Friday, November 23, 2007

Uchunguzi Wa Computer

Pengine umewahi kuota sikumoja unaweza kufanya uchunguzi kidogo katika computer yako au computer ya mtu mwingine , kujua alifanya nini , vitu anavyoweka katika computer yake na mambo mengine kuhusu computer yake si ndio ?


Leo nitakuonyesha njia chache ambazo unaweza kuzitumia kufanya uchunguzi mdogo katika computer yoyote ambayo utakutana nayo , kumbuka njia hizi zinatumika kwa bidhaa za Microsoft windows pekee .

Kabla ya kuanza maelezo haya kuna mambo muhimu ambayo mwenye computer anatakiwa awe anayajua au kuyatambua yeye kama mmilihi halali au mtumiaji wa computer husika nayo ni .

UTAMBULISHO

Right Click katika my computer , utaona general katika general utaona maelezo ya mwanzo kabisa kama aina ya operating system kama ni windows xp au 2000 , imesajiliwa kwa nani , aina ya CPU spidi yake , na ram iliyokuwepo katika computer hiyo

Kuna computer name hapo utaona jina la mwenye computer unaweza kubadilisha jina hili na kuweka jina lingine au kama utataka kujiunga na workgroup au domain Fulani makazini kwako hapo ndio pakuanzia , kubadilisha jina kunafanyika kama una mamlaka hayo yaani kama umelogin na account ambayo ina administrator Status kama sio administrator basi hutopata nafasi hiyo kamwe .

Ukifungua hardware kuna device manager hapo utaona hardware zote zilizochomekwa katika computer yako pamoja na driver zake kama ziko installed hapo na zinafanya kazi .

Kwa ufupi ukitaka maelezo ya kina ambayo hayahitaji sana utaalamu tafuta programu inaitwa Belarc Adviser au DriveMagician programu hizi ukitumia utaweza kuona hardware zote zilizomo ndani pamoja na watengenezaji wa vifaa hivyo na programu zilizomo ndani ubaya wake ni kwamba zitaonyesha mpaka licence za programu hizo maana yake mtu anaweza kuiba hizo licence au keys na kwenda kutumia kwingine kwa raha zake .

MAELEZO YA ZIADA


Kwanza fungua my computer – tools – folder options – view – show hide files and folders kuna baadhi ya watu wanapenda kutumia hatua ya hide kuficha folder na files zao ingawa njia hii ni ya kizamani kidogo kwa sababu kuna programu maalumu za kulock file au folders au file .

Njia hiyo ya hapo juu unaweza kufanikiwa kujua kama file zilizofichwa ukazipata , ila kama mtu alitumia programu maaalumu kulock hiyo folder hata ukiona huwezi kuifungua hapo ndio zinahitajika jitihada zingine ingawa kuna njia zaidi za kuweza kupata hizo file au folder .

Pili fungua my computer – fungua drive c (kama operating system iko drive c ) - Documents and settings – ( utakuta account nyingi kama computer yako unatumia jina mwehu basi utaona mwehu , la msingi wengi wanapenda kutumia administrator au user ) kama ni user fungua user – fungua templates ( utaona programu alizofungua muda mfupi uliopita au anazopenda kufungua au kutumia kumbuka usipofanya show hidden folders hutoweza kuona templates .

Hapo hapo katika user fungua My Recent Documents , ukifungua hiyo pia utaona files alizokuwa anatumia mtuhumiwa kwa kipindi kifupi kilichopita , pamoja na folder alizofungua , kama alichomeka flashdisk basi jina la flash disk utaliona pale au kama alichomeka kifaa chochote historia nzima utaiona pale pale .

Kuna cookies ,ambayo inapatikana katika user mara nyingi cookies ina maana kama computer husika huwa inatumia mtandao au imeunganishwa na mtandao , hapo utaweza kuona cookies na link fupi za tovuti ambazo mhusika amewahi kutembea au ambazo huwa anatembelea .

Watu wengine hupenda kuhifadhi link ya tovuti wanazotembelea katika browser zao , kwahiyo ukifungua favorites utaweza kuona link hizi za tovuti na kama mtu huyo anapenda kutembelea tovuti za ngono , au ambazo sio salama basi utaona hapo kwa sababu tovuti za hivyo huwa zinafanya hijack na kujihifadhi zenyewe kilazima .

Local Settings
Ndani ya local settings kuna Application Data , History , Temp ,Temporary Internet Files ,ukifungua history utaweza kuona tovuti zote alizowahi kutembelea mtuhumiwa na kama alikuwa anamtindo wa kuhifadhi password zake katika computer husika basi unaweza kufungua mpaka email zake na nyaraka zake zingine kwa kuwa zitakuwa zinafunguka moja kwa moja na ni rahisi kutumia programu zingine kuweza kutambua password husika .

Ukifungua Temporary Internet Files utaona file na programu zilizopatikana katika tovuti husika alizotembelea , mara nyingi hapo utakuta vitu haswa picha nakadhalika , pia virus huwa wanaanzia hapa katika folder hili , spyware na uchafu mwingine wa mtandao chanzo chake kikuu ni katika Temporary Internet Files .

Kama wewe ni mtumiaji wa windows 2000 kuna folder moja linaloitwa Recent hapo utaweza kupata mambo ya ziada kuhusu mtuhumiwa .

TAHADHARI

Maelezo ya hapo juu sio ya uhakika sana kwa sababu kuna programu za kuweza kufuta yote hayo kwa sababu huwa yanajaza computer na kusababisha ufumbufu mwingine kwahiyo ukikuta mtu ametumia programu ya kuondoa temporary Internet Files basi umeuwawa au programu ya Diskclean up basi napo umechemka .

Hata wewe unaweza kufuta baadhi ya vitu hivi

Start – Accessories – System Tools – Diskclean up – click Ok

Kisha kuna popup itakuja imeandikwa Disk Clean up for ( C) kama operating system yako iko Drive D basi chagua d na kadhalika , kuna programu zinazoweza kukusaidia na shuguli hii kama ccleaner , hijackthis na zingine nyingi zilizoko mitaani .

Utaona maelezo na cha kufanya kama unataka kufuta hizo files kwahiyo unaweza kuponyoka hapo kazini kwako kama unataka IT wetu asijue unafanya nini na umetembelea tovuti gani hapo unazifuta tu kiulaini .

Kuna sehemu zingine wanatumia server maalumu za kuhifadhi vitu ( BACKUP ) hii ina maanisha hata kama ukifuta au ukiformat Computer yako vile ulivyofanya vinakuwa viko katika hiyo server kwa ajili ya kumbu kumbu za baadaye kama chochote kikitokea , labda usijiunge na Domain ya Network husika ili usiwe unafanya backup na hiyo ni ngumu sana .
Hayo ni maelezo mafupi kuhusu uchunguzi na ndio mwanzo wake ingawa kuna programu maalumu zinaweza kutumika kuweza kuridisha vyote ulivyofuta na kuruhusu uchunguzi kuendelea kama kawaida .

Kuna wengine wanafikiri kufuta HDD ni suluhisho , siku hizi sio suluhisho hata ukifuta partition kuna programu za kuweza kurudisha pertition hizi pamoja na data zake ili ziweze kutumika hapo mbeleni au ziweze kutumika kama ushahidi mambo yanavyoweza kwenda kombo .

Katika kutumika kama ushahidi sijui kama Tanzania kuna sheria hizi za kutumia vifaa vya electroniki na kuwasilisha ushahidi mahakamani au la kama hamna basi ndipo tunapoelekea huko tujiandae kikamilifu

Kwaheri

No comments: