Friday, February 1, 2008

Kimwana Manywele achojoa nguo hadharani


Tukio hilo lililoshuhudiwa na waandishi wetu, lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika bonanza la bendi hiyo linalofanyika kila Jumapili katika Ukumbi wa Msasani Beach ambapo kimwana huyo alipanda stejini na kuanza kucheza Pekechapekecha huku akichojoa nguo zake.

Kimwana huyo, alipandwa na mzuka baada ya kushangiliwa na mashabiki ndipo alianza kuchojoa nguo ili kuonesha umahiri wake wa kunengua.

Kufuatia kitendo cha kusaula nguo kilichofanywa na mwanadada huyo na kusababisha sehemu kubwa ya mwili wake kuwa wazi, watu wengi walimshangilia, miongoni mwao wakiwa ni watoto wadogo.

Hata hivyo, baadhi ya watu waliokuwepo ukumbini hapo walisema kuwa, binti huyo alilazimika kufanya hivyo kutokana na kuwa na mwili mkubwa na kuvaa mavazi yaliyomshika mwili hali iliyosababisha ashindwe kunengua vizuri.

Waziri Kapuya ni miongoni mwa wapenzi wa burudani nchini ambaye alikuwepo ukumbini hapo kushuhudia jinsi vijana wa masauti wanavyokandamiza ‘kijotijoti’ kiasi cha kumfanya ainuke kwenye kiti na kwenda kulicheza sebene.

No comments: