Wednesday, February 24, 2010

SABUNI YA KICHINA YAHARIBU MAMBO


Honza alifanya uamauzi huo baada ya kutelekezwa na wake watatu kutokana na tatizo hilo, hivyo alitaka kuinusuru ndoa yake ya mke wa nne.

Honza, alisema alitumia dawa hiyo baada ya kupata ushauri kutoka kwa rafiki yake wa karibu Sebastian Mkwema ambaye aliwahi kuwa na tatizo hilo.

“Kwema aliniambia nimpe elfu 30 ili kupata dawa ya kukuza nyeti, ambapo baada ya siku tatu aliniletea dawa hiyo, nilianza kupaka na kuona nyeti zikiongezeka ndipo nilianza kupata furaha ya kuinusuru ndoa yangu.”

“Kumbe nilikosea masharti, ilikuwa nipake kwa muda wa siku mbili tu, mimi nilitumia kwa wiki nzima ambapo matokeo yake ni kama unavyoona sasa (akaonyesha) ni mzigo mkubwa hata suruali sivai na tendo la ndoa siwezi kufanya tena…

Kazi nilishaacha tangu Septemba mosi mwaka jana,” alisema.

Akizungumza kwa njia ya simu na Mtanzania, mke wa Honza, Nancy Kilungi, ambaye alimtelekeza mumewe baada ya nyeti hizo kuvimba na kufikia wastani wa kilo kumi, alijibu “Ndugu yangu ndoa ni unyumba …nitaishije ? Hakuniambia tatizo lake tangu awali na alishakimbiwa na wake watatu mimi ni wa nne.

Alikuwa na nyeti ndogo mithili ya kidole kidogo cha mkononi, tulishahangaika sana hadi waganga wa kienyeji bila mafanikio, alisema.

Hata hivyo, Mkwema ambaye kwa sasa amehamia visiwani Zanzibar, alikiri kumshauri Honza kutumia dawa hiyo ambayo alidai yeye ilimsaidia na sasa ndoa yake ina amani: ”Hee ndoa yangu ilikuwa inawaka moto. Mke wangu alikuwa anataka talaka jambo ambalo lilininyima usingizi , lakini Mungu si Athuman… jamaa fulani alinishauri kutumia ‘hypson’ sasa mambo si mabaya,” alisema.

Kwa upande wa familia ya Honza walisema jambo hilo ni la kusikitisha kwani amepoteza uwezo wa kufanya kazi amekuwa mtu wa kukaa nyumbani tu.”Yale yale ya akina Michael Jackson. Mungu anakuumba hivi, wewe unataka hivi na vile… tunafanya utaratibu wa kupata matibabu,” alisema mmoja wa familia hiyo.
Uchunguzi unaonyesha kuwa dawa zilizozalisha maafa haya ni kati ya zile zinazotajwa kuwa ni za Kichina.

CHANZO: MTANZANIA

No comments: