Thursday, December 13, 2007

NDOA YA FARAJA KOTTA KUFURU




Kufuru hiyo inatokana na sherehe hiyo kusheheni vigogo wa serikali na watu maarufu huku ulinzi wa 'kufa mtu' ukiwekwa kuzunguka ukumbi huo.

Miongoni mwa viongozi wa serikali waliokuwepo kwenye sherehe hiyo ni spika wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Samwel Sitta, Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Mhe. Ritta Mlaki pia alikuwepo mfanyabishara maarufu nchini Reginard Mengi pamoja na wageni wengine.

Mshereheshaji wa hafla hiyo alikuwa Mtangazaji wa ITV, Godwin Gondwe ambaye hakuwa nyuma kuhakikisha kila kitu kinakwenda kulingana na ratiba aliyokuwa nayo.

Gondwe alimuita mbele ya ukumbi huo spika wa Bunge kuongea machache kwa wanandoa hao.
Akiwa amelamba suti ya nguvu, spika aliitakiwa maisha mazuri ndoa hiyo na kumuagiza mbunge Nyalandu kwenda naye haraka bungeni mkewe ili kumtambulisha rasmi kama kanuni ya bunge inavyoagiza.

kwa mujibu wa spika, mbunge yeyote anapooa au kuolewa huyo mema “Huwezi kuamini kilichotokea katika hafla hii ya mheshimiwa kwani vinywaji vilivyokuwa vikigawiwa, vilikwisha katikati ya sherehe hali iliyosababisha ndugu wa bwana harusi kumtonja MC Godwin Gondwe kukatisha baadhi ya vitu vilivyo kwenye ratiba ili mambo yasije yakaharibika zaidi,” kilisema chanzo chetu.

Chanzo hicho kiliongeza kuwa, kwa kuhofia aibu zaidi ambayo ingeweza kuwapata waandaaji wa sherehe hiyo ambayo ilihudhuriwa na vigogo mbalimbali wa serikali, Gondwe aliamua kukata mambo mengine yaliyoainishwa kwenye ratiba ambayo yangelazimu sherehe hiyo kuchukua muda mrefu huku hali vinywaji vikiwa vimeisha, jambo ambalo lingeleta fedheha.

Katika fufunika funika ya mambo ukumbini hapo Gondwe alijikuta akilazimika kurukia kipengele cha mwisho cha ratiba ambacho kilikuwa kinamtaka Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samuel Sitta kwenda mbele ya ukumbi kuongea machache kwa wanandoa hao.

Akiwa amelamba suti ya nguvu, Spika aliitakia maisha mazuri ndoa hiyo na kumuagiza mbunge Nyalandu kwenda naye bungeni mkewe ili kumtambulisha rasmi kama kanuni ya bunge inavyoagiza.

Kwa mujibu wa Spika Bunge, mbunge yeyote anapooa au kuolewa anatakiwa kumpeleka mkewe au mumewe kwenye vikao vya bunge viwili mfululizo ili kumtambulisha kwa wabunge.

Baada ya Spika wa bunge kumaliza kutoa nasaha zake kwa wanandoa hao, alirudisha kipaza sauti kwa Gondwe ambaye naye bila kufanya ajizi alitangaza kuwa huo ndio ulikuwa mwisho wa sherehe hiyo. Ndoa hiyo ilifungwa katika kanisa la Azania Front jijini, Dar es Salaam siku hiyo ya sherehe.

Hata hivyo, mwandishi wetu alipoongea na baadhi ya waalikwa mara baada ya habari za ndoa hiyo kutangazwa kwenye vyombo vya habari wengi walioonekana kuwatabiria maisha marefu. "Unajua hawa ni tofauti na watu wengine maarufu ambao ndoa zao hugubikwa na migogoro ya mara kwa mara kwani wotre wamempokea Yesu Kristo yaani wameokoka , alisema mmoja wa nwatu waliohudhuria ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini. gazeti hili linawapongeza wanandoa hao na kuwatakia maisha marefu.

No comments: