Wednesday, January 23, 2008

Mke wa Banana avunja ndoa


Suzy na wifi yake huyo ambao inadaiwa walikuwa marafiki wakubwa, hivi sasa hawapikiki chungu kimoja baada ya Davina kubaini kuachika kwake kumesababishwa na Suzy.

Chanzo chetu cha kuaminika kinasema kwamba, Suzy inadaiwa alianza kupeleka maneno ya umbea kwa kaka yake kuhusu wifi yake, hivyo kusababisha mapenzi ya wawili hao kuanza kuyumba.

Inadaiwa maneno hayo ya umbea alianza kuyapeleka mara baada ya kaka yake, kufunga ndoa na Davina kwa kile kinachodaiwa kumchukia ghafla.

Chanzo chetu kinadai sababu kubwa ya kuwagombanisha wapendanao hao, ni pale alipoona kaka yake hamsikilizi vizuri kama mwanzo zaidi ya kuhamishia mapenzi kwa mkewe.

Mtoa habari kwetu aliendelea kudai kuwa, Suzy hakuishia hapo, bali aliendelea kutoa maneno ya kichonganishi hata kwa ndugu wengine wa familia yao na kujikuta akichukiwa na wengi.

“Kitendo kile kilimkosesha raha na kujiona hana thamani katika familia hiyo, kwani mumewe aliwasikiliza ndugu zake kuliko mkewe na ilifikia hatua hata fedha za matumizi akawa anaachiwa mfanyakazi wa ndani.
“Baada ya Davina kuona hata mumewe hana ushirikiano naye aliamua kuikimbia nyumba na kurudi kwao, mumewe alimfuata lakini alikataa kurudi ,” kilisema chanzo chetu.
]
Inadaiwa Hashimu anaishi kwenye nyumba ya familia iliyopo Mtoni Kijichi, Dar es Salaam na sharti lililotolewa na Davina ili arejee, ni kuwa wahame hapo lakini mumewe alikataa kwa kile kinachodaiwa kuonekana kama anatawaliwa.
Alipoulizwa kuhusu hilo, Davina awali alikataa kuzungumza lakini alipobanwa aliomba aachwe apumzike kwani kuna mengi anayokumbuka ambayo yanamtia machungu.

Ila alikiri Suzy kuhusika na kuachwa kwake, kwani mkono wake katika hilo ulikuwa mkubwa.
”Ninachojua hadi sasa Suzy amechangia kwa kiasi kikubwa kuvunjika kwa ndoa yangu, kwani yapo mengi aliyoyafanya juu ya ndoa yetu, lakini yote namuachia Mungu. Naye kaolewa, atatendewa kama alivyonitenda,” alisema Davina
Suzy yeye alikana kuwaachanisha na kudai sababu ya wao kuachana wanaijua wenyewe.

“Sikiliza nikuambie, mapenzi hayaingiliwi hata siku moja kwa wapendanao na mimi siwezi kuvunja ndoa ya kaka yangu, ina maana sitaki niwe na wifi, kama waliachana nadhani ipo sababu ambayo wanaijua wenyewe.

“Lakini mimi sihusiki hata kidogo. Kama Davina na ‘bro’ walichefuana na kupigana vibuti wanajua wao wenyewe siyo mimi,” alisema Suzy hashimu alipoulizwa kuhusu hilo, alimtetea Suzy na kudai hajahusika na kumpa talaka Davina isipokuwa mtalaka wake huyo anajua sababu halisi za yeye kuachwa.

“Kama Davina ndiyo alikuambia maneno hayo sawa, lakini kama mnataka ukweli kutoka kwangu mdogo wangu Suzy hajachangia chochote katika kuvunjika kwa ndoa yetu.

“Sababu za kumuacha anazijua Davina mwenyewe, kama yuko tayari awaeleze lakini si mdogo wangu,” alisema Hashimu.
Kwa upande wa Davina alikuwa mgumu kidogo kuliongelea hili lakini baada ya muda alitoa ushirikiano kwakueleza kuwa”mi ninachojua hadi sasa Suzy amechangia kiasi kikubwa sana kuvunjika kwa ndoa yangu lakini yapo mengi aliyo yafanya juu ya ndoa yetu lakini yote namuachia Mungu naye kaolewa akayaone,” alisema Daviana.

Pia alisema yapo mengi ambayo angeongea lakini anapokumbuka inamuuma sana kwani yanamrudishia maumivu yaliyoanza kupona.

No comments: