yake.

Anayependa kumsaidia apige namba 0717 555557 ambayo ni ya meneja wake.

No comments: