Wednesday, June 4, 2008

Miss anaswa!
Kukamatwa kwa mwanadada huyo kumekuja kufuatia taarifa zilizopelekwa polisi zikimtuhumu binti huyo kufanya vitendo vya kifuska huku akitembea na picha zinazomuonesha akiwa mtupu kwa lengo la kusaka wanaume.

Akiongea na mwandishi wetu, Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani hapa [R.C.O] Ahamed Msangi alithibitisha kukamatwa kwa chagudoa huyo huku akiiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa wahusika kwani tabia hiyo inadhoofisha juhudi za serikali za kupambana na ugonjwa hatari wa Ukimwi.

“Ni kweli baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema wakidai Vaileti James kabila Mmakonde kutembea na picha chafu kwenye pochi lake, niliwatuma vijana wangu ambapo Jumamosi iliyopita walifanikiwa kumnasa akiwa nazo baada ya kumpekuwa.

“Hata hivyo,tumemfikisha mahakamani na kesi yake ni namba 275 ya mwaka 2008 ambayo inatarajiwa kutajwa Mei 8 mwaka huu katika Mahakama ya Mwanzo Mazimbu,”alisema Msangi.

Awali mara baada ya binti huyo kukamatwa, Amani lilifanikiwa kuongea naye ambapo kwa mujibu wa maelezo yake alidai kuwa, mpenzi wake aliyemtaja kwa jina la Hassan ndiye aliyemlazimisha kuzipiga.

“Ni kweli nilipiga picha hizo lakini sio kwa nia mbaya, nilizipiga nikiwa nimelewa, lengo ni kwamba kule nyumbani Mtwara nina mchumba wangu anaitwa Hasani ambaye alinipigia simu akiomba nipige picha za hivyo kisha nimpelekee,”alisema dada huyo bila aibu.

Gazeti hili linalaani vikali vitendo vya upigaji picha chafu kwani licha ya kuwadhalilisha wahusika pia vinachochea kuenea kwa kasi kwa ugonjwa hatari wa Ukimwi.

No comments: