Friday, April 4, 2008

MAFURIKO DAR

Mkazi wa eneo la Tandale jijini Dar es Salaam (jina lake halikuweza kupatikana) akijaribu kutengegeza mfereji wa kuruhusu maji yaliyotuama kupita. Hiyo ni baada ya nyumba anayoishi kuzingirwa na maji mengi yaliyosababisha na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.
Moja ya nyuma zilizoathirika na mvua kubwa zinayoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam ikiwa imezingirwa na maji yaliyoingia mpaka ndani. Nyumba hii ipo maeneo ya Tandale jijini Dar es Salaam
Wakati mvua zinaendelea kunyesha jijini Dar es salaam uchafu nao unazidi kuongezeka na kutia hofu ya kwa wakazi wa jijini juu ya mlipuko wa magonjwa yanayosababishwa na uchafu kama picha hii inavyoonyesha leo jijini (Picha na Issa Mnally na RICHARD BUKOS).

No comments: