Friday, October 29, 2010

JK, Lipumba, Slaa na falsafa zao

Imeandikwa na Beda Msimbe; Tarehe: 29th October 2010 @ 19:40



Rais Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Dk. Willibrod Slaa.


Habari Zaidi:
IGP Mwema aahidi haki, amani katika uchaguzi
Tendwa: Kampeni zimeenda vizuri
JK, Lipumba, Slaa na falsafa zao
Ilikuwa vuta n’kuvute Chadema, CCM
Programu ya Urithi wa Ukombozi Afrika yaanza
Tujitanue kutangaza utamaduni wetu
Potwe mwenye madoa anavyoonekana majini.
UTAJIRI WA KISWAHILI:kijiti kimoja hakisimamishi jengo
Semayoga: Mfungwa aliyepata shahada gerezani
Umeme wa nguvu ya jua tegemeo jipya
Polisi wajiimarisha katika weledi
Morogoro ilivyojipanga kwa uchaguzi mkuu
VICOBA vyasaidia kuinua wanachama
Kilimo cha chai mkombozi wa wananchi Muheza
Asomesha watoto kutokana na ufugaji kuku
Wana Ludewa kunufaika na umeme wa Gridi
Ushindani ubunge Arusha Mjini
Kiama cha CUF chawadia Pemba
Tumieni nadharia za ukweli Oktoba 31
Wanaomchimba JK wameahidiwa nini?



Habari zinazosomwa zaidi:
Balaa lingine kwa Chenge
Salama: Jasiri aliyetangaza kuishi na virusi vya Ukimwi
Dina Marius, mrithi wa Amina Chifupa
‘Housigeli’ anataka kuniharibia ndoa
Vatican yamvua jimbo Askofu
Kikwete achekecha wakuu wa wilaya
Waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano waongezeka kwa 22%
Interpol yatumika kusaka wenye zeutamu
Orijino Komedi, Jay Dee waitwa Iringa
JK apigilia msumari wa mwisho Dowans


Jumapili hii ni siku ambayo Watanzania wanafanya uchaguzi wa uongozi wa juu, watunga sheria na madiwani.

Katika nafasi ya juu ya urais kuna wagombea saba, lakini mpaka kampeni inamalizika watatu ndio wamejitokeza zaidi katika vyombo vya habari.

BEDA MSIMBE anawaangalia wagombea hao na falsafa zao. BAADHI ya magazeti yamejipambanua wazi bila kujitaja rasmi kwamba yanapigania upinzani, huku sehemu kubwa ya watumiaji wa mitandao wakionesha ugumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuingia madarakani kwa madai kwamba kimeshindwa kushughulikia ufisadi.

Kwao, Oktoba 31 ni siku ya mwisho kwa CCM kutawala. Maandishi yao kwa namna nyingine kwa mtu anayefanya safari ya kisaikolojia na falsafa, yanaonesha kupelea kwenye vina vya vibwagizo vyao.

Uchaguzi ni zaidi ya wajihi wa mtu na falsafa inayotawala maisha ya wakati huo na msingi wa daraja la baadaye. Katika hilo, Profesa Ibrahim Lipumba, Dk Jakaya Kikwete na Dk Willibrod Slaa wanatofautiana.

Katika zaidi ya siku 70 kila mgombea alitumia mtindo wake kuomba kura na katika wote, walioonesha kukomaa kisiasa ni Lipumba na Kikwete kwa kutoa hoja.

Hoja ya ni nini wataifanyia Tanzania na nini mwingine amefanya, lakini Dk Slaa katika patashika nzima, alikuwa na majina ya watu midomoni, makombora aliyofyatua bungeni na hata sehemu moja hakuzungumzia majibu ya serikali katika kukabiliana na hoja zake.

Kuna kila sababu ya kuwaangalia watu hawa katika mizania yao ya elimu, uwezo wao wa kifalsafa na kisaikolojia na dhima nzima ya uongozi katika vipaji vyao. Dk Kikwete katika moja ya hotuba zake za mwisho, alisema wazi kwamba hana sababu ya kutaja majina, lakini pia katika mkutano wake wa Karatu ambayo ni ngome ya Dk Slaa, alisema hana sababu ya kutaja upungufu wa watu hadharani.

Vyombo vya habari vyenye itikadi na inda dhidi ya CCM, vimedhihirisha wazi vita baridi ya wajihi wa mtu na kudai serikali imeshindwa kukabiliana na rushwa. Pengine ni tatizo ambalo hata mwanafalsa Plato alilizungumza kwenye mbisho wa kiza katika pango, walakini wake katika utunzi wa sheria, mrejesho wake na ufuatiliaji wa utekelezaji makini kwa sheria ionekane, bila kupoteza umakini.

Hili limezaa utawala wa sheria ambao huwezi kukurupuka kwa sababu kuna madai, ukamfunga mtu, mahakama ndizo zenye uwezo wa kufunga. Mashitaka dhidi ya watu wanaotuhumiwa kutumia madaraka vibaya na wale wanaotuhumiwa kushiriki wizi wa mali ya umma, yako mahakamani, kusema kwamba wameshindwa kuondoa rushwa ni kashfa isiyokubalika.

Ipo methali ya ‘mnyonge, mnyongeni haki yake mpeni’. Usemi huu unataka kila mtu apewe haki yake, Profesa Lipumba ameyaweza hayo amekuwa akizungumzia suala la wenzao wameshindwa wapi na wao watafanya nini.

Falsafa ya CUF ni haki sawa kwa wote na hili ndilo lililokuwa linahubiriwa kila mahali anakokwenda; Chadema yenye mrengo wa kibwanyenye kihusiano inamtaja sana Nyerere; CCM yenye uwezo wa kujibadili kuzingatia utaratibu wa kiutawala wa kisasa, bado inahubiri Ujamaa kwa namna ya kutumikia Taifa na kuacha ubaguzi.

Dk Slaa anaonekana kuwa mshika bunduki zaidi akilenga katika mambo ambayo mtu mwenye akili za wastani hawezi kuchambua mpaka mwisho na kwa kuwa ni mtaalamu wa saikolojia, asilimia 25 ya ukweli huumbwa katika asilimia 75 ya maeneo elekezi, ili kuondoa nafasi ya upenyo wa kutambua ukweli na ugumu wa tatizo lililo mbeleni.

Hapo unaweza ukaona katika maeneo aliyotembelea yenye utata mkubwa, kama sehemu zenye madini na kwa wafugaji.

Wafugaji wenye utamaduni wa kuheshimu mifugo yao na utajiri wa ng'ombe wamekuwa wakiambiwa kwamba wanashindwa kujenga nyumba kwa sababu za gharama za vifaa vya ujenzi na kwamba saruji itashuka ghafla tu kwa kuondoa kodi, papo hapo wanasema kodi inatosha kuwezesha elimu bure.

Mkanganyiko wa kuondoa kodi na kutoa elimu bure kwa fedha za madini ambazo haziainishwi wazi, zinaleta mushkeli mkubwa katika falsafa ya mrengo wa kibwanyenye.

Akiwa mtaalamu wa kukabiliana na akili za kawaida, kuweza kujaza kasumba kwa kutumia hali ya umasikini na elimu ya watu, amekuwa akizungumzia mrabaha unaoachwa kwa halmashauri, katika upande wa madini akiacha kuzungumiza kodi zilizopo ambazo zinafanya asilimia 45 ya pato la madini kubaki nchini.

Mwenendo mzima wa kampeni umezingatia zaidi uwezo wa wazungumzaji wenyewe na namna wanavyoangalia jamii na hili ndilo hasa ninalotaka kuzungumzia. WASIFU Dk Willbrod Pter Slaa Hebu tuanze na Dk Willbrod Pter Slaa.

Lakini tuanze kwanza kwa nukuu kutoka kwa mmoja wa wanasiasa mahiri hapa nchini, Spika wa Bunge la Tanzania, Samuel Sitta. “Moja ya vitu ambavyo mbunge anatakiwa kuvifanya katika kazi zake ni kuangalia utendaji kazi wa serikali na kuishauri inavyostahiki kila kunapotokea shauri linalohusu taifa....” (Samuel Sitta Machi 5, 2009 mjini Dar es Salaam). Kama hivi ndivyo inavyostahili kuwa Dk Slaa hana haki ya kusema hivi hadharani katika mambo ambayo alishiriki kuyafanya na pengine ndiye aliyeshauri vibaya.

Masuala kama ya madini, matatizo ya Epa, matumizi mabaya ya mamlaka, yote ni masuala ambayo yalizungumzwa bungeni na yakapewa majibu na maelekezo na serikali mengine bado inaendelea kuyafanyia kazi.

Suala la Madini nakumbuka mmoja wa wanasiasa ambaye alishiriki moja kwa moja katika kulihoji kusaidia kutengeneza mustakabali wa sheria mpya ya madini yenye lengo la kulinda rasilimali na kuwawezesha Watanzania wenye mitaji midogo ni Zitto Kabwe Mbunge machachari wa Chadema kutoka jimbo la Kigoma kaskazini.

Hata katika moja ya vikao vikali vilivyokuwa na msuguano mkubwa kubadili sheria baada ya mvutano bungeni, Zitto alikuwa msaada mkubwa, anajua mengi na aliisaidia serikali lakini leo Slaa anasema serikali haijafanya kitu.

Lakini pia katika maisha ya kawaida, mtu hawezi kutoka na kutukana msingi wa majadiliano kwa kuubomoa ukweli na kusema uwongo kwa lengo tu la kupata kura. Ukweli ni sehemu muhimu sana ya kusaidia serikali iliyopo madarakani lakini staili aliyoitumia Dk Slaa katika kampeni ni staili inayotokana na malezi yake na masomo aliyosoma ambayo hutumia upeo wa saikolojia, kubabatiza hata ukweli kuonekana uwongo na mazingira ya kutokuaminika kuwa ya kweli.

Akiwa amezaliwa Oktoba 29, 1948 amepitia sehemu kubwa ya elimu yake ukiachia shule ya msingi katika sekondari na vyuo vya kansia Katoliki. Pamoja na kuchukua elimu ya maendeleo vijijini kupitia chuo kikuu cha Thomas Aquinas na cheti cha menejimenti pia alipitia seminari za Dung'unyi, Itaga; mwaka 1973 alimaliza elimu ya filosofia katika shule kuu ya Kibosho na teolojia shule kuu ya Kipalapala.

Alienda Roma, Italia kwenye Chuo Kikuu cha Urban na kupata digrii yake ya udaktari akibobea katika sheria za kanisa na za kawaida (PhD -JCD- Law)katika hali ya kawaida mtu wa kanisa anayechukua hii ni mmoja wa watu waliobobea katika sheria.

Wakitumia vibaya elimu yao waweza kuwa watu hatari. Sipendi kuzungumzia elimu nyingine alizo nazo na mamlaka aliyo nayo kwa watu kutokana na elimu hizo nilizozitaja hapo juu, ninachotaka kusema, silaha akipewa mtu ambaye anashindwa kuelewa madhara yake kwa wengine inaweza kuwa hatari kubwa.

Akiwa Rome, Italia akiwa bado ni padri alijiingiza katika madaraka ya kisiasa kupitia Chama Cha Mapinduzi - alikuwa Katibu wa CCM Foreign Branch (Rome) na kabla yake alipata kuwa katibu wa Tanu wa Umoja wa vijana na mwenyekiti wa akiwa Kipalapala.

Nafasi ya kuwa na madaraka lazima iwepo katika msingi unaofuata taratibu, lakini katika wanasiasa waliozungumza athari za watu wenye akili kutumia vibaya akili zao yupo Mtakatifu Agustino na nadharia yake ya kujenga Mji wa Mungu kwa kuwa na hofu ya Mungu na kutii mamlaka lakini yupo Plato kabla ya kuzaliwa Kristo ambaye alizungumzia kwa kina madalali wa maangamizi ambao hutumia fikira kupanga yasiyowezekana katika akili za kawaida.

Nazungumza kwa mifano kwa sababu nimekuwa nikitazama staili ya kuomba kura, staili ya kutaja majina ya watu ukidai una ushahidi kwamba wao ni mafisadi, kuwatukana mpaka matusi ya kudhalilishana katika hali ya kutumia muamara mdogo wa maarifa uliopo ndani ya watu wa akili za wastani.

Wengi na si suala la kutukana ukweli tuna akili za wastani tunaoataka faradhi ya kuambiwa yanayowezekana ambayo hayawezekani na kufurahishwa na hilo bila kufanya mchanganuyo wa nguvu unaokutanisha pointi zote za inayowezekana na isiyowezekana. Maarifa ni kitu kingine na akili ni kitu kingine.

Maarifa waliyonayo watu ni haba na hata Biblia inazungumza lakini wapo waliojawa na vipawa vya majitu na wanaweza kufanya mambo ya kushangaza na majitu hayan ynapoasi huwa chukizo.

Si ajabu matusi yaliyoambatana na watu kutotaka kusikia wasiyotaka kuambiwa yameambatana na Dk Slaa katika mikutano yote inayokaribia 500 akisema wazi haogopi kitu, mhanga hatari katika dunia ambayo siasa za wastani ndio hasa nia ya kuuweka ubinadamu na utu katika sehemu yake.

Profesa Ibrahim Haruna Lipumba Ni msomi wa masuala ya uchumi aliyezaliwa kijiji cha Ilolangulu Wilaya ya Tabora mkoani Tabora Juni 6, 1952 ameendesha kampeni yake kistaarabu zaidi, huku akionesha wapi CCM wamekosea na wapi wao kama Chama wanataka kuchukua nafasi ya kufanya mema na makubwa zaidi kwa taifa la Tanzania.

Akijua ubaya wa kudanganya watu katika kampeni zake alionekana kuwa mgombea pekee ambaye alitumia vyema elimu yake ya uchumi kuomba kura kwa kusema yale ambayo yanawezekana na mengi yakiwa ni kubadili mfumo wa kiuchumi kuufanya uweze kukidhi mahitaji ya watu.

Hakutaja majina ya watu, wala hakupambana na watu, alikuwa katika kueleza zaidi wananchi watarajie nini kutoka kwa Chama chake cha Wananchi (CUF) kama yeye mchumi ataingia madarakani. Ukipima hesabu zake na maelekezo yake unaweza kutambua kwamba udaktari wake wa uchumi kutoka Stanford si wa kubahatisha na busara alizo nazo ni sehemu ya kuiva katika madaraka.

Kampeni zake zilionyesha kwanini yeye ni profesa na kwa nini amekuwa akiandaa wasomi wa masuala ya kiuchumi na hakuwa anababaisha katika takwimu zinaozohusu uchumi na ndio maana alikuwa na sababu ya kupeleka sera zake katika mazingira ya usomi zaidi.

Akijua mwako wa vijana (kwani alishawahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tangu mwaka 1975 hadi 1976) ameendelea kuwa mfano hata anapoingia katika mikoa ambapo alikuwa anaenda kusalimia wakuu wa wilaya akijua kwamba kufanya kazi ni vyema kujenga mahusiano huru na ya kiutendaji kwa kujali na kuheshimu mamlaka iliyopo.

Hakuwa anasita kuwaomba kura wakuu wa wilaya tena kwa lugha nzuri zaidi huku akisema nini atawafanyia kama yeye atakuwa Rais, alikuwa na hoja za uchumi na alikuwa na hoja za ustawi na haki sawa kwa wote. Haki hizo sawa alikuwa anazijumuisha katika maisha bora akiamini mabadiliko kuanzia kwa wananchi katika mfumo wa kujielewa.

Mwaka 2005 alimaliza akiwa wa pili nyuma ya Kikwete kwa asilimia 11.68 ya kura zote na kama watu watakuwa na busara zaidi anaweza kujiongezea kura zaidi katika hili japo anaelewa wazi kwamba huenda asiende Ikulu.

Nimesema hivyo kwa sababu lugha yake aliyoitumia mara ya mwisho kule Kigoma ilionyesha kwamba anakubali yaishe akitaka Kikwete adhibitiwe safari zake za nje japo anajieleza kwamba zina manufaa kwa nchi. Dk Jakaya Mrisho Kikwete Kiwadhifa yeye ni askari. Kuna historia iliyomfanya awe askari na mpaka anajichomeka sawa katika siasa alikuwa ni Luteni Kanali.

Ndio kusema mpaka leo analazimika kuwa na tabia za uaskari ingawa nyingi ameziacha na kuwa msimamizi zaidi wa sheria, na pengine ni hili suala la kuwa askari linamponza kuwa mpole kwa kuona anaweza kuchukua hatua kubwa katika utekelezaji wa kazi zake na kuwaumiza wengine.

Tunapoingia katika uchaguzi Oktoba 31, tayari askari huyo ameshapokea rundo la matusi kutoka kwa watu wa mrengo wa kushoto na mengi hayafai kuyaeleza hapa. Ukomavu wake jeshini unampa maili nyingi zaidi katika kufuatilia matatizo ya wananchi na kupanga yanayowezekana na kuomba msaada pale inapobidi kama inapokuwa lazima ya kuhusisha msaada kutoka brigedi nyingine.

Hii unaiona anapokwenda safari za nje nyingi akiwa amelenga kutafuta msaada ili kusaidia kuokoa baadhi ya mambo yanayohitaji fedha nyingi katika nchi ambayo uchumi wake bado unategemea zaidi kilimo. Safari za kuomba msaada zilitokana na kuona ukweli kuwa bila kuomba msaada nyingi ya ahadi zilizolenga kuwakwamua wananchi hazitawezekana.

Alikuwa anafuata mtindo wa kawaida wa baba wa Kiafrika kuhemea inapobidi hasa nyumba inapokuwa na mapungufu. Kitu kingine ameacha watu wake waseme kuzoea mabadilishano ya lugha hata kama i kali ili kuwepo na sehemu ya kupumulia.

Hii ndio maana ya kupeleka watu renji, kuwaptia milio ya risasi na kupunguza munkari na kuweka saiti sawasawa. Akiwa anatafuta awamu ya pili ya uongozi staili yake ya kuomba kura ilikuwa tofauti na pengine hali hiyo inatokana na uzoefu wa kisiasa lakini zaidi ni namna utendaji kazi wa kijeshi unavyotakiwa kufanywa.

Akiwa mtu ambaye ameshapitia jeshini kazi ya kwanza ya mtu mwenye cheo kama chake ni kuhakikisha kwamba mapigano yanapelekwa kisayansi zaidi na kwa Jakaya Kikwete, kutaja mtu katika kazi ni dhambi, lakini kuangalia makosa ya wapiganaji na kuwapa nafasi ya kujipanga ni muhimu.

Ni makosa makubwa na ni kesi ya mahakama ya kijeshi kwa kiongozi kusababisha kusambaratika kwa vikosi kwa sababu ya kukosa plani ya mapigano. Kutokana na mafunzo ya kijeshi ipo sababu ya kumfikiri Kikwete kama mmoja wa viongozi wanaojali mustakabali wa askari wake katika vita.

Katika hili ni wananchi wa Tanzania ndio askari na kuruhusu watu wako kufa katika vita ni tatizo kwa hiyo ni lazima katika hili Kikwete aonekane ameshinda hasa katika ruzuku kwa wakulima, barabara za kufungua maeneo ya ndani, mfumo wa ushirika kufanyiwa kazi na kuanza kuiandaa Tanzania kuwa na viwanda vizito mama kwa ajili ya kusukuma kilimo na uchumi wa taifa.

Akiwa amezaliwa 7 Oktoba, 1950 katika kijiji cha Msoga, kata ya Lugoba, tarafa ya Msoga, Jimbo la Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani kutoka moja ya makabila madogo nchini la Wakwere, Kikwete ana maziwa ya siasa kutokana na babu yake Mzee Mrisho Kikwete kuwa chifu wa Wakwere na baba yake kufanya kazi katika wilaya za Pangani, Same na Tanga. Jakaya Kikwete alichukua digrii yake ya kwanza mwaka 1978 kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1978.

No comments: