Saturday, February 16, 2008

SINTA NI MAREHEMU JAMANIHuyu ndiye aliyemuumiza Juma Nature

Sinta aliwaambia waandishi wetu, wiki iliyopita akiwa nyumbani kwake Kimara, Dar es Salaam kwamba kuanzia sasa hivi angependa aitwe Christine peke yake.

“Sinta ni marehemu jamani, yaani ameshafariki siku nyingi, hivi sasa amebaki Christine peke yake. Nimeamua iwe hivyo kwasababu sitaki mambo ya sanaa wala kufuatwafuatwa na vyombo vya habari,” alisema Sinta.

Mbali na hilo, waandishi wetu waliweza kufanikiwa kumuona mtoto wa kiume wa galacha huyo wa maigizo anayeitwa Boyii ambaye ana umri wa miezi minane.

Ilielezwa kuwa mtoto huyo, Sinta alijifungua akiwa nchini Uganda, alikokuwa masomoni.
Hata hivyo, habari za ndani zinasema kwamba mzazi mwenza wa Sinta ni Mtanzania.

No comments: